TANZIA Mmiliki wa baa maarufu Magomeni, Hussein Macheni ameaga dunia ghafla nyumbani kwake

Huwa hakuna kulala pema wala pabaya
Ukifa ndio imetoka hivo hakuna tutalofanya libadili kifo au matendo yako kabla ya kifo
 
Hii bar si iliyozaa jina la KWA MACHENI?
Alitwa Macheni sababu ya kuvaa minyororo enzi hizo nasikia kwanza alikuwa baharia kabla ya kuanza kuendesha night club,na bendi alikuwa kama meneja bendi ilikuwa ya jamaa wa PPF
 
huyu jamaa ni mwenyeji wa wapi kwa anaefahamu/
 
Pole Kwa Ndugu, jamaa na marafiki. Nakumbuka nilikuwa nakatiza asubuhi nikiingia zangu skuli Azania, asubuhi saa moja nakuta bado kuna mtu kibao zinapata mambo. Kwa Macheni kweli enzi hiyo.

Pumzika Kwa Amani Hussein.
 
Jana nilimuona Mbezi beach, nikawa najiuliza hii sura nimeiona wapi.
Baada ya dakika kama tano nikamkumbuka. Alikuwa anapiga monde akiwa na rafiki yake mishen town mmoja
aliyekuwa Mbunge pamoja na mabinti wawili. Maisha mafupi sana.

RIP Macheni
true alikuwa hapo
 
Kwaheri Macheni ...last time nilimuona club Rouge kwenye disko la oldies...
 
Amemtumikia sana Lucifer,ngoja akapumzike.
Naam mkuu alikua anamiliki Bar maarufu sana magomeni, na aliwahi kua mmiliki wa Bendi ya muziki FM. Academia) pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…