Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza au kuuliza, naomba mwenye taarifa atujuze ni wakala gani pekee alifaulu mtihani wa FIFA wa uwakala wa wachezaji?
Je, watanzania ni vilaza kiasi hiki? Nimetoa taarifa hizi toka kwa Angitile Osiah kama alivyo eleza katika moja ya makala yake kwenye gazeti la mwananchi.
Kwa bahati mbaya mwandishi hajamtaja huyo aliyefaulu na hajasema kulikuwa na watahiniwa wangapi katika mtihani huo.
Kutokana na tatizo hili Tanzania itaendelea kuona wachezaji wa kitanzania wakiishia kucheza ndani ya Tanzania tu. wachache sana watapata nafasi ya kuchezea ligi kubwa nje ya Tanzania hasa barani Ulaya.
Ushauri wangu nawaomba watafiti waanze kuangalia kama lishe ya watanzania wengi inachangia udumavu wa akili. Au tatizo la kutojua kiingereza lina mchango mkubwa kwa watanzania wengi kutofanya vema kwenye mitihani ya kimataifa?