Ni sawa dawa zinafanya kazi sana lakini Lazima utakuwa na umaskini flani hivi ndiyo gharama zake kwako mfanyaji. na pili ili ufanikishe hili zoezi unadhalilika sana, kama una moyo mwepesi huwezi ifanya, mfano uchome kidole gumba kwenye nyaa! kabla ya kuongea.....jamani!!!.
Si unaona mfano pale Mbwewe, kwa Ng'andu, kwa mkono, Msata nk, huko Uziguani hakuna Maendeleo ya watu na vitu, kama sehemu zingine za kuelekea Moshi! Mabasi pale hayasimami mpaka Korogwe! hata wasomi serikalini Mzigua, au Mzaramo hakuna, km wapo walikulia sehemu nyngine tu!
Madalali wakipata zile hela wana maisha flani hivi ya uhitaji sana, hata wakiwa na nyumba nzuri vipi! watoto wao hawafanyi vyema darasani wanaishia kutumia hela vibaya na kuwa Maskini mbeleni. kuna namna flani hivi ya kujitia umaskini.