tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe huujui ukubwa wa serengetiGari lichomwe ad kuteketea tena kwenye hifadhi bila askar Wa wanyama pori kugundua wala kutouona moshi!?
Alafu wanajisifu kwa kupambana na majangili.
Mungu hailaze mahali pema roho ya marehem.
Lini sasaWakipatikana hao watuhumiwa naomba mnitagi!
Kwa hiyo tz ujambazi ulishaisha ?Watu wasiojulikana hao.
Hii ndio TZ ya sasa. Mtu wiki mbili hapatikani kisha maafa ju yake
Mshana hebu ieleze hii picha kidogo hata kwa ufupiView attachment 709152
Rest in peace
....Unauliza hili swali as if hujasoma huu uzi, sasa hapa unafanya nini?kachomewa kwenye gari lake au amewawa tuu nagari kuchomwa moto pembeni??
Walikuwa bussy na matamko kuhusu dogo aliyetekwaAskari walikua wapi mda wote Wote huo
na wewe acha kuropoka ropoka apa huna habari kamili tulia sio kusema unasikia halafu huna uhakikaNasikia alikuwa anawafadhili chadema
Laiti kama angetupwa baharini waziri wetu angelisema si mtanzania.View attachment 708766View attachment 708767![]()
View attachment 708768
Mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah maarufu kama Super Sami au mmiliki wa mabasi ya Super Sami amefariki. Ni baada takribani wiki mbili zilizopita alikuwa hapatikani hewani wala kujulikana alipo. Amekutwa amekufa Serengeti na gari lake limechomwa moto.
========
Mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah ametoweka kwa zaidi wiki mbili sasa gari lake aina ya Toyota Landcruizer kukutwa likiwa limechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara.
Gari hilo lililokutwa likitumiwa na mfanyabiashara huyo ambaye ni mkazi wa Mwanza, lilikutwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara jana likiwa limeteketea kwa moto.
Ofisi habari wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa), Mustapha Mwalongo, aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kuwa mfanyabiashara huyo licha ya gari lake kukutwa limeteketea moto, hawakukuta mabaki ya mwili wake.
"Gari lake limeteketea kweli lakini hatujabaini mwili kama na yeye alikuwa kwenye gari lile kwa sababu waliofika eneo la tukio hawajakuta mwili au mabaki ya mwili ya aina yeyote", alisema Mwalongo.
Alisema baada ya mmiliki huyo wa mabasi kutoweka tangu Machi Mosi, Kamati iliundwa ya kufuatilia sababu za kutoweka kwake na wapi alipo ambayo inashirikiana na familia.
"Kamati ilipopata taarifa kuwa kuna gari limeteketea kule Serengeti, walishirikiana na Jeshi la Polisi kwenda hadi eneo la tukio na kubaini kweli ni gari lake lakini hawajabaini kama alikuwepo mle wakati linachomwa", alisema Mwalongo.