Mnakumbuka tukio la majambazi kuvamia Pugu Secondary mwaka 2003?

Mnakumbuka tukio la majambazi kuvamia Pugu Secondary mwaka 2003?

Hao majambazi walifuata nini shuleni chaki au madaftari, hii stori ina nini ndani yake...!
Nini shule?!huu mwaka pale Msimbazi Police Station waliingia wezi majira ya 09:40 AM wakaondoka na mishahara ya askari wote wa kituo.

Hiyo miaka ilikuwa haangaliwi anaibiwa nani bali walikuwa wanaangalia kilichopo popote pale alimradi pana kitu.
 
Mkuu kipindi hicho na nyuma yake majambazi yanayotumia silaha walikuwa wengi hasa Dar. Nakumbuka mjomba wangu alikuwa na maduka ya jumla Dar, wakamlia ''timing'' asubuhi kama saa nne anapeleka fedha za mauzo za jana yake benki. Ile anatoka mlangoni mwa duka, ikaja gari moja kwa kasi sana na kuamuru kila mtu alale chini. Alikuwa na watu wengine wawili na wote wakatii. Baada ya majambazi kuchukuwa fedha wakaamua kupiga risasi chini, ikatifua mchanga. Waliendlea kulala kama dakika tano wakati majambazi wameshaondoka. Na mbaya zaidi mjomba alijinyea hivyo alivyo alivyoamka uharo ukawa unachuruzika.
Aise

Ova
 
Kuna mtu kaniambia hapa, Jamaa kwanza alikuwa sukari ya warembo, wale wadada wa evening program, Form Six 2003- EGM, mpole sana.

Nazidi kusimuliwa hapa, wale majambazi walivamia usiku kama wa saa moja hadi saa 4 usiku wakitokea pori la kambini kwa bakabaka.

Naambiwa, zamani mshahara ulikuwa unaletwa, au pesa yoyote ilikuwa inaletwa, sio benki kama sasa, jamaa wakanusa, wakavamia pale jengo la Utawala kwa mhasibu, kulikuwa na madarasa na wengine walikuwa wanasoma nje.

Zikapigwa juu pyu pyu, ikatoka amri hakuna kukimbia, jamaa akakimbia wenzake wakalala chini, akapigwa ya mguu, mpaka anafika hosptali damu zimevuja za kutosha. AKAFARIKI.

Naambiwa, vijana wa Mabweni ya Mapinduzi, Ujamaa na wale waliokuwa madarasa ya nyuma, wakaanza kukimbia kuelekea porini uelekeo wa Kisarawe.

Naambiwa, majambazi hayakuiba kitu, walishindwa kuvunja lile kabati la chuma kwa burser. Wakaondoka.

Alibakiza miezi isiyozidi mitatu kumaliza Form Six 2003. Tukio lilitokea kati ya Februari na Mei 2003.

Namuambia huyu boss aliyenipa stori, inawezekana kiroho, dhumuni halikuwa pesa, dhumuni lilikuwa huyu kijana ambaye leo angekuwa Msomi mbobevu wa Uchumi, Uhasibu nk. Roho chafu huwa zinamfuata mtu popote, zinaweza kutoka Kijiji cha MASAKI, KISARAWE zikamfuata mtu mwenye feature huko PARIS, UFARANSA ili zitimize lengo la maagano ya uharibifu kwa sababu nyepesi tu.

RIP TEDSON MASATU
Ted alikuwa mtu wa watu,mcheshi,jasiri,mwanamichezo,alicheza na kupenda sana mpira wa miguu.

Wengi tulimfahamu na kumchukulia kama kaka shuleni.Binafsi,alikuwa vidato vitatu mbele yangu ngazi ya O-level huko Kantalamba Sec school.

Rest easy Ted.
 
Hii ni fact! Gen-Z hawaamini kabisa ukiwaambia longtime, mandata, njagu, maafande ndio walikuwa wakichukua hela na mikwaju! Tumetoka mbali hii nchi. 😊
Benki mjini kati inavamiwa, safe zinavunjwa watu wanatokomea na mpunga, ndio mapoti wanajitokeza! 😊
Kabisa ,kuna askari wa KJ34 miaka ya nyuma ilikuwa michezo yake lakini alikuja kustukiwa.
 
Wanafunzi wa kipindi cha nyuma walikuwa wana miili na muonekano wa kikubwa tofauti na miaka ya hv karibuni
Aendelee kupata pumziko lililo jema Amen

secretarybird unamkumbuka wa umbwe huku nikiwa nimekuficha chini mto wa Tacri, mm kakako aseeh
Hapa umenikumbusha kipindi naenda kuriport form five tulikua na mdada mmoja alikua na umbo kubwa Sana mw.akampa shampoo akijua ni mzazi.
 
Hapa umenikumbusha kipindi naenda kuriport form five tulikua na mdada mmoja alikua na umbo kubwa Sana mw.akampa shampoo akijua ni mzazi.
Aaan
Hapa umenikumbusha kipindi naenda kuriport form five tulikua na mdada mmoja alikua na umbo kubwa Sana mw.akampa shampoo akijua ni mzazi.
i walikuwa wakubwa mno, me nilikuwa kama mtoto wao 😂
 
Mkuu kipindi hicho na nyuma yake majambazi yanayotumia silaha walikuwa wengi hasa Dar. Nakumbuka mjomba wangu alikuwa na maduka ya jumla Dar, wakamlia ''timing'' asubuhi kama saa nne anapeleka fedha za mauzo za jana yake benki. Ile anatoka mlangoni mwa duka, ikaja gari moja kwa kasi sana na kuamuru kila mtu alale chini. Alikuwa na watu wengine wawili na wote wakatii. Baada ya majambazi kuchukuwa fedha wakaamua kupiga risasi chini, ikatifua mchanga. Waliendlea kulala kama dakika tano wakati majambazi wameshaondoka. Na mbaya zaidi mjomba alijinyea hivyo alivyo alivyoamka uharo ukawa unachuruzika.
Ila we jamaa unamatatzo asee unamtania mjomba kama mtani wako duh
 
Back
Top Bottom