Mnakumbuka tukio la majambazi kuvamia Pugu Secondary mwaka 2003?

Mnakumbuka tukio la majambazi kuvamia Pugu Secondary mwaka 2003?

2003 walimu walifuata mishahara yao halmashauri na kupanga foleni dirishani kupokea pesa taslimu.

Hilo la mishahara kupelekwa shuleni ni jipya! Labda walifuata ada na michango mingine ya wanafunzi sababu ililipwa cash shuleni.
 
Sasa miaka hiyo pesa za mishahara nk,zilikuwa zinapelekwa mashuleni
Mfumo wa kibenki ulikuwa hautumiki
Anyway hao majambazi walikuwa njaaa kali

Ova
Mishahara walikua wanapokelea bomani/ halmashauri/ wilayani tena dirishani wanapanga foleni. Ila hela zote za shule kuanzia ada na michango mingine ilikua inapokelewa/ kukusanywa na kutunzwa shuleni kabla ya kupelekwa Bank/ wilayani ama kokote panapohusika. Na hiyo ndo ilikua kazi ya muhasibu wa shule. Kesi za Walimu wakuu/ wakuu wa shule kula hela zilikua nyingi sana kipindi hicho. Ila kesi za shule kuvamiwa kwa ajili ya kuiba hela hazikua nyingi kwa kiwango hicho. So hoja ya kwenda kuiba hela inaweza kua kweli ngoja tuwasubiri wajuvi wa mambo waje watupe full stori ilikuaje
 
Cashless economy ni nzuri sana, imepunguza ujambazi wa silaha kwa asilimia kubwa sana. Enzi za yule Bwana wa ngunguri, ilikuwa kuvamiwa na majambazi dakika tu. Changamoto sasa imekuwa, wizi wa kimtandao, hawa wanaofanya hivi wengi ni wale wavaa tai kwenye hizo taasisi.
Safari moja huanzisha nyingine# Makosha kwa sauti ya DJ AFRO KIMODA😀
 
Kuna mtu kaniambia hapa, Jamaa kwanza alikuwa sukari ya warembo, wale wadada wa evening program, Form Six 2003- EGM, mpole sana.

Nazidi kusimuliwa hapa, wale majambazi walivamia usiku kama wa saa moja hadi saa 4 usiku wakitokea pori la kambini kwa bakabaka.

Naambiwa, zamani mshahara ulikuwa unaletwa, au pesa yoyote ilikuwa inaletwa, sio benki kama sasa, jamaa wakanusa, wakavamia pale jengo la Utawala kwa mhasibu, kulikuwa na madarasa na wengine walikuwa wanasoma nje.

Zikapigwa juu pyu pyu, ikatoka amri hakuna kukimbia, jamaa akakimbia wenzake wakalala chini, akapigwa ya mguu, mpaka anafika hosptali damu zimevuja za kutosha. AKAFARIKI.

Naambiwa, vijana wa Mabweni ya Mapinduzi, Ujamaa na wale waliokuwa madarasa ya nyuma, wakaanza kukimbia kuelekea porini uelekeo wa Kisarawe.

Naambiwa, majambazi hayakuiba kitu, walishindwa kuvunja lile kabati la chuma kwa burser. Wakaondoka.

Alibakiza miezi isiyozidi mitatu kumaliza Form Six 2003. Tukio lilitokea kati ya Februari na Mei 2003.

Namuambia huyu boss aliyenipa stori, inawezekana kiroho, dhumuni halikuwa pesa, dhumuni lilikuwa huyu kijana ambaye leo angekuwa Msomi mbobevu wa Uchumi, Uhasibu nk. Roho chafu huwa zinamfuata mtu popote, zinaweza kutoka Kijiji cha MASAKI, KISARAWE zikamfuata mtu mwenye feature huko PARIS, UFARANSA ili zitimize lengo la maagano ya uharibifu kwa sababu nyepesi tu.

RIP TEDSON MASATU
Kweli kabisa mkuu huenda walimroga huyu watu wa kijijini kwao kwa sababu hao majambazi mwisho wa siku hata hawakuchukua chochote


Cc LIKUD
 
Zamani ada na michango mingine ilikuwa ikilipwa shuleni kwenye ofisi ya bursor na inawezekana ikahifadhiwa hapo kabla ya kupelekwa bank kesho yake.

Jamaa walivamia kwa lengo ya kuiba hizo pesa.
Hapana mishahara huchukuliwa huko itokako na kugawiwa kwa mtumishi mmoja mmoja. Tuliita mishahara dilishani
 
Sasa miaka hiyo pesa za mishahara nk,zilikuwa zinapelekwa mashuleni
Mfumo wa kibenki ulikuwa hautumiki
Anyway hao majambazi walikuwa njaaa kali

Ova
Mishahara? Sio kweli bwana, huo mwaka kama sikosei hata ATM zilikuwepo. Hata miaka ya 90 huko haukuwepo utaratibu wa kupeleka mishahara shuleni
 
Back
Top Bottom