Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Ni picha ya kumbukumbu nayowaleteeni hapa Jukwaani ikiwa inaonyesha Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete Rais mstaafu wa awamu ya Nne ambaye pia ni Mwanajeshi mstaafu lakini pia waweza kumwita Jasusi Imara na Komandoo wa Mikakati .Akikumbatiana kwa tabasamu na bashasha kubwa sana na Rais Wa Awamu ya Tano Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Joseph Magufuli.
Huku Pembeni yao kukiwa na Marais watatu pichani ambao kati yao wawili bado wapo hai na bado wapo madarakani,ambao ni Mheshimiwa Paul Kagame wa Rwanda pamoja na Yoweli Kaguta Museveni Wa Uganda pamoja na mmoja ambaye ametangulia mbele za Haki Hayati Robert Mugabe wa Zimbabwe moja ya Marais waliokuwa na kauli za misimamo kwelikweli kutetea masuala mbalimbali ya Afrika na waafrika.
Sasa somo nalopenda kuwapeni na mnalopaswa kujifunza na kuelewa ni Kuwa Tanzania chini ya uongozi thabiti wa serikali ya CCM itaendelea kuwa yenye amani na utulivu kwa miaka mingi sana. CCM kamwe na katu haiji kutolewa wala kuyumbishwa madarakani. Hii ni kutokana na kubadilishana na kupokezana kwa madaraka kwa njia ya Amani na upendo mkubwa kabisa.
Hali hiyo inapelekea hata wananchi kutoichoka wala kuikinai wala kuikifu CCM na serikali yake. Kwa sababu kila baada ya miaka kumi wanaona CCM mpya na yenye mawazo ,fikira ,mtizamo ,mipango, mikakati,sera,ajenda,maono ,ndoto,kiu ,kauli na kauli mbiu mpya kabisa lakini zenye lengo la kuinua maisha ya watu,kugusa na kuboresha maisha ya wengi,kuleta usawa katika nyanja zote na kuwahudumia wananchi kwa ukaribu mkubwa huku masikio ya serikali yakiwa na usikivu wa hali ya juu kwa shida na kero za watu.
Kila baada ya miaka kumi watanzania wanapewa sura mpya na yenye mawazo mapya yenye kubeba matamanio,kiu ,ndoto na matarajio ya mamilioni kwa mamilioni ya watanzania. Ndio Maana utaona baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi .
utaona CCM ya wakati wa Hayati Benjamini Mkapa ni tofauti na ile ya wakati wa Mzee Daktari Jakaya Kikwete na pia CCM ya wakati wa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete ni tofauti ni ile ya wakati wa Hayati Dkt John Magufuli ,lakini pia CCM ya wakati wa Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan ni tofauti kabisa na ile CCM ya wakati wa mtangulizi wake Hayati Mwalimu Daktari John Magufuli.
Utofauti huo unajitokeza na kuonekana katika vipaombele,ajenda ,sera , mikakati na uwekezaji. Mfano utaona katika suala la ajira na mishahara wakati wa mzee Kikwete na Daktari Samia ni tofauti na wakati wa Hayati Magufuli. Vipaombele pia ni tofauti katika awamu hizo tatu. Lakini pia hata mazingira ya sasa ni tofauti pia na mazingira ya wakati uliopita.
Hali hii inapelekea hata wananchi kuwa na matumaini mapya katika kila awamu. Kwa sababu CCM imekuwa na utamaduni wa kubeba na kusikiliza sauti ,matamanio na kiu za watu na kuziweka katika ilani na hatimaye katika utekelezaji wake.
Hii ndio sababu huwezi ukawaambia watanzania waandamane barabarani kuiondoa CCM madarakani. Kwa sababu wanapewa kila wakitakacho katika kila awamu .hali hii imepelekea hata wapinzani kubadilika kimisimamo dhidi ya CCM kulingana na wakati na kuamua kujiunga na CCM. Utakuta mtu aliyekuwa anaisakama CCM awamu hii,utakuta kesho amejiunga CCM katika awamu nyingine ya CCM na Rais wake.hivyo CCM imetengeneza mfumo wa kutokuwa na adui au mpinzani wa kuiandama kwa awamu zote .
Ndio maana leo hii mnaona watu kama akina Mheshimiwa David Kafulila, mtela Mwampamba,Juliana Shonza,Kitila Mkumbo,Julius mtatiro ,peter msigwa,peter Lijuakali,Joshua Nasari, Vincent Mashinji ,Upendo Peneza,Mwita Waitara, Paulina Gekul ,Patrobas Katambi na wengine wengi sana wapo CCM na wanaendelea kuisifu na kuipongeza kwa nguvu zote .japo waliisakama sana CCM siku za nyuma na kuapa kwa viapo vikali sana kwamba hawawezi kamwe kujiunga CCM. Lakini leo wapo CCM wanapendeza na wanaisemea vizuri CCM na kujitoa kwa kila hali kuitumikia CCM kwa uzalendo.
Kwanini wapo CCM? Kwa sababu CCM hubadilika kulingana wakati na kuja na kila kitu kipya kila awamu. Kwa hiyo mtu anajikuta kama awamu hii alikuwa hakubaliani na mambo fulani ya CCM,anajikuta amenaswa na kuvutiwa na Rais fulani wa awamu fulani kutoka CCM hiyo hiyo ya wimbo ule ule wa CCM mbeleee kwa mbeleee,Au sasa kumekuchaa Jogoo limekwisha wika Dodoma.
Au wewe muangalie hata Dkt Slaa japo hayupo CCM lakini utagundua Dkt Slaa wa wakati wa Dkt Jakaya Kikwete ni tofauti na yule Dkt Slaa wa wakati wa Hayati Dkt Magufuli. Ambapo Dkt Slaa wa wakati wa Kikwete asingeweza kukubali kupewa hata ubalozi. Lakini Dkt Slaa wa wakati wa Hayati Magufuli alikubali kupewa Ubalozi na kuitumikia nafasi hiyo na kuisifu sana serikali ya CCM ileile iliyoongozwa na Dkt Jakaya Kikwete. Hata Zitto Kabwe tu japo hayupo CCM lakini utaona ni tofauti na yule zito wa awamu ya Tano au ya nne. CCM inajua namna ya kucheza na akili za wapinzani.siasa ni sayansi.
Lakini kwa hao wengine pichani unakuta wapo madarakani Tangia miaka na miaka mpaka wengine vijana wamezaliwa na sasa wamepita miaka ya ujana lakini wanajikuta wanaongozwa na mtu yule yule waliyemkuta wakati wanazaliwa. Naomba niishie hapa ndugu zangu. Ila kiukweli naipenda sana tena sana CCM. Nakipenda hiki chama kwa dhati ya moyo wangu. Nipo tayari kutukanwa na kuitwa chawa na kupe kwa sababu ya CCM. Nipo tayari kudhalilishwa kwa matusi ya aina yoyote ile kwa sababu ya CCM na bado nitaendelea kuipenda CCM yangu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.