Mmoja wa Mawakili wa Erick Kabendera aeleza kinachoendelea

Unavyotaka washangilie na kumsifia mkandamizaji wa haki zao? Wawe wanagugumia kimyakimya ili 'mzungu asisikie na 'kututukana'? Wasitoe siri ya kuonewa kwao katika nchi yao ili wasimchafue 'Rais' wao? KAMA kweli hayo yatoka moyoni mwako, basi tuna tatizo kubwa katika nchi hii. Kwani hiyo ndio style ilokuwa ikitumiwa na makaburu SA. Amen.
Aaaah! Mbona hujitambui kiasi hicho? Lini ulimtegemea Mzungu na akakusaidia? Unao mfano wowote wa hivi karibuni wewe, au yeyote aliyeshitaki kwao na kupata support? Europe has enough in bed not even to care what is coming from outside her borders. Be calm and avoid hysterical comments that are based on personal grievances. We are not in problems rather, you are in problems.
 
..hivi Mtanzania akimuandika vibaya Raisi Magufuli kwenye gazeti linalochapishwa nje ya Tanzania anakuwa amefanya uchochezi?

..naomba muongozo wa wanaJF wenye uelewa wa masuala ya sheria.

Cc Petro E. Mselewa , Pascal Mayalla

Wangekuwa hawana madhaifu, wangepuuzia. Kinachofanyika sasa ni kumnyamazisha kila anaye onekana kuwa na mawazo/mtazamo tofauti na wa kwao.

Kiukweli kosa lililofanyika 2015, hata Mungu anaweza asitusamehe.
 
Pole zake.Kama kweli ni yeye, basi hakutenda sawa ktk uandishi wake. Tulisoma makara zake bila kujua nani anaandika. Aliandika kwa kujifichaficha, jambo ambalo lilimpa uhuru wa kusema mawazo yake. Pamoja na haya ya wakili, sielewi kazi ya wanasheria ni nini? Je, ni kuwaokoa wenye makosa? Au kuwahakikishia hukumu wanayostahili. Naona mara nyingi mafaikio yao na majivuno ni kuona muharifu akiachiwa!

Uandikaji wa mwandishi huyu, haukuwa na staha kwa rais, hata kama anaamini rais aliyepo ni bwege. Alistahili kuheshimu nafasi hiyo.
Unaonekana una uelewa finyu kuhusu kazi ya wakili na pia kuhusu kesi zote zilizopo mahakamani.

Mwenye kujua kwamba huyu kweli alivunja sheria ni mahakama tena baada ya kusikiliza pande zote.

Wewe na akili yako yote unahukumu bila hata kutaka kumsikiliza mtuhumiwa,na unataka hata wakili afanye hivyo hivyo?
 
TAARIFA KUHUSU KUKAMATWA, KUWEKWA MAHABUSU NA KUHOJIWA KWA MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ERICK KABENDERA

Tarehe 29 Julai 2019, majira ya saa 11 jioni, watu wasiojulikana na waliovaa kiraia, walifika nyumbani kwa Erick Kabendera eneo la Mbweni Mpigi Dar, wakitaka kumkamata.

Hata hivyo, ushirikiano wa marafiki wa Erick na majirani waliofika katika eneo la tukio, ulilazimisha watu hao kujitambulisha kuwa ni askari Polisi.

Baada ya kujitambulisha, watu hao walifanikiwa kumchukua Erick na kwenda naye kusikojulikana, wakachukua simu yake na kuifunga kiasi kwamba hakuweza tena kuwasiliana tena na wenzake.

Kufikia leo, Erick Kabendera amefikisha siku tano akiwa mikononi mwa Polisi.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, Polisi inatakiwa kukaa na mtu kwa muda usiozidi saa 24 kabla ya kumfikisha mahakamani. Kama itataka kukaa na mtu kwa zaidi ya muda huo, inatakiwa kupata kibali cha Mahakama.

Katika jambo hili la Kabendera; taratibu zote hizi hazijafuatwa -kwamba Polisi imekaa naye kwa zaidi ya saa 24 na haijapata ruhusa ya Mahakama kufanya hivyo.

Katika siku yake ya kwanza kushikiliwa, Kabendera alihojiwa kwa zaidi ya saa nne na maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuhusu Uraia wake.

Ni Idara hiyohiyo ya Uhamiaji iliwahi kusema huko nyuma kwamba suala la uraia wa Kabendera halina utata.

Agosti Mosi, 2019, Kabendera alichukuliwa na askari wa Kituo cha Polisi cha Kati kitengo cha Makosa ya Mtandaoni na kuhojiwa kwa zaidi ya saa tatu kwa tuhuma za uchochezi kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari kifungu cha 52 na 53.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kumshitaki Erick Kabendera kwa makosa ya uchochezi kwa madai kwamba mnamo Julai 31 mwaka huu, alichapisha habari katika jarida la The Economist yenye kichwa cha habari kisemacho “John Magufuli is bulldozing Tanzania’s Freedom”.

Erick amenyimwa dhamana na Jeshi la Polisi ingawa dhamana ni haki yake kikatiba.

Mchana huu, Jeshi la Polisi limetuma maofisa wake kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Kabendera.

Kama Wakili wake, nalifuatilia jambo hili kwa karibu na nitakuwa nikitoa kwa Watanzania na Jamii ya Kimataifa kila itakapohitajika kufanya hivyo.

Imetolewa na

Jebra Kambole
Law Guards Advocates
2nd August 2019.

Kwa maelezo zaidi, tunaweza kuwasiliana kupitia

Phone: +255 717334032
Email: jebrakambole@gmail.com
Sasa huku ndio mahakamani?kapambane mahakamani huku tutajaza server za JF bure.
 
Unaonekana una uelewa finyu kuhusu kazi ya wakili na pia kuhusu kesi zote zilizopo mahakamani.

Mwenye kujua kwamba huyu kweli alivunja sheria ni mahakama tena baada ya kusikiliza pande zote.

Wewe na akili yako yote unahukumu bila hata kutaka kumsikiliza mtuhumiwa,na unataka hata wakili afanye hivyo hivyo?
Umesoma maelezo ya huyo mwanasheria wake anasema nini? Nincompoop!
 
Pole zake.Kama kweli ni yeye, basi hakutenda sawa ktk uandishi wake. Tulisoma makara zake bila kujua nani anaandika. Aliandika kwa kujifichaficha, jambo ambalo lilimpa uhuru wa kusema mawazo yake. Pamoja na haya ya wakili, sielewi kazi ya wanasheria ni nini? Je, ni kuwaokoa wenye makosa? Au kuwahakikishia hukumu wanayostahili. Naona mara nyingi mafaikio yao na majivuno ni kuona muharifu akiachiwa!

Uandikaji wa mwandishi huyu, haukuwa na staha kwa rais, hata kama anaamini rais aliyepo ni bwege. Alistahili kuheshimu nafasi hiyo.
Kaka umesema maneno yangu
Umeandika mawazo yangu
Sijajua nimuweke wapi Kabendera kwa uandishi ule.
Ni Janga
 
Tatizo la wachangiaji JF na hasa wanasiasa ambao hapa wameficha majina yao, wanadhani rais akitukanwa basi wao wataonekana wanafaa kushika nafasi. Mtu kama huyu Kabendera ni limbukei ambaye akishangiliwa na wanaotaka nafasi hiyo, anashindwa kujizuia na kuanza kujirusha kuzidi kipimo. Ukweli ni kwamba, MAgufuli anapodhalilika, wao wanaiona TZ kama nchi isiyofaa.

Huyu lazima atiwe kibano kwa kushindwa kujitambua. Amekuwa mtumwa anayelinda watumwa wengine na kujiona yeye ana nafuu.
 
TAARIFA KUHUSU KUKAMATWA, KUWEKWA MAHABUSU NA KUHOJIWA KWA MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ERICK KABENDERA

Tarehe 29 Julai 2019, majira ya saa 11 jioni, watu wasiojulikana na waliovaa kiraia, walifika nyumbani kwa Erick Kabendera eneo la Mbweni Mpigi Dar, wakitaka kumkamata.

Hata hivyo, ushirikiano wa marafiki wa Erick na majirani waliofika katika eneo la tukio, ulilazimisha watu hao kujitambulisha kuwa ni askari Polisi.

Baada ya kujitambulisha, watu hao walifanikiwa kumchukua Erick na kwenda naye kusikojulikana, wakachukua simu yake na kuifunga kiasi kwamba hakuweza tena kuwasiliana tena na wenzake.

Kufikia leo, Erick Kabendera amefikisha siku tano akiwa mikononi mwa Polisi.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, Polisi inatakiwa kukaa na mtu kwa muda usiozidi saa 24 kabla ya kumfikisha mahakamani. Kama itataka kukaa na mtu kwa zaidi ya muda huo, inatakiwa kupata kibali cha Mahakama.

Katika jambo hili la Kabendera; taratibu zote hizi hazijafuatwa -kwamba Polisi imekaa naye kwa zaidi ya saa 24 na haijapata ruhusa ya Mahakama kufanya hivyo.

Katika siku yake ya kwanza kushikiliwa, Kabendera alihojiwa kwa zaidi ya saa nne na maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuhusu Uraia wake.

Ni Idara hiyohiyo ya Uhamiaji iliwahi kusema huko nyuma kwamba suala la uraia wa Kabendera halina utata.

Agosti Mosi, 2019, Kabendera alichukuliwa na askari wa Kituo cha Polisi cha Kati kitengo cha Makosa ya Mtandaoni na kuhojiwa kwa zaidi ya saa tatu kwa tuhuma za uchochezi kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari kifungu cha 52 na 53.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kumshitaki Erick Kabendera kwa makosa ya uchochezi kwa madai kwamba mnamo Julai 31 mwaka huu, alichapisha habari katika jarida la The Economist yenye kichwa cha habari kisemacho “John Magufuli is bulldozing Tanzania’s Freedom”.

Erick amenyimwa dhamana na Jeshi la Polisi ingawa dhamana ni haki yake kikatiba.

Mchana huu, Jeshi la Polisi limetuma maofisa wake kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Kabendera.

Kama Wakili wake, nalifuatilia jambo hili kwa karibu na nitakuwa nikitoa kwa Watanzania na Jamii ya Kimataifa kila itakapohitajika kufanya hivyo.

Imetolewa na

Jebra Kambole
Law Guards Advocates
2nd August 2019.

Kwa maelezo zaidi, tunaweza kuwasiliana kupitia

Phone: +255 717334032
Email: jebrakambole@gmail.com
Tumeshakuwa Rwanda waandishi mchichungu
 
Back
Top Bottom