Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich awekewa vikwazo na Uingereza

Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich awekewa vikwazo na Uingereza

Dah, mambo yamekuwa magumu mno, hii ni ishara ya kurudi tulipotoka
 
kuna msemo unasema mwaga ugali, namwaga mboga

Roman Abramovich awekewa vikwazo na Uingereza​

10 Machi 2022
TH

Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amewekewa vikwazo na serikali ya Uingereza kama sehemu ya majibu yake kwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.
Yeye ni mmoja wa wafanyabiashara saba matajiri kuwekewa vikwazo vipya, ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kwa mali yao na marufuku ya kusafiri.
Orodha hiyo pia inajumuisha mabilionea Igor Sechin na Oleg Deripaska, wote wanaoonekana kuwa washirika wa Vladimir Putin.
Waziri Mkuu Boris Johnson alisema "hakuwezi kuwa na maeneo salama" kwa wale ambao wameunga mkono uvamizi huo
 
Vita ya nini ikiwa vikwazo haviathili Urusi? Labda Urusi ianzishe vita kwasababu nyingine na si vikwazo.
Unaishi nchi gani, Waziri wa mambo ya nje wa Urusi kalamikia dhahiri hivi vikwazo akisema havijawahi kutokea, wewe uko humu unasema havina athari. Usifikiri hizi nchi zinaongozwa na wajinga.
 
Unaishi nchi gani, Waziri wa mambo ya nje wa Urusi kalamikia dhahiri hivi vikwazo akisema havijawahi kutokea, wewe uko humu unasema havina athari. Usifikiri hizi nchi zinaongozwa na wajinga.

Mimi nimekoment kwa niaba ya pro Urusi.
Furthermore ngoja waje wakuambie midia za magharibi zinakudanganya kuhusu athali za vikwazo. putin alijipanga mapema hadi pesa ya kuendeshea serikali aliziweka kwenye cryptocurrency kabla hajavamia Ukraine😊😊
 
Back
Top Bottom