Kuna bosi wetu mhindi alikua ana mtindo wa kuturudisha kwa gari hadi Victoria tulikua tunapita Kkoo almost daily.
Kuna siku gari ikapata pancha tukiwa hapo Kkoo. Tukasogeza gari pembeni kwenye uwanja wa nyumba ambayo wamiliki ni waarabu au wazenji.
Tukatoka kwenda kutafuta mtu wa pancha. Tumefika mbele bosi akasema tuwahi ofisini turudi baadaye, baadaye akasema kesho. Kesho akasema kesho.
Ikakata wiki.
Mkewe akatuhimiza tukamuonyeshe nyumba tukafunga safari, tumefika lile eneo mke akasema ngoja nikachukue vocha dukani, tulivyofika dukani akanunua soda tumekunywa tulivyomaliza akasema tuwahi nyumbani tutarudi kesho.
Mpaka naacha pale kazi ilikua miezi miwili lile gari halikufuatwa.
Miaka minne mbele work mate wangu ananiambia lile gari halikufuatwa. Ila mkipita Kkoo bosi atasema halafu pale niliacha gari langu, kesho nalifuata. Na hafuati.