Mnakumbuka tukio la majambazi kuvamia Pugu Secondary mwaka 2003?

Mnakumbuka tukio la majambazi kuvamia Pugu Secondary mwaka 2003?

TheGreatest Of AllTime

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2025
Posts
207
Reaction score
679
Mnakumbuka tukio la majambazi kuvamia pugu sec mwaka 2003 hadi kupelekea mauaji ya mwanafunzi mmoja?

Wenye stori kamili tunaomba mtupatie

Rest Easy Mwamba


Screenshot_20260810_090846_Instagram.jpg

Res
 
Sasa miaka hiyo pesa za mishahara nk,zilikuwa zinapelekwa mashuleni
Mfumo wa kibenki ulikuwa hautumiki
Anyway hao majambazi walikuwa njaaa kali

Ova
Zamani ada na michango mingine ilikuwa ikilipwa shuleni kwenye ofisi ya bursor na inawezekana ikahifadhiwa hapo kabla ya kupelekwa bank kesho yake.

Jamaa walivamia kwa lengo ya kuiba hizo pesa.
Duh! Kweli tumetoka mbali..
 
Kuna mtu kaniambia hapa, Jamaa kwanza alikuwa sukari ya warembo, wale wadada wa evening program, Form Six 2003- EGM, mpole sana.

Nazidi kusimuliwa hapa, wale majambazi walivamia usiku kama wa saa moja hadi saa 4 usiku wakitokea pori la kambini kwa bakabaka.

Naambiwa, zamani mshahara ulikuwa unaletwa, au pesa yoyote ilikuwa inaletwa, sio benki kama sasa, jamaa wakanusa, wakavamia pale jengo la Utawala kwa mhasibu, kulikuwa na madarasa na wengine walikuwa wanasoma nje.

Zikapigwa juu pyu pyu, ikatoka amri hakuna kukimbia, jamaa akakimbia wenzake wakalala chini, akapigwa ya mguu, mpaka anafika hosptali damu zimevuja za kutosha. AKAFARIKI.

Naambiwa, vijana wa Mabweni ya Mapinduzi, Ujamaa na wale waliokuwa madarasa ya nyuma, wakaanza kukimbia kuelekea porini uelekeo wa Kisarawe.

Naambiwa, majambazi hayakuiba kitu, walishindwa kuvunja lile kabati la chuma kwa burser. Wakaondoka.

Alibakiza miezi isiyozidi mitatu kumaliza Form Six 2003. Tukio lilitokea kati ya Februari na Mei 2003.

Namuambia huyu boss aliyenipa stori, inawezekana kiroho, dhumuni halikuwa pesa, dhumuni lilikuwa huyu kijana ambaye leo angekuwa Msomi mbobevu wa Uchumi, Uhasibu nk. Roho chafu huwa zinamfuata mtu popote, zinaweza kutoka Kijiji cha MASAKI, KISARAWE zikamfuata mtu mwenye feature huko PARIS, UFARANSA ili zitimize lengo la maagano ya uharibifu kwa sababu nyepesi tu.

RIP TEDSON MASATU
 
Mimi story yake niliiskia kwa juu juu tu kwa mmoja ya watu aliosoma nao kuwa alikuwa anatoka kucheki game akapigwa pyu pyu maeneo ya mguu na alifariki kwa kuvuja damu nyingi sana maana baada ya huduma ya kwanza kushindikana kabla ya kufika hosptali jamaa alikuwa kiongozi wa michezo....ngoja waje watu wa pugu waeleze vizuri
 
Kuna mtu kaniambia hapa, Jamaa kwanza alikuwa sukari ya warembo, wale wadada wa evening program, Form Six 2003- EGM, mpole sana.

Nazidi kusimuliwa hapa, wale majambazi walivamia usiku kama wa saa moja hadi saa 4 usiku wakitokea pori la kambini kwa bakabaka.

Naambiwa, zamani mshahara ulikuwa unaletwa, au pesa yoyote ilikuwa inaletwa, sio benki kama sasa, jamaa wakanusa, wakavamia pale jengo la Utawala kwa mhasibu, kulikuwa na madarasa na wengine walikuwa wanasoma nje.

Zikapigwa juu pyu pyu, ikatoka amri hakuna kukimbia, jamaa akakimbia wenzake wakalala chini, akapigwa ya mguu, mpaka anafika hosptali damu zimevuja za kutosha. AKAFARIKI.

Naambiwa, vijana wa Mabweni ya Mapinduzi, Ujamaa na wale waliokuwa madarasa ya nyuma, wakaanza kukimbia kuelekea porini uelekeo wa Kisarawe.

Naambiwa, majambazi hayakuiba kitu, walishindwa kuvunja lile kabati la chuma kwa burser. Wakaondoka.

Alibakiza miezi isiyozidi mitatu kumaliza Form Six 2003. Tukio lilitokea kati ya Februari na Mei 2003.

Namuambia huyu boss aliyenipa stori, inawezekana kiroho, dhumuni halikuwa pesa, dhumuni lilikuwa huyu kijana ambaye leo angekuwa Msomi mbobevu wa Uchumi, Uhasibu nk. Roho chafu huwa zinamfuata mtu popote, zinaweza kutoka Kijiji cha MASAKI, KISARAWE zikamfuata mtu mwenye feature huko PARIS, UFARANSA ili zitimize lengo la maagano ya uharibifu kwa sababu nyepesi tu.

RIP TEDSON MASATU
🙄🥹🥹🥹
 
Jamaa alitoka kuangalia mechi. Sasa amefika maeneo ya darasani anasikia milio ya risasi akawa anakimbia ndio Majambazi wakampiga risasi. Majambazi hawakuwa na lengo la kumuuwa Bali walitoa amri watu walale chini, yeye hakujua hilo alikuta amri ilishatoka. Hivyo alivyosikia milio ya risasi akakimbia mbio ndio Majambazi wakamlima risasi.
 
Inasikitisha sana ,hao majambawazi walifata MCHUZI tu ,kama lengo lilikuwa kumuua huyo kijana wasingempiga ya mguu,alijichanga kukimbia kama wadau walivyosema.

Zamani majambazi walikuwa ni maaskari wetu(Polisi/wajeda) wakikosa pesa wanaingia field kuiba.

Hii ni fact! Gen-Z hawaamini kabisa ukiwaambia longtime, mandata, njagu, maafande ndio walikuwa wakichukua hela na mikwaju! Tumetoka mbali hii nchi. 😊
Benki mjini kati inavamiwa, safe zinavunjwa watu wanatokomea na mpunga, ndio mapoti wanajitokeza! 😊
 
Sasa miaka hiyo pesa za mishahara nk,zilikuwa zinapelekwa mashuleni
Mfumo wa kibenki ulikuwa hautumiki
Anyway hao majambazi walikuwa njaaa kali

Ova
Mkuu kipindi hicho na nyuma yake majambazi yanayotumia silaha walikuwa wengi hasa Dar. Nakumbuka mjomba wangu alikuwa na maduka ya jumla Dar, wakamlia ''timing'' asubuhi kama saa nne anapeleka fedha za mauzo za jana yake benki. Ile anatoka mlangoni mwa duka, ikaja gari moja kwa kasi sana na kuamuru kila mtu alale chini. Alikuwa na watu wengine wawili na wote wakatii. Baada ya majambazi kuchukuwa fedha wakaamua kupiga risasi chini, ikatifua mchanga. Waliendlea kulala kama dakika tano wakati majambazi wameshaondoka. Na mbaya zaidi mjomba alijinyea hivyo alivyo alivyoamka uharo ukawa unachuruzika.
 
Cashless economy ni nzuri sana, imepunguza ujambazi wa silaha kwa asilimia kubwa sana. Enzi za yule Bwana wa ngunguri, ilikuwa kuvamiwa na majambazi dakika tu. Changamoto sasa imekuwa, wizi wa kimtandao, hawa wanaofanya hivi wengi ni wale wavaa tai kwenye hizo taasisi.
 
Back
Top Bottom