View attachment 2538313
Baada ya kuupima mziki wa ghorofa na kuona ni kina kirefu sasa nahamia rasmi kwenye mabangaloo aka Freemason.
Kuna floor plan ya huyo mwamba hapo. Naombeni maoni yenu na kukosoa kwingi kabla sijamchek
1.Ni ngumu ku-comment kindaga ubaga kama hamna Plot Plan/Block plan hapo. Kuna ile alama kuonesha North ,ni muhimu kuliko watu wanavyofkiri.
Mana hakuna anayejua.
-Kuzama na Kuchomoza kwa jua.
-Uelekeo wa upepo
2.Haijarishi mwanga utatokea upande gani...
-Korido yako itakuwa na kiza mchana.
-Sebureni Mwanga ni hafifu.Paa la verandah lime-extend parfum
3.Weka Open Floor plan,kati ya Sebure,Jiko na Dinning,,,la sivyo jiandae kwa joto.
-Hakuna mzunguko wa Hewa
4.Store,Kama una makabati ya chini na ya juu...kwa ukubwa nyuma yako,store haina umuhimu sana.
5.Privacy,kuna mdau ametaja choo,nami nakazia
NB
Mwite afike site, akusanifie ramani inayoendana na Kiwanja chako....