Mmeziona Fursa za kusomeshwa Bure na KCB? Changamkia hizi short course nchi nzima

Mmeziona Fursa za kusomeshwa Bure na KCB? Changamkia hizi short course nchi nzima

Ngoja niifanyie kazi, inshallah.
 
Wasalaam

Nianze kwa kuwapongeza benki ya KCB kupitia KCB FOUNDATION kuanzisha program ya jiajiri ikiwa na lengo la kumpa ujuzi kijana ambaye hana ajira aweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi Program hiibwameshirikiana na chuo cha ufundi cha Veta.

Vijana wengi wapo mtaani na wengine wana elimu kubwa lakini kutokana na Kukosa ajira hata ujuzi wa mambo madogo madogo hawana. Ila kwa program hii itaweza kuwasaidia kufanya mambo mengine hata yake ambayo hawakuyasomea.

Nilikuwa nashauri kuwa kipindi vijana hawa watakapochaguliwa na kujiunga na kozi hizo waruhusiwe kubadili kozi ambazo hazikuorodheshwa kipindi wanatangaza program husika.

Nasema hivi kwa sababu kuna vijana kipindi wapo huku mitaani walianza kujifunza skills mbalimbali mfano graphic designs n.k ila walipoona tangazo hawakuona kozi ya graphics na kuamua kuchagua kozi zingine imladi apate nafasi.

Sasa kama kachaguliwa na tayari ana skills za labda hiyo graphics huku mtaani na hicho chuo alichochaguliwa kuna hiyo kazi basi waruhusiwe kubadili ili ajiendeleze zaidi kwenye hilo eneo kuliko kwenda kuanza kozi mpya ambayo hakuwa na interest nayo hapo kabla.

Vijana wasaidiwe na waendelezwe pale wanapoona vijana wanavutiwa na hicho kitu.

Pia hata wengine wakitaka kuama chuo kingine cha veta basi waruhusiwe kama hiyo kozi anayo taka kusoma ipo huko.

Mwisho natumaini taasisi, mashirika na serikali zitaendeleza program hizi ili vijana wapate ujuzi ili Taifa kikombolewe. Vijana ni nguvu kazi ya Taifa ni lazima kuwakomboa.
 
Back
Top Bottom