Mmezipata habari za ChatGPT? Automation inatishia ajira za watu

Thanks sana kiongozi
 
View attachment 2558617
Nilikuwa naandaa article ya weekend kakakosea, good thing huwa natumia GPT kuandaa template tu ila sio kila kitu, kwanza ni insult kuwaandikia watu newsletter kwa kutumia AI considering wanalipia
Jakuna insult yoyote ile, tukienda hivyo mwisho utasema ni insult kuwaandikia watu kwa kutumia computer badala ya kuandika kwa kalamu ya mkono
 
Hii kitu ina na ita tengeneza wajinga wengi.
"I fear the day when the technology overlaps with our humanity. The world will only have a generation of idiots." Albert Einstein
 
Google wamekuja na chatbot yao inaitwa AI chatbot ambayo pia inajulikana kama Bard

Lengo kushindana na ChatGPT iliyoanzishwa na kampuni ya Microsoft.

Marekani na Uingereza wameanza kuitumia

Patamu sana hapa vita vya teknolojia kati ya google na Microsoft 🔥🔥🔥
 

=
How to:
Code:
1. https://www.reddit.com/r/artificial/comments/11yd55r/gpt_4_google_search_ive_been_working_on/
=
2. https://chrome.google.com/webstore/detail/gpt4-for-google-search-an/bkkkaebljlanbmkbkajelmjgcmgaiapd/related
 

Imekaa poa sana. Hii ni zaid ya google.
 
Nakubali, wanadamu tuna akili, ila kwa ufanisi technology, machine na computer zinaweza kufanya makubwa zinapotengenezwa kufanya kitu fulani. Walisema mawingu ndio kikomo,ila sasa mawingu ni upeo wa macho tu; tunaweza kwenda zaidi hata ya mawingu yalipoishia. Ebu fikiria ikifika kipindi binadamu akiweza kutengeneza mfumo ambao unaweza kujitengeneza, kujifanyia marekebisho, kujichaji (kuhakikisha hauishiwi chaji), mfumo unaoweza kuwaza kama binadamu, unaweza kujiboresha kwa kujiongezea utaalamu, uwezo ama kujitengenezea mfumo ambao utaufanya kuwa bora zaidi. Unajaribu kuimagine hilo??? Yote haya binadamu anaweza kuyafanya kutengeneza kitu kama hicho, huenda hata sasa inawezekana, ila nadhani kuna Sheria za kudhibiti hivyo vitu... , kuna sheria na kanuni nyingi ambazo zinalenga kuhakikisha usalama na uhuru wa binadamu katika matumizi ya teknolojia hizi.

Kwa mfano, kuna sheria za kudhibiti uvumbuzi wa teknolojia ya silaha, ambazo zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kijeshi au kusababisha madhara kwa binadamu. Kuna pia sheria na kanuni zinazolenga kuhakikisha usalama wa mtandao na data, ambazo zinaweza kuhitaji kampuni za teknolojia kuweka hatua za usalama kwenye bidhaa zao.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya jinsi ya kudhibiti maendeleo ya teknolojia kama vile roboti na akili bandia-artificial intelligence. Wakati baadhi wanahofia kwamba teknolojia hizi zinaweza kusababisha madhara kwa binadamu, wengine wanaamini kwamba kudhibiti maendeleo haya kunaweza kuzuia maendeleo mazuri. Kwa hiyo, suala la kudhibiti teknolojia mpya bado linaendelea kujadiliwa katika jamii na katika ngazi ya serikali. Nahitimisha kusema kwamba inawezekana kuziongezea machine, computers na akili bandia uwezo zaidi ya binadamu wa kawaida, ila hilo litafanya ile kwetu...

Hapa nakubishia mazima kaka...
Ukumbuke huyo robort hajitumi pekeake mpaka awe controled na human mind.They can settle out a day without nothing if human does nothing to it.
 
Swezi kuiponda Techologia maana Ni uwanja Mpana sana Ila ukakasi uliopo kuhusu hii chat...Ni iko published Sana Ila bado tofauti sio kubwa na ggl so bado kwa Sasa Ila kwa mbeleni cjui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…