Mnaacha Kuwaombea Watanzania wengi wenye Shida mbalimbali 'Mnajipendekeza' Kumuombea Mtu ambaye ni Tajiri hadi Umauti wake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Watumishi wa Mungu Tanzania wakiongozwa na Mtume @mtume_boniface_mwamposa wameandaa kongamano maalumu kwa ajili ya kumuombea Dua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. @samia_suluhu_hassan na kuliombea Dua Taifa la Tanzania liepukane na migogoro ya kisiasa, vita na kila aina ya baya linaloikumba Nchi yetu.

Kongamano hilo litafanyika Febuari 28 mwaka huu katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni kuanzia majira ya saa 8 za mchana hadi jioni.

Chanzo: manaratv

Mwamposa tunajua unajipendekeza sana Kwake ili yale mambo yetu unayoyaingiza na kuyafanya TZ yasibughudhiwe.
 
Mwambie pia swaiba wako wakukutukuka Mch Mwamposa, haki na usawa huleta amani na wala hauhitaji maombi.

Kukiwa na haki na usawa automatically tu Taifa linabarikiwa bila maombi.

Wachungaji wajikite kuwaambia watawala watende haki na kuleta usawa miongoni kwenye jamii.
 
Kudos.
 
Haha! shida sio hiyo shida huelewi namna vitu vinavyoenda!.
 
Viongozi waliombewa kitaifa tangu enzi za mapambano ya uhuru wa tanganyika......
 
Ubinafsi uliotukuka ,na mara nyingi watu wa hivyo huwa ni waovu sana,sasa ili wasifatiliwe lazima wajipendekeze kwa wakubwa
 
Kwa hiyo hutaki raisi wa nchi aombewe
 
waombee mvua Dar joto nikali sana na upepo ndio unahisha kabisa mvua kwenda bara
 
Acha wamuombee tu...
Sisi maskinini tunahitaji utajiri sio maombi.

🤔Ila nae atakanyaga mafuta na kuuziwa maji na kalenda ya upako au anapewa tubure
 
Kama wewe ni Christian chukua hii
1 Timothy 2:1-2
[1]
Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
[2]
kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
 
Hata hilo la kulalamika? Kwanini usiwaombee hao unaona wanastahili kuombewa? Samia ameshabarikiwa mnajiumiza bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…