Mna Nini Ndani ya Kitabu cha Sheikh Ponda?

Ujamaa...
Siku zote nimesafiri kwa gharama za wanaonialika baadhi ni hao hapo chini:

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).

Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).

Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).

Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.

Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.

Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.

Hao hapo chini walinialika 2011:

University of Iowa, Iowa City, USA.
Northwestern University, Chicago, Illinois, USA.
Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

Nimealikwa Iran na Wizara ya Nchi za Nje kuhudhuria Hawli ya Imam Khomeni 2007.

Nimealikwa Saudi Arabia Hijja na Mfalme wa Saudia 2014.

Nilialikwa Turkey kwenye Bookfair na Kilimanjaro Dialogue Institute 2015.


Bado nasafiri kwa mialiko ukipenda naweza kukuwekea picha zangu za hivi karibuni safari ya mwisho ni mwaka jana 2022.


Istanbul Book Fair 2015​
 
Mjamaa...
Hapana tatizo ikiwa wewe unaona kitabu hakikuwa na taarifa za kutisha.

Kitabu pdf iko mtandaoni miaka mingi sasa na watu wengi wamekisoma.

Taarifa gani za kutisha zaidi ya uongo, uvumi, uchonganishi na fitna dhidi ya jamii za watanzania. Serikali iliona hakina umuhimu kwa maudhui yake, serikali ni pana sana kumanage mamilioni ya watanzania na uhusiano kimataifa sio swala dogo. Leo hii serikali ione kuna tishio gafla mtu mmoja au kikundi kione hakuna tishio. Serikali Ina mkono mpana sana na wengi wenu mmeshughulikiwa vya kutosha wengine walikaa miaka na miaka magereza wengine walifungwa kwa mambo yao ya kijinga na uchonganishi. kule zenji yaliyowakuta wale mamluki wa uamsho waliokuwa na vinywa vipana kwasasa adabu nidhamu na utii umewajaa na wengine wamerudi magomeni makwao. Mtandao wa mamluki ulisha vunjwa vunjwa kuanzia zanzibar, tanga, mwanza, arusha bila kusahau mkuranga, ikwiriri, rufiji na kibiti. Mliobakia ni sample ndogo kama mtego wa kuendelea kukamata masalia salia yatakayoendelea kujitokeza.
 
Umenikumbusha mwaka 2012 pale Uongozi wa UDOM walipoharibu uchaguzi wa Serikali ya wanafunzi college ya Social Science pale UDOM
Walifyeka majina ya wagombea Urais wote ambao sio waislamu (mgombea aliyekua anaungwa mkono na wengi alikua anaitwa Zamba Nasser alikatwa makusudi lengo ikiwa ni Rais awe mwislamu. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo(fedha na mipango) Prof.S. Mlacha ndiye alikua anapigania sana hii issue
 

Naam, bado naendelea kukuchambua na kuna vitu kama ushahidi navipata kwene maandishi yako. Hivyo najifunza kitu hapa, mjadala ni mtamu sana watu zaidi ya 1k hapa wanakusoma kama fanani na michango ya hadhira inasomwa pia. awali hawakufika idadi hio.
 

Unamkumbuka yule madam kama dean of student aliyekuwa na tabia ya kukamata mabinti wa kikristo mtaani. Anakuja chuo na kuwafungulia mashtaka ya utomvu wa maadili mpaka baadhi yao wakafukuzwa. Alikuwa ni sumu sana akitaka mavazi yawe yale makanzu yao ya kike. Hawa watu ni sumu hakika tuishi nao kwa taadhari kubwa sana. Ushahidi ni mwingi kwa kilichokuwa kinaendelea UDOM dhidi ya hawa watu.
 
Bila shaka unamuongelea Madame Aziza ni Albino.
Kiukweli UDOM iliharibiwa sana kipindi kile kwa movement za kidini
 
Umesema kweli nikiwa sekondar nilienda wizara ya elimu chumba cha mipango nilikua na ndugu wa ukoo ameajiriwa pale kwenye mazungumzo yao niliona pana agenda za siri,,,maneno yalijadili kuhusu nyerere fondesheni ilionesha ndani ya taasisi palikuwa na kitengo maalum cha kupiga vita uislam ila niliekti kama sikusikia ...
 
Ujamaamf,
Sina taarifa hizo.
Ningependa sana kuzijua.
 
Kwenye asilimia zako....
Nimeona waislamu na Wakristo pekee.
Vipi Wahindu, waabudu mizimu, na wapagani hao hawakushika nafasi?
Au kila mtu anayeitwa Marco ni mkristo?
Unataka tutambuane kwa Dini ili iwaje? Faida za kutambuana kwa dini ni zipi na hasara za kutambuana kwa dini ni zipi?
 
Ujamaamf,
Sina taarifa hizo.
Ningependa sana kuzijua.

Zipo nyingi sana. Ukiwa kama gwiji wa uvumi mitandaoni sizani kama hujawahi ona mada hizi hapa jukwaani, kama upo tiari basi fungua mjadala mpya watu waanze kushusha nondo.
 
Illma...
Inaelekea hujui tatizo linaloikabili Tanzania na mjadala ulioko JF kati yangu na wengine sasa zaidi ya miaka 10.

Harakati za kuwaondoa wakoloni Tanganyika zilianza na African Association mwaka wa 1929 waasisi wakiwa Cecil Matola (President), Kleist Abdallah Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima, Ibrahim Hamisi, Zibe KIdasi, Suleiman Majisu, Rawkes Kusi na Rawson Watts.

Kuna Mpagani au Muhindu katika orodha hiyo ya waasisi wa AA?
Unajua sababu yake?

Unajua pia kwa nini Waislam ni wengi katika waasisi hao?

Unajua kwa nini Wajerumani waliwanyonga majemadari wengi Waislam katika Vita Vya Maji Maji?

Nenda Sekenke Songea kaangalie makaburi utapata jibu.

Kuna kaburi la halaiki wamezikwa Waislam wanokaribia 77 na pembeni yake kuna kaburi la Nduna Abdulrauf Songea Mbano maarufu kwa jina la Songea Mbano.

Unajua kwa nini Kilwa walionyongwa na Wajerumani ni Hassan Omari Makunganya, Omari Muenda na Jumbe?

Kuna Mpagani aliyenyongwa?

Unaijua historia ya TAA na viongozi wake?
Wako Wapagani au Wahindu?

Unawajua Wapagani na viongozi wao katika historia ya kuigania uhuru wa Tanganyika?

Unazijua picha hizo hapo chini na zinaeleza nini?


Omari Hassan Mkunganya Makunganya na wenzake 1895

Baraza la Wazee wa TANU 1957

Shambani kwa Sheikh Abdallah Iddi Chaurembo Mtoni 1956

Dodoma 1955/56

 
Hujajibu mswali langu ila Umespin mazungumzo Sitaki kuzungumzia hayo ya resistance ni mada pana japo ipo wazi.

Nilichouliza mimi hiyo 2015 hizo teuzi hakukuwa na wapagani? Vipi nao umewajumlisha katika wakristo.

Unafanya hivi kwa manufaa gani?
Unataka kupanda nini kwenye nyoyo za watu?
Wewe ni mtu mzima sasa Pengine ni baba au babu wa wengi humu, vipi utakuwepo hichi unachopanda kitakapomea?
Au utakuwa ushaenda kwa muumba ( siombei ila ndio uhalisia ).
Swali langu kuu kwanini unataka kutambulika kwa dini yako? Na sio kwa vitu vingine.

Nakuambia tena kwa mara Nyingine ( nilishawahi kukuambia humu). Aina hii ya harakati unayofanya sio relative tena......hasa kwa kizazi cha sasa.
Vjana hawajali tena kuhusu TAA wala TANU, si ajabu hawazijui.......
 
mkuu nadhani hujanielewa! Mi nataka pdf yenye huo ushahidi wa ubaguzi wa govt kwa wenzetu waislamu ..Ambao hadi mkapa alistuka.
 
Illma...
Nimekujibu ila si jibu unalolitaka wewe.

Sipandi chochote katika moyo wa yeyote.

Nimesahihisha historia ya uhuru wa Tanganyika iliyokuwa na makosa mengi sana.

Na nimeeleza yaliyotokea baada ya uhuru kupatikana.

Huu mwaka wa 25 kitabu kinasomwa na watu wanaelewa ukweli.

Hapajatokea tatizo lolote.

Tuko hapa huu mwaka wa 10 tunaijadili historia hii.

Kama unaona historia hii haistahili kuwepo baada ya kufutwa mimi sina tatizo na mawazo yako.

Kwangu mimi hii ni historia ya wazee wangu na itabaki kuwa urithi wa kizazi kijacho.

Haya ndiyo manufaa yake na kitabu kimependwa sana.

Huu mwaka wa 25 bado nahojiwa na vyombo mbalimbali kuhusu Kleist Sykes na wanae.

Mwaka wa 2011 waliingia katika Dictionary of African Biography (DAB).
 
Kuwa na idadi ya wateule bila kupepesa ni sifa ndizo zinafanya wateuliwe, sasa mfano darasa lina watu wenye majina ya Kikristo 40 ,Islam 10 unategemea nini hapo? Anzeni chini chini Ng'ombe hanenepi siku ya mnada viongozi wana andaliwa, pita mashuleni uone idadi zao ndiyo utajua.
 
Ulweso,
Sawa lakini itapendeza jibu hilo Waislam walisikie kutoka serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…