Tatizo taasisi binafsi wanachukua mapato yao kuwekeza kwenye biashara nyingine ambazo nyingi hazirudishi fedha na faida.
Wanachukua mikopo mabenki kwa kutumia dhamana na kipato cha biashara mama na kununulia amana/mali (asset) zingine ambazo hazizalishi kitu au zinatia hasara tu. Nyingi ya asset hizo huwezi kufanya Liquidity ya haraka na kurudisha pea sawa au zaidi ya uliyowekeza kwa haraka ukaenda kurudisha kuokoa kampuni mama inapokuwa katika msukosuko wa kiuchumi kama huu wa sasa wa COVID-19 au recession.
Kwa mfano wamiliki wengi wanaingia tamaa ya kuwekeza miundombinu mipya ya kudumu kama majengo mapya, shule na vyuo vipya ambavyo bado virudishi pesa haraka kama shule mama.
Kama pale St. An*e Mar*e naona majengo mapya kila kukicha unafikiri ada pekee zitaweza kujenga vile na bado wakalipa wafanyakazi kwa wakati na kutunza akiba itakayo saidia wakati wa dharula kama sasa?
Huenda kuna mikopo mikubwa wanachukua. Hawa wanataka pesa yao ya robo muhula siku mwanao anaripoti shule kwa robo muhula husika vinginevyo hapokelewi hadi ombi maalum, hivyo tusingetegemea kuyumba kirahisi hivyo angalau mishahara ya mwezi March, na nusu mshahara wa mwezi April, kisha likizo bila malipo au robo mshahara mwezi May.
Mambo ndiyo hivyo karibu biashara zote binafsi ilitakiwa serikali isimamie vizuri mifumo ya kifedha, mahesabu ya mapato, na mikopo ya taasisi binafsi kama wanavyo dhibiti taasisi za kifedha binafsi na za umma. najua wanajaribu kudhibiti hivyo lakini pia kuna udanganyifu kwenye mambo ya kifedha unafanywa na baadhi ya hizi taasisi wanapochukua mikopo na kufanya hesabu zao.
Inatakiwa tuige mifumo kama ya kwenye soka ya FIFA Financial Fair Play taasisi zisikwame kirahisi na kudhulumu au kutesa waajiriwa wao.
Ningeshauri kwa sasa serikali iwasaidie mikopo isiyo na riba hizi shule kama kuzifanyia BAIL OUT walipe nusu mishahara kipindi hiki au wawalipe kama theluthi mbili (two thirds) ya kima cha chini cha mishahara ya waalimu wa serikali wa ngazi husika. Waanze kulipa huo mkopo miezi miwili baada ya kufunguliwa shule lakini malipo yote ya shule hizo yapitie account maalum za serikali siyo za shule ili kulinda fedha za walipa kodi wasije kusumbua kulipa.
Serikali na wenye shule wapige hesabu gharama za uendeshaji shule kisha wajue kiasi gani serikali itawapa pesa zao hizo shule toka kwenye hayo malipo ya ada.
Hawa waalimu ni wachche sana serikali inaweza, taasisi binafsi sekta ya elimu ni kama ya afya wanaisaidia serikali kutoa huduma muhimu ya kijamii. mbona kwenye afya serikali inazisaidia taasisi binafsi kama Bugando, KCMC na nyinginezo?
CC: Prof Ndalichako , Dr. Mpango, Mh. Jafo, BOT, Waziri Mkuu, Mh. Raisi.