Mmiliki wa Shule za Tusiime jitafakari na uwalipe wafanyakazi stahiki zao

Mmiliki wa Shule za Tusiime jitafakari na uwalipe wafanyakazi stahiki zao

Kwa kile ambacho hakikutarajiwa na wengi Ni suala la wamiliki wa Shule za Binafsi ikiwemo Tusiime ambayo inamiliki Tusiime nursery, primary na secondary kukaidi kulipa mishahara ya watumishi wake wakiwemo walimu.

Mmiliki wa Tusiime aliitisha kikao na wafanyakazi mnamo tarehe 17/4 kwa nia ya kuwaeleza wafanyakazi wake wote Nia yake ya kupunguza wafanyakazi, kuvunja mikataba pamoja na kutolipa mishahara kwa mwezi April na kuendelea.

Watumishi walipinga vikali ajenda hiyo na akaamua kupendekza ajenda ya wafanyakazi 500 kuwa na wawakilishi 50 ambao watakaa kikao kingine ili kujadili na kuamua hatma ya stahiki za watumishi

Vikao vyote alihakikisha anakua na mwanasheria ambae atatetea maslahi yake na hakuwapa wafanyakazi nafasi ya kuwa na mwanasheria au kiongozi wa chama Cha wafanyakazi.

Katika kikao Cha pili aliwashawishi wafanyakazi wasiokua walimu kukubali na ajenda yake ya kutolipa mishahara na kuwataka kuchukua likizo Bila malipo, kwa kutumia ushawishi huo watumishi (auxiliary) ambao wengi ni wahaya wakaunga mkono na hivyo hatma ya wafanyakazi kuamuliwa kwa Kura.

Walimu wa sekondari hawakuridhia uamuzi huo na kuamua kukutana ili kupata mastakabali wao. Baada ya Taarifa hizo kumfikia Ndugu Albert (Mmiliki) aliomba polisi wa kutuliza ghasia kutoka kituo Cha Staki Shari ili kuwadhibiti walimu hao wasikusanyike ili kunadiliana kuhusu mustakabali wao katika eneo lilokubaliwa na kwa bahati nzuri walimu hawakukutana!

Baada ya hapo ameandaa fomu maalum ya likizo Bila malipo na kuwaita wafanyakazi kimya kimya ili wasaini huku akiwapa malipo ya tsh laki Moja na nusu(rushwa) ambao watakubali!

Ikumbukwe kwamba baada ya agizo la kufungwa Shule kwa siku 30 wafanyakazi walitakiwa kujaza fomu za likizo, je inawezekana kisheria ndani ya mwezi mmoja kuwe na likizo, halafu likizo Bila malipo?

Walimu Hawa wanalipa PAYE Kila mwezi, walimu Hawa wanatoa mchango kwa serikali katika utoaji elimu Kama sekta Binafsi.

Serikali na vyombo vyake vimwagize Mr Albert Katagira alipe mishahara ya mwezi April na May haraka! Na pia vikao vyote alivyofanya viamuliwe Ni batili kisheria!

Baada ya hapo aone Ni namna gani atahakikisha wafanyakazi wake wanaishi katika kipindi hiki Cha Covid

Serikali imfanyie ukaguzi katika mapato na matumizi yake kwani hi ni Tusiime holdings kwa maana hiyo Ni group of companies. Kabla uchafu wake mwingine haujaanikwa hadharani. T
Huyu mtamuonea tu. Geukieni mifuko yenu ya hifadhi ya jamii iwasaidie. Huu ndio muda wa mifuko hiyo kuwahifadhi wachangiaji wake.

Tusiime alipe pesa kutoka wapi wakati mnajua kabisa malipo yenu yanatoka kwenye ada za wanafunzi na wanafunzi hawapo? Kwa umoja wenu ombeni nssf iwahifadhi kupitia michango yenu.
 
Hapo cha msingi serikali itoe fao la kujitoa kwa waajiriwa secta bnafsi wote waliotemeshwa mzigo,ila kwa serikali za kiafrica msitegemee serikali kutoa luzuku kwa sclecta bnafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
The only solution ni hii mifuko kuwapa watu kilicho chao hata kwa uchache ili kiwstunze. Umenena vyema sana
 
Ukivaa uhusika wa mmiliki utakuwa upande wa mmiliki,, Ukivaa uhusika wa walimu utakuwa upande wa mwalimu.

Ila ukweli ni hela hakuna,, so hata wakitaka kulipwa bado itakuwa ni deni.

BUT, Ni muda wa walimu kuchunga ndimi zao sana, Coz wakizembea wanaweza chezea Kazi na Mshahara
Kama mshahara wa mwezi wa tatu amewalipa basi atakuwa na nguvu ya kujitetea maana kwa mwezi wa NNE ni robo ya pili ambayo wazazi walio wengi hawajalipa ada!! Kuna shule ambazo hata mwezi wa tatu hawajalipwa kwa kisingizio cha kufungwa shule wakati wazazi walishalipa ada yote kwa robo ya kwanza.

Serikali iliangalie hili. Napendekeza serikali izikopeshe pesa shule za binafsi ili ziweze kulipa mishahara. Shule zikifunguliwa wazazi watalipa ada na shule zitalipa deni serikalini.
 
N
Siwezi kulipa akati sina hela, walimu mvumilie tu
Njaa haivumilii!! Ndio maana propesa lipumber alitengua barua yake na kukirudia tena kigoda cha kafu!! Chezea njaa weye!! Hali kadhalika Dr mihogo, Dr Kushinjy nk
 
Hivi baada ya corona kwisha wazazi watalipa full school fees wakati kuna siku kede kede watoto hawapo shuleni na hawafundishwi au kutumia resources za shule?
Lazima walipe full school fees maana watafundishwa full syllabus! Waalimu hawawezi kuruka mada ambazo zilikuwa zifumdishwe April! Mwanafunzi hawezi kufundishwa mada za juu kabla ya za chini.
 
Achen kulaumu hawa mamiliki.

Ni vema serikali ifanye kitu kwaajili ya kulinda Ajira za sekta binafsi hususani hawa walimu.

Kwan wazazi wote mmelipa Ada ya mwaka mzima wa masomo??..wapo wanaolipa kwa mafungu....

Sasa kama nayeye uchumi umeyumba afanyaje ??

Serikali itoe fungu, angalau nusu kisha wamiliki waongezee, ili Watu walindiwe ajira zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Well said mkuu ...

One love
 
Lazima walipe full school fees maana watafundishwa full syllabus! Waalimu hawawezi kuruka mada ambazo zilikuwa zifumdishwe April! Mwanafunzi hawezi kufundishwa mada za juu kabla ya za chini.
Kama ndivyo mbona nasikia kuna baadhi ya shule za binafsi walimu wameangua kilio baada ya kupewa likizo ya bila malipo au wanafunzi wakirudi hao walimu watapewa mishahara dabo dabo?
 
Kwa kile ambacho hakikutarajiwa na wengi Ni suala la wamiliki wa Shule za Binafsi ikiwemo Tusiime ambayo inamiliki Tusiime nursery, primary na secondary kukaidi kulipa mishahara ya watumishi wake wakiwemo walimu.

Mmiliki wa Tusiime aliitisha kikao na wafanyakazi mnamo tarehe 17/4 kwa nia ya kuwaeleza wafanyakazi wake wote Nia yake ya kupunguza wafanyakazi, kuvunja mikataba pamoja na kutolipa mishahara kwa mwezi April na kuendelea.

Watumishi walipinga vikali ajenda hiyo na akaamua kupendekza ajenda ya wafanyakazi 500 kuwa na wawakilishi 50 ambao watakaa kikao kingine ili kujadili na kuamua hatma ya stahiki za watumishi

Vikao vyote alihakikisha anakua na mwanasheria ambae atatetea maslahi yake na hakuwapa wafanyakazi nafasi ya kuwa na mwanasheria au kiongozi wa chama Cha wafanyakazi.

Katika kikao Cha pili aliwashawishi wafanyakazi wasiokua walimu kukubali na ajenda yake ya kutolipa mishahara na kuwataka kuchukua likizo Bila malipo, kwa kutumia ushawishi huo watumishi (auxiliary) ambao wengi ni wahaya wakaunga mkono na hivyo hatma ya wafanyakazi kuamuliwa kwa Kura.

Walimu wa sekondari hawakuridhia uamuzi huo na kuamua kukutana ili kupata mastakabali wao. Baada ya Taarifa hizo kumfikia Ndugu Albert (Mmiliki) aliomba polisi wa kutuliza ghasia kutoka kituo Cha Staki Shari ili kuwadhibiti walimu hao wasikusanyike ili kunadiliana kuhusu mustakabali wao katika eneo lilokubaliwa na kwa bahati nzuri walimu hawakukutana!

Baada ya hapo ameandaa fomu maalum ya likizo Bila malipo na kuwaita wafanyakazi kimya kimya ili wasaini huku akiwapa malipo ya tsh laki Moja na nusu(rushwa) ambao watakubali!

Ikumbukwe kwamba baada ya agizo la kufungwa Shule kwa siku 30 wafanyakazi walitakiwa kujaza fomu za likizo, je inawezekana kisheria ndani ya mwezi mmoja kuwe na likizo, halafu likizo Bila malipo?

Walimu Hawa wanalipa PAYE Kila mwezi, walimu Hawa wanatoa mchango kwa serikali katika utoaji elimu Kama sekta Binafsi.

Serikali na vyombo vyake vimwagize Mr Albert Katagira alipe mishahara ya mwezi April na May haraka! Na pia vikao vyote alivyofanya viamuliwe Ni batili kisheria!

Baada ya hapo aone Ni namna gani atahakikisha wafanyakazi wake wanaishi katika kipindi hiki Cha Covid

Serikali imfanyie ukaguzi katika mapato na matumizi yake kwani hi ni Tusiime holdings kwa maana hiyo Ni group of companies. Kabla uchafu wake mwingine haujaanikwa hadharani. T
Poleni sana kwa mkasa uliowakuta.
 
Unampaje m
Poleni saanaa ndugu waalimu na wafanyakazi wa shule za private kwa ujumla

Cha msingi ni kuwa wavumilivu na kutafuta njia mbadala ya kuishi katika hili janga litapita na ajira zenu zitaendelea kama kawaida.

Kuwen makin sana kuepusha migogoro isiyo ya lazima kwa janga la mpito.

Sio tusiime tùuu ni shule nyingi saana za private zinapitia the same situations.

Mimi binafsi tangu janga la korona sijawalipa watumishi wangu wa katushen center kangu.

Tawalipa nini wakati wanafunzi hawaji kulipa ??

Tusiime pia ada wanalpa in phases. Three month phases. Sasa mwezi wanne alitegemea akuaanye ada ili awalipe. Ndio hivyo tena kovid imetukatili

Sent using Jamii Forums mobile app
Fa
Unampaje mfanyakazi likizo isiyo na malipo na huku ada wazazi watalipa vilevile,kwanza at least angehesabu siku za mapumziko za mhula kama zimeisha ndio angekuja na hiyo plan maana hizi siku zitalipwa endapo janga litawai kuisha sasa huo si utakuwa utapeli yaan mwalimu atakuwa hajapata likizo yake ya malipo kama jinsi utaratibu ulivyo siku zote.

Haya kwa nini wasiingie makubaliano ya kurusha malipo kuwa watalipwa pesa zao baada ya miezi kadhaa mbeleni yaan kama deni.Huu ni utapeli tu kama ulivyo utapeli mwingine
 
Mmiliki hajafanya Biashara, mwajiriwa hajafanya kazi, badala tukomalie mifuko ya pension ilipe wafanyakazi kila mwezi, tunamlalamikia wamiliki wa shule...
 
Ndy biashara ina changamoto nyingi..mbinu ilikua ni kuwalipa mishahara hata ya miez miwili wapate where to start sio kuwatreat vile..hata trump ni Tajiri lakini historia yake alipata kuuza aset zake ili kampuni zisfe..ni swala la hesabu tu...
Aisee ...tuna safari ndefu sana! Kwahiyo auze mali zake sio? Wewe unaweza kuuza vyako kwaajili ya jirani yako tu mwenye njaa?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh kumbe biashara ya kumiliki shule nayo nipasua kichwa tu
 
Lakini hebu tuweni wakweli. Kama hazalishi kwa maana ya kuwa hakuna ada zinazolipwa kutokana na watoto kuwa katika likizo ya lazima ya Corona ambapo wazazi sasa hawalipi mmiliki wa shule atatoa wapi pesa za kuwalipa wafanyakazi wake?

Yeye mwenyewe kwanza hana hela na bado ata takiwa kulipa umeme na baadhi ya huduma kama ulinzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni saanaa ndugu waalimu na wafanyakazi wa shule za private kwa ujumla

Cha msingi ni kuwa wavumilivu na kutafuta njia mbadala ya kuishi katika hili janga litapita na ajira zenu zitaendelea kama kawaida.

Kuwen makin sana kuepusha migogoro isiyo ya lazima kwa janga la mpito.

Sio tusiime tùuu ni shule nyingi saana za private zinapitia the same situations.

Mimi binafsi tangu janga la korona sijawalipa watumishi wangu wa katushen center kangu.

Tawalipa nini wakati wanafunzi hawaji kulipa ??

Tusiime pia ada wanalpa in phases. Three month phases. Sasa mwezi wanne alitegemea akuaanye ada ili awalipe. Ndio hivyo tena kovid imetukatili

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini hakuforesee risks ambazo lazima ujue kwamba zipo? Aliyemwambia alipishe ada kwa awamu ni nani? Wakati anatengeneza faida alikuwa haweki akiba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Napendekeza serikali izikopeshe pesa shule za binafsi ili ziweze kulipa mishahara. Shule zikifunguliwa wazazi watalipa ada na shule zitalipa deni serikalini.

Hio riba kipindi wanarudisha hio hela ndio wamiliki wanaikwepa,, so ni bora wadaiwe na wafanyakazi wao kuliko wao kudaiwa na serikali,, labda kama watapewa bila riba..

Ki biashara faida ndio huangaliwa,, mambo ya ubinadamu hufuata baadae, (utu umeshuka bei, thamani ya pesa imepanda by, Fid Q)
 
Yale talw ya Hospital ya kairuki na uhaya.Nachukia sana mambo ya ukabila, sitarudisha wanafunzi pale.
 
Back
Top Bottom