Mmoja Afariki, Wanne Walazwa Wakishindana Kunywa Pombe Moshi

Mmoja Afariki, Wanne Walazwa Wakishindana Kunywa Pombe Moshi

Bora umpe mtihani kwamba hawezi kufanya kitu fulani afanye umpe hiyo hela au ashindwe kuliko kuchezea vitu vya hatari kama hivyo.

Hii nchi kila kitu fake unaweza kukuta hiyo burudani ni vya wale Wachagha wa Manzese ukauwa mtoto wa mtu ukabaki na lawama.
SIO VITU FEKI MZEE NI VITU OG KABISA HAO JAMAA KILICHOWAUA SIO UFAKE WAKINYWAJI ILA NI ALCOHOL OVERDOSE
 
Hao jamaa kilichowaua sio Kwamba wamekunywa pombe feki ila kitaalamu kilichomuua uyo jamaa ni ALCOHOL OVERDOSE ndio MAANA wanasemaga KUNYWA POMBE KUPITA KIASI NI HATARI KWA AFYA YAKO ATA BIA UKINYWA NYINGI ZINAKUUA PIA KWAIYO.MSITAKE KUHARIBU BRAND YA WATU HAO JAMAA WAMEJI OVERDOSE
 
Mtu mmoja amefariki dunia, huku wengine wanne wakinusurika kifo wakati wakishindana kunywa pombe kali aina ya 'Smart Gin', baada ya kuahidiwa kupewa mkate, sukari na Sh50,000 kwa atakayeshinda.

Tukio hilo limetokea Juni 8, 2023 katika kata ya Sanya Juu, wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya watu hao kuahidiwa na mtu anayedaiwa kuwa mfanyabiashara wilayani humo, ambaye sasa ametoroka.

Inadaiwa kuwa mtu huyo aliwaahidi kuwapa zawadi hizo na mpaka mmoja anafariki walikuwa wameshakunywa chupa tano kati ya tisa zilizokuwa zikishindaniwa.

Hata hivyo, baada ya kumaliza kunywa chupa tano hali zao zilianza kuwa mbaya na wengine kupoteza fahamu ambapo baadaye waliokolewa kwa kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kupata msaada wa dharura.

Mkuu wa wilaya ya Siha, Christopher Timbuka alimtaja aliyepoteza maisha kuwa ni Benson Mshiri, mkazi wa Kijiji cha Merad na kwamba waliolazwa hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na muda wowote wataruhusiwa kwenda majumbani.

Mwananchi
Mashindano ya kijinga na kipuuzi sana. Classmate wangu moja pia majuzi mwezi April kijijini ametoka shamba kapitia kilabuni kakuta mabishano juu ya nani anaweza kumaliza k-Vant kubwa anunuliwe? Akajitokeza, na njaa yake na ulafi wake akaifakamia within 2minutes kaimaliza na aft10minutes akatapika damu mambonge mabonge ( kwa observation yangu isiyo ya kidaktari ni Maini yamekatikakatika) na akawa no more in20 minutes. Na hadidhi yake ikaishia apo.
So, Friends, ladies and gentlemen pombe si chai, na haina mashindano. Hebu kunywa kiasi kistaarabu utainjoy sana. Haiuzwi kwa aliye chini ya Miaka18. Pole kwa wafiwa, pole sana kwa ambao pia wamepata madhara baada ya kufakamia Gin.
 
Umasikin ni mbaya sana mungu atusaidie, unadhalilika na kukumbwa na magonjwa nyemelezi Kwa kukosa lishe bora mwisho unakuwa mwehu kama walimu
ss ww walimu wanashida gani mana wanakula mshahara kila mwez hata kama hautoshi mana hata ww kipato chako hakitosh ndo mana kila siku unaenda kazin hulali ndani acha kuwakejel walimu
 
Back
Top Bottom