Elimu elimu elimu hilo la kwanza, kisha inakuja kuishinda nafsi.
Gaidi wa kiislam lazima ahusike kwenye hayo mawili,
1. Aidha awe hana elimu nzuri anakuwa brainwashed, anapewa aya za kupigana na hadithi pasina maelezo ya kina, nae kwa kuwa dini anaichukulia kwa mihemko, anaumuka kama katiwa hamira.
2. Kuishinda nafsi, yaani anakuwa na elimu anajua hiki ni kibaya ama ni haramu, lakini kwakuwa anahitaji kitu fulani hajali, anachotenda.
Hii sio kwa magaidi tu hata sisi waislamu wa kawaida, zinaa mbaya myu anajua lakini anafanya, anapiga ulabu akijua haifai, mtu mshirikina, sheikh anapiga ramli hali ya kuwa anajua ni haram, mtu haendi msikitini hali anajua umuhimu wa ibada ya swala, mtu anadhulumu yatima akijua ni moja ya madhambi makubwa, mtu ni mnafiki akijua uzito wa unafiki, mtu msengenyaji na anajua ubaya wake. n.k
Niliwahi kumsikiliza saana sheikh rogo nikakiri mwenyewe kama nisingekuwa na elimu kidogo, akili y utambuzi kuchambua hiki sawa hiki si sawa basi nilikiri huyu aboud rogo anaweza mbadili mtu akili vizuri tu na akafanya jambo la hovyo kabisa.