guwe_la_manga
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 2,820
- 2,758
poleni sana walimu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wala hakuhitaji hata kuhamisha yeye alitakiwa asiguse walimu angehangaika na non core function staff ambao sio walimu aongee nao the way forward politely .Lakini walimu no no no.Ni rafiki take mkubwa na wanashauriana.
Wakati Alpha schools amekaa na watumishi wake na kukubaliana awalipe 50% na inayobakia iwe Deni yeye kwa aliposikia janga la Covid akaamua kuhamisha mpunga wa kutosha kwenda kwingine! Na kwakua anajua walimu wake Ni weupe kwenye financial statements akawaambia Ana mil 30 tu bank nao wakakubali kwa kusoma ile figure ya chini wajanja wakstuka, Asante Serikali kwa kumtokea Jana na hakikisheni account zake zote je Ni kweli hawezi kujiendesha hata mwezi mmoja? Mana huu Ni mwanya wa kuhujumu uchumi kwa kutopeleka PAYE.
Absolutely right....Ukivaa uhusika wa mmiliki utakuwa upande wa mmiliki,, Ukivaa uhusika wa walimu utakuwa upande wa mwalimu.
Ila ukweli ni hela hakuna,, so hata wakitaka kulipwa bado itakuwa ni deni.
BUT, Ni muda wa walimu kuchunga ndimi zao sana, Coz wakizembea wanaweza chezea Kazi na Mshahara
Huyu Mmiliki ni mshenzi sana.....kama alifanya miscalculation hiyo ni juu yake.[Tusiime ajiongeze taasisi yake Ni household name pesa zote anazopata anapeleka wapi huwa anakula zote? Aajiri investment manager au financial controller ammsaidiae jinsi ya kuwekeza au atafute investment consultant s mbona wahaya wenzie wako kibao tu wamsaidie.
Walimu ndio capital yake kubwa asicheze nao.Mtaji wake sio pesa ,mijengo au migari ya shule Ni walimu
Napinga kwa nguvu zote kitendo Cha yeye kugusa walimu.Mtaji mkuu wa shule Ni walimu.Hata tuition nyingi mfano mwenge dar watoto wengi huenda kwenye vibanda umiza vya hovyo lakini vyenye vijana walimu wa kutisha wenye uwezo wake kufa mtu kwenye kufundisha masomo ya sayansi
Tusiime be careful with teachers hao Ni producers wa hela za tusiime sio consumers
Haiwezekani taasisi kubwa Kama Tusiime iyumbe na ipate economic shock muda mufupi hivi .
Ada akilipwa akishatoa matumizi huwa anazipeleka wapi? Zote anazifanya dividend yake au?
Yes ana shule kubwa na wanafunzi wengi sana. Ni hivi kwa primary std 1-7 wanafunzi ni 60+, kwa stream 4 ni wangapi? Then zidisha mara 7. Bado nursery, O level na A level. Upo?Wafanyakazi 500? seriously?
.Kwa mtaji wa ada?
Naunga mkono hojaHuyu Mmiliki ni mshenzi sana.....kama alifanya miscalculation hiyo ni juu yake.
Hatari ninayoiona mimi ni kuwa walimu wakiamua kufanya revenge victims watakuwa watoto wetu hivyo wazazi wawe macho sana otherwise itakula kwao.
No way aajiri mtaalamu wa financial management hata wa short time.Kuwa na mtaji sio kuwa unajua biashara hl.Bakhresa darasa la pili lakini anamiliki kuanzia meli,vyombo vya habari,nk wakati aliishia a,e,I,o,u sababu anatumia na kaajiri wataalamu kibaoAchen kulaumu hawa mamiliki.
Ni vema serikali ifanye kitu kwaajili ya kulinda Ajira za sekta binafsi hususani hawa walimu.
Kwan wazazi wote mmelipa Ada ya mwaka mzima wa masomo??..wapo wanaolipa kwa mafungu....
Sasa kama nayeye uchumi umeyumba afanyaje ??
Serikali itoe fungu, angalau nusu kisha wamiliki waongezee, ili Watu walindiwe ajira zao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali yako iliyoandaa bakuri la kuchangia coronavirus ndo unasema ina akiba ya dharula? Kama serikali tu haina hela ya kutosha bado inalazimisha watu walipe kodi unatakaje sekta binafsi iwe na hela.Wala hakuhitaji hata kuhamisha yeye alitakiwa asiguse walimu angehangaika na non core function staff ambao sio walimu aongee nao the way forward politely .Lakini walimu no no no.
Walimu hawakutakiwa waguswe kabisa alitakiwa at any time awe na akiba hata ya miezi sita ya kuendelea kulipa walimu hata Kama shule itafungwa kwa corona au kwa kukosa wanafunzi ili alinde walimu wazuri wasije ondoka .Hana retention policy endelevu kwa teachers itamgharimu Sana
Ameshajenga jina anataka kubomoa .Kurudisha jina sio kazi rahisi .Ku build brand sio easy task kubomoa one day inatosha.Aachane kusumbua walimu brand builders waliomjengea tusiime Brand
Serikali huwa na akiba ya dharura ,mkulima pia ana akiba ya kiangazi ya chakula taasisi kubwa Kama Tusiime haina akiba ya kiangazi ? Very bad and hopeless financial management .Aajiri wataalamu aache ubahiri
Dharura naongelea mishahara ya wafanyakazi wake siongelei mtu kashikwa kipindu pindu serikali iwe na hela ya kumtibia kuharisha kwake mfululizo non stop!!Serikali yako iliyoandaa bakuri la kuchangia coronavirus ndo unasema ina akiba ya dharula? Kama serikali tu haina hela ya kutosha bado inalazimisha watu walipe kodi unatakaje sekta binafsi iwe na hela.
Poor financial management ina maana Tusiime wanaishi hand to.mouth? Mzazi hamiliki shule Hana Cha ku share iwe profit or loss kwa Nini utake mzazi agawane na mumiliki loss? Profit wakati huwa hapewi?Hapa ni Suala la:
1. Wamiliki
2. Wazazi
Wazazi ndo wateja wakubwa, wapo wazazi wanaolipa ada kwa mwaka na wengine kwa awamu(kidogo dogo). Wazazi wengi ukiwasikiliza wanasema hawawezi kulipa ada bila masomo. Wamiliki nao wanasema hawawezi kulipa mshahara bila kazi.
Nikirudi katika andiko; niwaombe wamiliki na wazazi watambue kuwa hili ni janga. Wakubaliane biashara nusu gharama. Wamiliki wazungumze na walimu na wafanyakazi wengine wa shule kuwalipa nusu mshahara. Ubinadamu ndo kipindi chake sasa cha kuonekana.
Shule kama Tusiime nina imani haishindwi kulipa nusu mshahara hata kwa miezi 3. Mmiliki rudi mezani ukayajenge na wafanyakazi wako. Hao ndo waliokufikisha hapo.
Sheria zetu za ajira zina changamoto na serikali imekaa kimya kama vile hakitokei kituAisee , hapa serikali ndo inapswha kuweka mambo sawa kama hotuba ya Kambi kuu ya Upinzani Jana ilivyoelezea .
Ni rafiki take mkubwa na wanashauriana.
Wakati Alpha schools amekaa na watumishi wake na kukubaliana awalipe 50% na inayobakia iwe Deni yeye kwa aliposikia janga la Covid akaamua kuhamisha mpunga wa kutosha kwenda kwingine! Na kwakua anajua walimu wake Ni weupe kwenye financial statements akawaambia Ana mil 30 tu bank nao wakakubali kwa kusoma ile figure ya chini wajanja wakstuka, Asante Serikali kwa kumtokea Jana na hakikisheni account zake zote je Ni kweli hawezi kujiendesha hata mwezi mmoja? Mana huu Ni mwanya wa kuhujumu uchumi kwa kutopeleka PAYE.
Nimesikia nitwalipa.Kwa kile ambacho hakikutarajiwa na wengi Ni suala la wamiliki wa Shule za Binafsi ikiwemo Tusiime ambayo inamiliki Tusiime nursery, primary na secondary kukaidi kulipa mishahara ya watumishi wake wakiwemo walimu.
Mmiliki wa Tusiime aliitisha kikao na wafanyakazi mnamo tarehe 17/4 kwa nia ya kuwaeleza wafanyakazi wake wote Nia yake ya kupunguza wafanyakazi, kuvunja mikataba pamoja na kutolipa mishahara kwa mwezi April na kuendelea.
Watumishi walipinga vikali ajenda hiyo na akaamua kupendekza ajenda ya wafanyakazi 500 kuwa na wawakilishi 50 ambao watakaa kikao kingine ili kujadili na kuamua hatma ya stahiki za watumishi
Vikao vyote alihakikisha anakua na mwanasheria ambae atatetea maslahi yake na hakuwapa wafanyakazi nafasi ya kuwa na mwanasheria au kiongozi wa chama Cha wafanyakazi.
Katika kikao Cha pili aliwashawishi wafanyakazi wasiokua walimu kukubali na ajenda yake ya kutolipa mishahara na kuwataka kuchukua likizo Bila malipo, kwa kutumia ushawishi huo watumishi (auxiliary) ambao wengi ni wahaya wakaunga mkono na hivyo hatma ya wafanyakazi kuamuliwa kwa Kura.
Walimu wa sekondari hawakuridhia uamuzi huo na kuamua kukutana ili kupata mastakabali wao. Baada ya Taarifa hizo kumfikia Ndugu Albert (Mmiliki) aliomba polisi wa kutuliza ghasia kutoka kituo Cha Staki Shari ili kuwadhibiti walimu hao wasikusanyike ili kunadiliana kuhusu mustakabali wao katika eneo lilokubaliwa na kwa bahati nzuri walimu hawakukutana!
Baada ya hapo ameandaa fomu maalum ya likizo Bila malipo na kuwaita wafanyakazi kimya kimya ili wasaini huku akiwapa malipo ya tsh laki Moja na nusu(rushwa) ambao watakubali!
Ikumbukwe kwamba baada ya agizo la kufungwa Shule kwa siku 30 wafanyakazi walitakiwa kujaza fomu za likizo, je inawezekana kisheria ndani ya mwezi mmoja kuwe na likizo, halafu likizo Bila malipo?
Walimu Hawa wanalipa PAYE Kila mwezi, walimu Hawa wanatoa mchango kwa serikali katika utoaji elimu Kama sekta Binafsi.
Serikali na vyombo vyake vimwagize Mr Albert Katagira alipe mishahara ya mwezi April na May haraka! Na pia vikao vyote alivyofanya viamuliwe Ni batili kisheria!
Baada ya hapo aone Ni namna gani atahakikisha wafanyakazi wake wanaishi katika kipindi hiki Cha Covid
Serikali imfanyie ukaguzi katika mapato na matumizi yake kwani hi ni Tusiime holdings kwa maana hiyo Ni group of companies. Kabla uchafu wake mwingine haujaanikwa hadharani. T