Mmiliki wa Shule za Tusiime jitafakari na uwalipe wafanyakazi stahiki zao

Mmiliki wa Shule za Tusiime jitafakari na uwalipe wafanyakazi stahiki zao

DolphinT

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2016
Posts
2,014
Reaction score
2,979
Kwa kile ambacho hakikutarajiwa na wengi Ni suala la wamiliki wa Shule za Binafsi ikiwemo Tusiime ambayo inamiliki Tusiime nursery, primary na secondary kukaidi kulipa mishahara ya watumishi wake wakiwemo walimu.

Mmiliki wa Tusiime aliitisha kikao na wafanyakazi mnamo tarehe 17/4 kwa nia ya kuwaeleza wafanyakazi wake wote Nia yake ya kupunguza wafanyakazi, kuvunja mikataba pamoja na kutolipa mishahara kwa mwezi April na kuendelea.

Watumishi walipinga vikali ajenda hiyo na akaamua kupendekza ajenda ya wafanyakazi 500 kuwa na wawakilishi 50 ambao watakaa kikao kingine ili kujadili na kuamua hatma ya stahiki za watumishi

Vikao vyote alihakikisha anakua na mwanasheria ambae atatetea maslahi yake na hakuwapa wafanyakazi nafasi ya kuwa na mwanasheria au kiongozi wa chama Cha wafanyakazi.

Katika kikao Cha pili aliwashawishi wafanyakazi wasiokua walimu kukubali na ajenda yake ya kutolipa mishahara na kuwataka kuchukua likizo Bila malipo, kwa kutumia ushawishi huo watumishi (auxiliary) ambao wengi ni wahaya wakaunga mkono na hivyo hatma ya wafanyakazi kuamuliwa kwa Kura.

Walimu wa sekondari hawakuridhia uamuzi huo na kuamua kukutana ili kupata mastakabali wao. Baada ya Taarifa hizo kumfikia Ndugu Albert (Mmiliki) aliomba polisi wa kutuliza ghasia kutoka kituo Cha Staki Shari ili kuwadhibiti walimu hao wasikusanyike ili kunadiliana kuhusu mustakabali wao katika eneo lilokubaliwa na kwa bahati nzuri walimu hawakukutana!

Baada ya hapo ameandaa fomu maalum ya likizo Bila malipo na kuwaita wafanyakazi kimya kimya ili wasaini huku akiwapa malipo ya tsh laki Moja na nusu(rushwa) ambao watakubali!

Ikumbukwe kwamba baada ya agizo la kufungwa Shule kwa siku 30 wafanyakazi walitakiwa kujaza fomu za likizo, je inawezekana kisheria ndani ya mwezi mmoja kuwe na likizo, halafu likizo Bila malipo?

Walimu Hawa wanalipa PAYE Kila mwezi, walimu Hawa wanatoa mchango kwa serikali katika utoaji elimu Kama sekta Binafsi.

Serikali na vyombo vyake vimwagize Mr Albert Katagira alipe mishahara ya mwezi April na May haraka! Na pia vikao vyote alivyofanya viamuliwe Ni batili kisheria!

Baada ya hapo aone Ni namna gani atahakikisha wafanyakazi wake wanaishi katika kipindi hiki Cha Covid

Serikali imfanyie ukaguzi katika mapato na matumizi yake kwani hi ni Tusiime holdings kwa maana hiyo Ni group of companies. Kabla uchafu wake mwingine haujaanikwa hadharani. T
 
Walimu Hawa wanalipa PAYE Kila mwezi, walimu Hawa wanatoa mchango kwa serikali katika utoaji elimu Kama sekta Binafsi.
Serikali na vyombo vyake vimwagize Mr Albert Katagira alipe Mishahara ya mwezi April na May haraka! Na pia vikao vyote alivyofanya viamuliwe Ni batili kisheria!
Kama hawajaridhika na maamuzi hayo wapeleke malalamiko yao kwenye tume ya usuhishi wa migogoro ya ajira baina ya mwajiri na mwajiriwa.
 
Poleni saanaa ndugu waalimu na wafanyakazi wa shule za private kwa ujumla

Cha msingi ni kuwa wavumilivu na kutafuta njia mbadala ya kuishi katika hili janga litapita na ajira zenu zitaendelea kama kawaida.

Kuwen makin sana kuepusha migogoro isiyo ya lazima kwa janga la mpito.

Sio tusiime tùuu ni shule nyingi saana za private zinapitia the same situations.

Mimi binafsi tangu janga la korona sijawalipa watumishi wangu wa katushen center kangu.

Tawalipa nini wakati wanafunzi hawaji kulipa ??

Tusiime pia ada wanalpa in phases. Three month phases. Sasa mwezi wanne alitegemea akuaanye ada ili awalipe. Ndio hivyo tena kovid imetukatili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni saanaa ndugu waalimu na wafanyakazi wa shule za private kwa ujumla

Cha msingi ni kuwa wavumilivu na kutafuta njia mbadala ya kuishi katika hili janga litapita na ajira zenu zitaendelea kama kawaida.

Kuwen makin sana kuepusha migogoro isiyo ya lazima kwa janga la mpito.

Sio tusiime tùuu ni shule nyingi saana za private zinapitia the same situations.

Mimi binafsi tangu janga la korona sijawalipa watumishi wangu wa katushen center kangu.

Tawalipa nini wakati wanafunzi hawaji kulipa ??

Tusiime pia ada wanalpa in phases. Three month phases. Sasa mwezi wanne alitegemea akuaanye ada ili awalipe. Ndio hivyo tena kovid imetukatili

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa tution una haki ndio maana wanafunzi wanalipa mara nyingi kitopic au ki mwezi.
Sasa shule nyingi tena kubwa kama hizo wazazi hulazimishwa lipa ada ya nusu mwaka au mwaka mzima kabisa.Wachache sana wanalipa robo mwaka.

Kumbuka sa hivi hakuna hata mwanafunzi shuleni hivyo hakuna utumiaji wa chakula umeme au maji kam wanafunzi wanapokuwepo. Hivyo angalau wangewambia walimu wanawalipa nusu au robo mshahara hadi mwezi June ambako ndo mwisho wa nusu mwaka.

Anyway kuajiriwa ni sehemu naona yakijinga sana na kuishi bila akiba ni mbaya sana
 
Ukivaa uhusika wa mmiliki utakuwa upande wa mmiliki,, Ukivaa uhusika wa walimu utakuwa upande wa mwalimu.

Ila ukweli ni hela hakuna,, so hata wakitaka kulipwa bado itakuwa ni deni.

BUT, Ni muda wa walimu kuchunga ndimi zao sana, Coz wakizembea wanaweza chezea Kazi na Mshahara
 
Poleni sana ndugu zetu walimu wa shule binafsi. Hakuna maumivu makali kama yale ya kuishi bila pesa ya kuendeshea maisha! Mbaya zaidi uwe na familia inayokutegemea, halafu hukujiandaa kukabiliana na hiyo hali ya ukata.

Ahueni kwa wale walimu wanaoweza kujibanza sehemu kwa wakati huu wa mpito! mfano kwa wazazi wao, waume/wake zao wanaofanya kazi sekta nyingine, marafiki zao, nk.
 
[Tusiime ajiongeze taasisi yake Ni household name pesa zote anazopata anapeleka wapi huwa anakula zote? Aajiri investment manager au financial controller ammsaidiae jinsi ya kuwekeza au atafute investment consultant s mbona wahaya wenzie wako kibao tu wamsaidie.
Walimu ndio capital yake kubwa asicheze nao.Mtaji wake sio pesa ,mijengo au migari ya shule Ni walimu

Napinga kwa nguvu zote kitendo Cha yeye kugusa walimu.Mtaji mkuu wa shule Ni walimu.Hata tuition nyingi mfano mwenge dar watoto wengi huenda kwenye vibanda umiza vya hovyo lakini vyenye vijana walimu wa kutisha wenye uwezo wake kufa mtu kwenye kufundisha masomo ya sayansi

Tusiime be careful with teachers hao Ni producers wa hela za tusiime sio consumers

Haiwezekani taasisi kubwa Kama Tusiime iyumbe na ipate economic shock muda mufupi hivi .

Ada akilipwa akishatoa matumizi huwa anazipeleka wapi? Zote anazifanya dividend yake au?
 
Wahaya wanashida yule wa St Anne maria hayohayo


Kukumweupe

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni rafiki take mkubwa na wanashauriana.
Wakati Alpha schools amekaa na watumishi wake na kukubaliana awalipe 50% na inayobakia iwe Deni yeye kwa aliposikia janga la Covid akaamua kuhamisha mpunga wa kutosha kwenda kwingine! Na kwakua anajua walimu wake Ni weupe kwenye financial statements akawaambia Ana mil 30 tu bank nao wakakubali kwa kusoma ile figure ya chini wajanja wakstuka, Asante Serikali kwa kumtokea Jana na hakikisheni account zake zote je Ni kweli hawezi kujiendesha hata mwezi mmoja? Mana huu Ni mwanya wa kuhujumu uchumi kwa kutopeleka PAYE.
 
Achen kulaumu hawa mamiliki.


Ni vema serikali ifanye kitu kwaajili ya kulinda Ajira za sekta binafsi hususani hawa walimu.


Kwan wazazi wote mmelipa Ada ya mwaka mzima wa masomo??..wapo wanaolipa kwa mafungu....


Sasa kama nayeye uchumi umeyumba afanyaje ??


Serikali itoe fungu, angalau nusu kisha wamiliki waongezee, ili Watu walindiwe ajira zao.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu ni mkombozi wa maisha, fika kwa mwenyewe binafsi mwambie mzee nikope kiasi kadhaa utanikata kwa mshahara hali ikiwa shwari.
 
Back
Top Bottom