Mmewahi kukumbana na uchawi wa kusahaulishwa

Kuna mmoja alimloga baba mwenye nyumba wake jamaa akasahau nyumba yake kwa miaka 8

Kimara mwisho hii kitu though ni hear say
Mkuu kule ununio kuna mama mmoja aliachiwa nyumba akae, yeye akafanya yake sasa wenyewe kila wakija wanaipotea nyumba yao. Siku ya siku sijui dawa ziliisha nguvu au nao walitumia ndumba walipofika tu kwenye nyumba yao gari ikapata pancha wakaingia ndani alafu wakamfurusha yule mama.

Kwa hasira na nyumba wakaamua kuiuza.
 
Ndio maana yake hiyo hakuna mashtaka tena juu yako
Mkuu file kabla halijaenda mahakaman linachapishwa Kwanza inamaana copy yake inakua ipo mpelelez wa kesi anakua na ushahid mwng sana wa kukutia hatiani hizo kes ni mbaya Sana, we bora umtandike mtu mtaan umjeruhi siku ya kesi ndo umloge asahau kuja mahakamani ila hizi kes unazo shtakiwa na jamuhuri hizo hazipanguliwa kwa uchawi peke yake lazma umwage na pesa hapo
 
Uchawi haupo,uchawi ni akili zako.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] duh kumbe pale ununio kuna mambo ya kutisha kiasi hichi bila shaka watakuwa wazee wa pwani pale

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kesi ya mauaji hustakiwi na ndugu wa marehemu unashtakiwa na jamuhuri mzee ustegemee hiyo dawa kufanya kaz labda umwage pesa huko mahakamani
Hebu nambie mkuu. Kesi ya mauaji iko mahakamani. Kila anayetakiwa kutoa ushahidi anakufa siku tatu kabla ya kutoa ushahidi.

Hata askari mpelelezi wa kesi kafa. Nani ataendeleza kesi? Lazima uachiwe huru fasta.
 
We jamaa Kama hujui kaa kimya....faili linaliwa na mchwa ata Kama liko kwenye sefu ya chuma....acha maneno Kama hujui kitu
 

Kipindi flani kuna kesi ya jinai ilikuwa inaendelea iko moto ushahidi umesimama sasa kwenye hukumu PP alishindwa kupanda kuonana na MH ..kila akipanda tumbo linakata linamvuruiga vibaya..akienda toilet hamna kitu..akirudi tu kwenye chamber hali inakuwa mbaya ghafla..ngoma ika hairishwa kama mara mbili hivi....majamaa wenzie wazoefu wakamfata wakamwambia ukikomaa unaweza kata moto hapo bora uwatafute ndugu wa mtuhumiwa uvute chako uyeyushe mambo usitoke kwa hasara..kweli mambo yakaisha.

Shenzi kabisa hayo mambo ya kichawi
 
Hii nishawahi kuona mkuu, zamani kuna binti mmoja wa kizaramo alikuwa na kesi nzito sana mahakamani...aliwekwa ndani kwa muda wa miezi kadhaa huku kesi ikiendelea mahakamani..
Ndugu zake walifatilia ile kesi mahakamani lakini wakaona hamna ndoto za kutoboa..wakapoteaga kama wiki moja hivi wakaenda huko kusini.. Walivyorudi yule binti mara ya mwisho anapelekwa mahakaman akaachiwa kwa dhamana na kesi ikaishia juu kwa juu.
 
Hebu nambie mkuu. Kesi ya mauaji iko mahakamani. Kila anayetakiwa kutoa ushahidi anakufa siku tatu kabla ya kutoa ushahidi.

Hata askari mpelelezi wa kesi kafa. Nani ataendeleza kesi? Lazima uachiwe huru fasta.
Labda uwauwe wote hapo utawavuruga ushahid utakosekana
 
Uchawi haupo,uchawi ni akili zako.
Miaka mitano nyuma niliamini hivyo. Hata Mungu aliponitahadharisha kwa ndoto juu ya mipango miovu ya giza juu yangu nilipuuzia.

Hata nyuzi zangu za miaka ya 2011 - 2014, kila nilipokuwa naona nyuzi za dizaini hiyo, niliishia kuwakashifu waleta nyuzi na kuwaambia Ni kwa kuwa hawana Yesu.

Leo hii sihitaji kuambiwa na mtu ili niamini kwamba uchawi una nguvu, na ukikosea ukampa nafasi shetani ndipo utajua kwa undani zaidi.

Unajua hadi unaweza sahaulishwa kusoma hata Biblia? Acha niishie hapa.
 
Umeona eenhh!!!!,Kumbe ishu ni wewe mwenyewe.Kwa hiyo uchawi haupo kwa wenyewe isipokuwa ni jambo binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…