kama kichwa cha habari kinavyojieleza binafsi nimetumia sana chatgpt ila nilipo jaribu kutumia bard sikutaka kuendelea sana labda kutokana na mazoea niliokuanayo kutoka chatgpt, kwanza kilicho nifanya nisiendelee kuitumia ni kutokana na mfumo wake upo tofauti sana, hauneshi mada inazungumzia nini
Pili ni lugha chache sana inazozielewa
yapo mengi ila kama nilivyoelezea hapo mwanzo nimeshindwa kuendelea kuitumia naona bado ipo nyuma sana kulinganisha na chatgpt ingawa chatgpt inadata za 2021 ila ni helpful sana
kwa mlioitumia mnaweza kutuambia ubora wake upo wapi
NOTE: Sijasema kuwa haifai wala haina uwezo bari hayo ni maoni yangu binafsi kulingana na matumizi yangu, na inaweza kuwa bora zaidi ya chatgpt kwa hilo msiniquote vibaya.
View attachment 2618892