Aahahahaaaahahaa umenifanya nitabasamu huku naangalia dirishani jinsi matone ya mvua yanavyogonga ardhini na kutuama juu ya uso wa nchi.
Acha uchokozi banaa..... aahahahaha
Kwani, alikusimulia hili tukio...?
Umejuaje ndo huyo niliyekutana naye?
Ilikuwa ndo tabia yake hadi akapata mke kwa style hiyo?
Yawezekana ni kweli, maana alikuwa rangi kama yangu si mweusi si mweupe ila mrefu kiasi cha kusema ni mmasai...
Taswira yake siikumbuki, ila hilo tukio halinitoki sijui kwanini hata....!!!🤔🤔🤷♀️🤷♀️🤷♀️🤷♀️
Well, pia huwezi jua, kupishana na lifti ya hela si ajabu nisingewezana nayo....
Malezi niliyokulia tofauti na waschana wa kisasa....
Kuna vipaumbele nilifunzwa kuviangalia kwa mwanaume na si mali au pesa au nyadhifa....
Isitoshe, mara nyingi, watoto au familia za nyoka huwa wanaoana wenyewe kwa wenyewe... ngumu sana kama sina chimbuko la nyoka nikaolewa kwenye familia ya nyoka...
Wewe sema ukweli kuwa umetania tuu, ila mie nimesimulia ukweli wa tukio halisi.