Mmiliki wa Shule za Tusiime jitafakari na uwalipe wafanyakazi stahiki zao

Mmiliki wa Shule za Tusiime jitafakari na uwalipe wafanyakazi stahiki zao

Walimu vumilieni ni kitambo kidogo haya yatapita. Kwa kuwa ana historia ya kuwalipa kabla ya janga la korona mvumilie.
Hata shule zikifunguliwa mishahara mtacheleweshewa,kwani hao wazazi hawana pesa za kulipa ada.
 
Hapo St Anne Marie mshahara wa March miaka yote huwaga ni shida mshahara wa December nao ni shida wanalipwa robo robo mpaka shule zikifunguliwa.
Sasa pata picha kipindi hiki.
Hela huwa wanapeleka wapi hawa?

Wanahitaji kuwe na bodi ya kuregulate shule za binafsi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara chache sana TRA kukagua.
Mahesabu yanayopelekwa yanachezewa sana.
Mishahara ya wafanyakazi inapunguzwa sana ili kushusha PAYE idadi ya wanafunzi inapunguzwa.
Hakuna link kati ya maaafisa wa elimu na TRA kungekuwa kuna link huu wizi wao. TRA ingewashtukia.
Kwani uwa haikaguliwi ? Na maofisa elimu na tra ?
 
Dah, ila haya mambo yanazidi kuwa magumu kweli kweli
Poleni saanaa ndugu waalimu na wafanyakazi wa shule za private kwa ujumla

Cha msingi ni kuwa wavumilivu na kutafuta njia mbadala ya kuishi katika hili janga litapita na ajira zenu zitaendelea kama kawaida.

Kuwen makin sana kuepusha migogoro isiyo ya lazima kwa janga la mpito.

Sio tusiime tùuu ni shule nyingi saana za private zinapitia the same situations.

Mimi binafsi tangu janga la korona sijawalipa watumishi wangu wa katushen center kangu.

Tawalipa nini wakati wanafunzi hawaji kulipa ??

Tusiime pia ada wanalpa in phases. Three month phases. Sasa mwezi wanne alitegemea akuaanye ada ili awalipe. Ndio hivyo tena kovid imetukatili

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kiukweli watu wa haki za binadamu hapa kwa wa ajili private wanachezea sana haki za wafanyakazi. mkatabab siku zote unatakiwa uheshimike pande zote (mwajiri na mwajiriwa). mara nyingi mwenye haki ya kuheshimu mkataba n mwajiriwa (uelewa wa wengi kirahisi). private unasaini mkataba ukiwataka kulipa mshahara kila tarehe 23 ya kila mwezi wenye makato ya PAYEE TRA na mifuko ya jamii. mwajiri huyo huyo analipa mshahara tarehe atakayojisikia, walio private wengi huwa wanaielewa sana tarehe 40, maana huwa wanaisubiri sana japokuwa ni haki yao inayotakiwa kulipwa mapema. katika mikataba mingi haionyeshi sehemu ya majanga na kwamba kwa janga hili la covd 19 ni stahiki yao kulipwa kwa mujibu wa mikataba ya walio wengi (rejea mkataba wako).
Waajiri private ni muda wa kujitafakari je mikataba uliowapatia wafanyakazi wako unaeza itekeleza?
unakuta taasisi mf shule inachanzo kimoja tu cha mapato""'"""""''.... uzembe kama huu kwa waajiri wengi lazima ilete shida kwenye utekelezaji wa mikataba.
ushauri wangu kwa waajiri,, kipindi hiki cha covd 19 iwe sehemu ya kujifunza kuhakikisha msitegemee pesa za wanafunzi pekee.
ukifuatilia vzr kwa taasisi zinazocheza na mishahara kipindi hk cha covd utabaini waajiriwa wanadai pesa nyingi ambazo wamekuwa wakiishi kwa kuahdiwa///
 
Hii familia ilitumia bilioni kwenye harusi ya mwanae, kumbe ilikuwa show off kwanini hataki kulipa stahiki za wafanyakazi wake?
 
Back
Top Bottom