Kipangaspecial
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 20,778
- 28,722
Ajira za pale zinabagua makabilaMkuu ile sio taasis ya Umma. Ni kampuni binafsi kwahiyo anajiri yeyote anaetaka!
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ajira za pale zinabagua makabilaMkuu ile sio taasis ya Umma. Ni kampuni binafsi kwahiyo anajiri yeyote anaetaka!
Mkuu nitashukuru kama kuna uwezekano ujumbe huu ukawafikia nilio wanukuu serikalini.ujumbe wako utawafikia
duh samahani Ila nimejikuta nahisikia Tu kukwambia TAFUTA ZAKO HALAFU UFANYE HIVYO UNAVYO SHAURI[Tusiime ajiongeze taasisi yake Ni household name pesa zote anazopata anapeleka wapi huwa anakula zote? Aajiri investment manager au financial controller ammsaidiae jinsi ya kuwekeza au atafute investment consultant s mbona wahaya wenzie wako kibao tu wamsaidie.
Walimu ndio capital yake kubwa asicheze nao.Mtaji wake sio pesa ,mijengo au migari ya shule Ni walimu
Napinga kwa nguvu zote kitendo Cha yeye kugusa walimu.Mtaji mkuu wa shule Ni walimu.Hata tuition nyingi mfano mwenge dar watoto wengi huenda kwenye vibanda umiza vya hovyo lakini vyenye vijana walimu wa kutisha wenye uwezo wake kufa mtu kwenye kufundisha masomo ya sayansi
Tusiime be careful with teachers hao Ni producers wa hela za tusiime sio consumers
Haiwezekani taasisi kubwa Kama Tusiime iyumbe na ipate economic shock muda mufupi hivi .
Ada akilipwa akishatoa matumizi huwa anazipeleka wapi? Zote anazifanya dividend yake au?
Wewe ndo umeongea mambo ya msingi. Kuna watu hawajawahi kusimamia hata vibarua wanaleta hoja za kufikirika ambazo haziwezekani.Hapa ni kukaa chini muajiri/muajiriwa na kuja na win win situation. Mwalimu anadai alipwe mshahara wakati hajaingia darasani kufundisha na mwajiri anadai hana pesa ya kumlipa kwa sababu chanzo chake cha mapato kimesimama. Wote wapo sahihi. Mwalimu anafikiri mwajiri ana pesa nyingi za ziada lazima amlipe hizo na au akakope bank ili amlipe. Ila ni mara chache kumpata mfanyabiashara mwenye excess capital kwa ajili ya kusubiri majanga kama corona (ingawa kwa jicho la mwalimu linaona huyu jamaa ni tajiri sana ila hajui source of capital yake ni ipi na anaifinace kivipi)). Na wala hakuna benki itakayomkopesha bila kuwa na business plan inayo onyesha atalipaje hilo deni. Kwanza haijulikani huku kufungwa kwa shule kutaisha lini. Hata angeweza kulipa nusu mshahara (ambao kwa atitude ya hao walimu sidhani wanawesa kuukubali) atalipa hadi lini kama siyo kudrain accounts. Kwa mwajiri priority ni kulinda capital ili baada ya corona biashara iendelee. Kwa mwalimu hajali kama bishara itafungwa baada ya corona ili mradi amelipwa mshahara hata kama mtaji utatumika kumlipa maana ataenda kutafuta ajira kwingine. Kila upande unazo sababu za kulinda upande wake na zote zina mashiko.
Ila sasa mwisho wa siku ni lazima muafaka ufikiwe baina ya pande zote mbili. Lazima wote wajue hili ni janga na halijulikani mwisho wake na pande zote hazijahusika na ujio wa janga. Wajue kila upande una changamoto zake na wachore mstali unao wafanya wote waishi katika kipindi hiki. Mwisho wa siku mwenye shule hawezi kulipa zaidi ya uwezo wake. Ni serikali tu yenye uwezo wa kuwalipa wafanyakazi hata katika mazingira haya. Suala la stimulus package kwetu ni ndoto. Marekani Raisi kaidhinishiwa US2.5 trilion kwa tatizo kama hili na vile vile wana unemplyoment benefit . Nasikia hili neno linaimbwa na NSSF na wenzake. Hapa ndo pangekuwa na jibu badala ya kumbana mwajiri na mabo yangekuwa shwari. Basi kaeni mzungumze mkubaliane na mwajiri. Options ni mbili zenye maamuzi magumu kwa pande zote.
1. Termination of the contract by either party - Worse case scenario; itamfilisi mwajiri na kuwafanya waajiriwa kupoteza ajira
2. Kuwa na retention arrangement, walimu wakubali likizo bila malipo ila mwajiri atoe chochote kwa jina watalokubaliana nalo hata kama ni kidogo kuwezesha kuishi wakati utaratibu wa kufungua shule ukisubiriwa. Walimu wakubali kuwa this is not life as usual na wafunge mikanda kama ilivyo kwa secta zingine kama utalii, usafiri, baa,mahoteli nk. Kote kumepigwa.
Mtu anayefanya biashara kubwa vile huwezi nambia hana akili nikakubali.Akili hana
Kama makampuni yanaoyoingiza mabilion Kwa siku kama voda na Tigo..hayaajiri madereva na cleaners..
Yeye ilikuwaje akaajiri Hadi cleaners?
Why asitumie basi za kukodi?
Anatakiwa kuajiri walimu wasiozidi 50 na wapishi Tu ..
The rest ni matatizo ya kujitakia
Tatizo taasisi binafsi wanachukua mapato yao kuwekeza kwenye biashara nyingine ambazo nyingi hazirudishi fedha na faida.
Wanachukua mikopo mabenki kwa kutumia dhamana na kipato cha biashara mama na kununulia amana/mali (asset) zingine ambazo hazizalishi kitu au zinatia hasara tu. Nyingi ya asset hizo huwezi kufanya Liquidity ya haraka na kurudisha pesa sawa au zaidi ya uliyo wekeza, Kisha kwa haraka ukaenda kurudisha kuokoa kampuni mama inapokuwa katika msukosuko wa kiuchumi kama huu wa sasa wa COVID-19 au recession.
Kwa mfano wamiliki wengi wanaingia tamaa ya kuwekeza miundombinu mipya ya kudumu kama majengo mapya, shule na vyuo vipya ambavyo bado havirudishi pesa haraka kama shule mama.
Kama pale St. An*e Mar*e naona majengo mapya kila kukicha unafikiri ada pekee zitaweza kujenga vile na bado wakalipa wafanyakazi kwa wakati na kutunza akiba itakayo saidia wakati wa dharula kama sasa?
Huenda kuna mikopo mikubwa wanachukua. Hawa wanataka pesa yao ya robo muhula siku mwanao anaripoti shule kwa robo muhula husika vinginevyo hapokelewi hadi ombi maalum, hivyo tusingetegemea kuyumba kirahisi hivyo angalau wangemudu kulipa mishahara ya mwezi March, na nusu mshahara wa mwezi April, kisha likizo bila malipo au robo mshahara mwezi May.
Mambo ndiyo hivyo karibu biashara zote binafsi ilitakiwa serikali isimamie vizuri mifumo ya kifedha, mahesabu ya mapato, na mikopo ya taasisi binafsi kama wanavyo dhibiti taasisi za kifedha (banks, saccos, Bureau De Change) binafsi na za umma. najua wanajaribu kudhibiti hivyo lakini pia kuna udanganyifu kwenye mambo ya kifedha unafanywa na baadhi ya hizi taasisi wanapochukua mikopo na kufanya hesabu zao.
Inatakiwa tuige mifumo kama ya kwenye soka ya FIFA Financial Fair Play taasisi binafsi ziwekewe kanuni za kisheria namna ya kudhibiti (regulate) mapato, matumizi, na mikopo zisikwame kirahisi na kudhulumu au kutesa waajiriwa wao.
Ningeshauri kwa sasa serikali iwasaidie mikopo isiyo na riba hizi shule kama kuzifanyia BAIL OUT walipe nusu mishahara kipindi hiki au wawalipe kama theluthi mbili (two thirds) ya kima cha chini cha mishahara ya waalimu wa serikali wa ngazi husika. Hizi taasisi (shule) waanze kulipa marejesho huo mkopo miezi miwili baada ya kufunguliwa shule lakini malipo yote ya ada za shule hizo yapitie account maalum za serikali siyo za shule ili kulinda fedha za walipa kodi wasije kusumbua kulipa.
Serikali na wenye shule wapige hesabu gharama za uendeshaji shule kisha wajue kiasi gani serikali itawapa pesa zao hizo shule toka kwenye hayo malipo ya ada baada ya kukata marejesho.
Hawa waalimu ni wachache sana serikali inaweza, taasisi binafsi sekta ya elimu ni kama ya afya wanaisaidia serikali kutoa huduma muhimu ya kijamii. mbona kwenye afya serikali inazisaidia taasisi binafsi kama Bugando, KCMC na nyinginezo?
CC: Prof Ndalichako , Dr. Mpango, Mh. Jafo, BOT, Waziri Mkuu, Mh. Raisi.
wenye mikopo benki mtajibebaPole sana mwalimu mwenzangu, hapo uwe na familia wanataka kula na mnategemea mshahara mbona utatamani ummeze huyo mdingi sijui mmaza na kishule chake.
Kwa kile ambacho hakikutarajiwa na wengi Ni suala la wamiliki wa Shule za Binafsi ikiwemo Tusiime ambayo inamiliki Tusiime nursery, primary na secondary kukaidi kulipa mishahara ya watumishi wake wakiwemo walimu.
Mmiliki wa Tusiime aliitisha kikao na wafanyakazi mnamo tarehe 17/4 kwa nia ya kuwaeleza wafanyakazi wake wote Nia yake ya kupunguza wafanyakazi, kuvunja mikataba pamoja na kutolipa mishahara kwa mwezi April na kuendelea.
Watumishi walipinga vikali ajenda hiyo na akaamua kupendekza ajenda ya wafanyakazi 500 kuwa na wawakilishi 50 ambao watakaa kikao kingine ili kujadili na kuamua hatma ya stahiki za watumishi
Vikao vyote alihakikisha anakua na mwanasheria ambae atatetea maslahi yake na hakuwapa wafanyakazi nafasi ya kuwa na mwanasheria au kiongozi wa chama Cha wafanyakazi.
Katika kikao Cha pili aliwashawishi wafanyakazi wasiokua walimu kukubali na ajenda yake ya kutolipa mishahara na kuwataka kuchukua likizo Bila malipo, kwa kutumia ushawishi huo watumishi (auxiliary) ambao wengi ni wahaya wakaunga mkono na hivyo hatma ya wafanyakazi kuamuliwa kwa Kura.
Walimu wa sekondari hawakuridhia uamuzi huo na kuamua kukutana ili kupata mastakabali wao. Baada ya Taarifa hizo kumfikia Ndugu Albert (Mmiliki) aliomba polisi wa kutuliza ghasia kutoka kituo Cha Staki Shari ili kuwadhibiti walimu hao wasikusanyike ili kunadiliana kuhusu mustakabali wao katika eneo lilokubaliwa na kwa bahati nzuri walimu hawakukutana!
Baada ya hapo ameandaa fomu maalum ya likizo Bila malipo na kuwaita wafanyakazi kimya kimya ili wasaini huku akiwapa malipo ya tsh laki Moja na nusu(rushwa) ambao watakubali!
Ikumbukwe kwamba baada ya agizo la kufungwa Shule kwa siku 30 wafanyakazi walitakiwa kujaza fomu za likizo, je inawezekana kisheria ndani ya mwezi mmoja kuwe na likizo, halafu likizo Bila malipo?
Walimu Hawa wanalipa PAYE Kila mwezi, walimu Hawa wanatoa mchango kwa serikali katika utoaji elimu Kama sekta Binafsi.
Serikali na vyombo vyake vimwagize Mr Albert Katagira alipe mishahara ya mwezi April na May haraka! Na pia vikao vyote alivyofanya viamuliwe Ni batili kisheria!
Baada ya hapo aone Ni namna gani atahakikisha wafanyakazi wake wanaishi katika kipindi hiki Cha Covid
Serikali imfanyie ukaguzi katika mapato na matumizi yake kwani hi ni Tusiime holdings kwa maana hiyo Ni group of companies. Kabla uchafu wake mwingine haujaanikwa hadharani. T
Worry not,count it doneMkuu nitashukuru kama kuna uwezekano ujumbe huu ukawafikia nilio wanukuu serikalini.
Kama kuna ufafanuzi kidogo wa sehemu fulani katika mchango wangu naweza kutoa ushirikiano kwenye Private messages (PM) na siyo lazima nijitambulishe jina na mengineyo.
NB: Mimi siyo mwalimu au mmiliki wa shule, I'm just an average Joe in street, sina maslahi yoyote katika hili labda kwa vile mimi ni mzazi tu wa wanafunzi wa kati ya hizi shule.
Kwann waajiriwa hawakutunza akiba ili inapotokea janga kama hili waweze kujikimu walau miezi 3 bila kuwa na stress au kugombana na mwajiri.Wala hakuhitaji hata kuhamisha yeye alitakiwa asiguse walimu angehangaika na non core function staff ambao sio walimu aongee nao the way forward politely .Lakini walimu no no no.
Walimu hawakutakiwa waguswe kabisa alitakiwa at any time awe na akiba hata ya miezi sita ya kuendelea kulipa walimu hata Kama shule itafungwa kwa corona au kwa kukosa wanafunzi ili alinde walimu wazuri wasije ondoka .Hana retention policy endelevu kwa teachers itamgharimu Sana
Ameshajenga jina anataka kubomoa .Kurudisha jina sio kazi rahisi .Ku build brand sio easy task kubomoa one day inatosha.Aachane kusumbua walimu brand builders waliomjengea tusiime Brand
Serikali huwa na akiba ya dharura ,mkulima pia ana akiba ya kiangazi ya chakula taasisi kubwa Kama Tusiime haina akiba ya kiangazi ? Very bad and hopeless financial management .Aajiri wataalamu aache ubahiri
Wazazi hawajalipa ada unataka mmiliki atoe wapi pesa za kuwalipa mishahara? Halafu huwezi kulipa watu ambao hawazalishi kwa sasa. Hii ni biashara siyo non profit organization.[Tusiime ajiongeze taasisi yake Ni household name pesa zote anazopata anapeleka wapi huwa anakula zote? Aajiri investment manager au financial controller ammsaidiae jinsi ya kuwekeza au atafute investment consultant s mbona wahaya wenzie wako kibao tu wamsaidie.
Walimu ndio capital yake kubwa asicheze nao.Mtaji wake sio pesa ,mijengo au migari ya shule Ni walimu
Napinga kwa nguvu zote kitendo Cha yeye kugusa walimu.Mtaji mkuu wa shule Ni walimu.Hata tuition nyingi mfano mwenge dar watoto wengi huenda kwenye vibanda umiza vya hovyo lakini vyenye vijana walimu wa kutisha wenye uwezo wake kufa mtu kwenye kufundisha masomo ya sayansi
Tusiime be careful with teachers hao Ni producers wa hela za tusiime sio consumers
Haiwezekani taasisi kubwa Kama Tusiime iyumbe na ipate economic shock muda mufupi hivi .
Ada akilipwa akishatoa matumizi huwa anazipeleka wapi? Zote anazifanya dividend yake au?
Wazazi hawajalipa ada unataka mmiliki atoe wapi pesa za kuwalipa mishahara? Halafu huwezi kulipa watu ambao hawazalishi kwa sasa. Hii ni biashara siyo non profit organization.
Sent using Jamii Forums mobile app