Mnaoamini Mungu, kwenye vichwa vyenu mna "imagine" sawa jinsi alivyo?

Ilitarajiwa ushindwe kumuelezea huyu Mungu wa level nyingine. Sasa unamuelezea kirahisi tu. Mungu ni wa level yetu kabisa. Tatizo linaanzia pale unapomuogopa. Mungu ni uwepo, na kumbuka usipokuwepo, hakuna kilichopo. Uwepo ni ukamilifu, hali nadhifu kabisa isiyo na doa. Ukamilifu ni upendo, unyenyekevu na kila tendo jema unalofikiri unapaswa kutendewa. Sasa ni ajabu kuu mno kuwaza kuwa Mungu ni level nyingine.

Ni ajabu kuu pia kusema unaogopa upendo, unyenyekevu, unadhifu. Ni ajabu kabisa.
 
Bila kujali unaamini nini kama Mungu wako, ikiwa imani yako ipo kwenye misingi ya kujali mahitaji ya utu,utaendelea kuwa sahihi katika maisha yako yote ndugu. Zingatia hili na utaona namna maisha yalivyo rahisi. Huwezi kusumbuka sana kuhusu Mungu.
 
Usawa pekee unaopaswa kuwa vichwani mwetu ni kulinda na kutetea maslahi ya utu, basi.
 
Huwezi kushindwa kueleza, hata moja?
OK !, Mambo Makuu aliyonitendea Mwenyezi Mungu ni 1.Kunipa Uhai, 2.Kunipa Riziki 3.Kuniepusha na hatari mbalimbali, km vile Magonjwa hatarishi mfano HIV na Magonjwa mengine ya zinaa, kuniepusha na ajali, n. K. 4.Kunifanya niwe hivi jinsi nilivyo 5.Kunipa Familia, Kwa Kweli ni Mengi mno siwezi kuelezea, kwa hakika Nitamsifu na Kumtukuza MUNGU wangu kwani ni Mwema Kwangu.
 
mkuu mungu yupo
ila hayupo kama wafia dini wanavyotaka tuamini MUNGU ALIKUWEPO,NA YUPONA ATAKUWEPO
MUNGU ni nguvu au uwezo beyond our imagination
we can't comprehend the imagination of our maker
GOD IS REAL
IMPERSONATION OF GOD IS WHAT BRINGS CONFUSION UPON US
 
Mkuu, waliopatwa na ajali, wenye hiv, wasiokuwa na familia, n.k wao hawana Mungu? Wanaopata madhila haya ni kama vile wanapewa adhabu au? Ila Mungu ni ukamilifu na katika ukamilifu hakuna adhabu. Binafsi ninachelea kuwa kinyume kidogo nawe.
 
Heshima kwako mkuu. Hapa umeuliza maswali mengi sana hivi kwamba ni vigumu kukujibu yote kwa urahisi. Wacha tujaribu, bila shaka kuna kitu utajifunza.

Kwa hali ya kawaida kuna tofauti kati ya vile tunaoamini Mungu tunamfikiria. Yaani hatufanani katika fikra za vile Mungu yuko. Ni sawa na uende kwa wanafunzi uulize 2+3=? wakikujibu ni 5. Usifikiri wote wanaifikiri 5 sawa, wako wanaoiona ni namba ndogo sana, wengine haigawanyiki, wengine kubwa sana,wengine shufwa, witiri, tasa etc,.... Jambo la msingi ni kuwa WOTE wako SAHIHI kuhusu swali la msingi 2+3=? Wanaoamini uwepo wa Mungu hawajatulia pasipo kuwasaidia wengine kuhusu mambo yanayofuata baada ya swali la msingi juu ya uwepo wa Mungu.

Na hii ndiyo sababu kuna juhudi kubwa ya kuelimishana kati ya watu wa dini tofauti. Yaani Yeyote anayeamini kuwa Mungu yupo anatakiwa kupongezwa kwamba amepatia kujibu swali la msingi, japokuwa yako maswali yanayofuata baada ya hapo( 50%+...). Kwa upande mwingine WANAOAMINI kwamba Mungu hayupo wamekosa swali la msingi hivyo hakuna uwezekano kabisa wa kupata maswali yote yanayoendelea baada ya hilo ( 0%)

Kuhusu vitabu hivi vya dini, havitumiki/havipaswi kutumiwa sana kama ushahidi pekee/mkuu wa uwepo wa Mungu, hivi hutumika kwa watu ambao wamekwisha kuamini uwepo wa Mungu kupitia ushahidi mwingine kutegemeana na ufahamu/uelewa binafsi wa mambo. Kuna ushahidi wa muhimu kuhusu uwepo wa Mungu tofauti na kutumia vitabu vya dini.
 
Heshima kwako mkuu.

Ikiwa mna uhakika kuwa Mungu hayupo kiasi cha kuwa 'fact'- bila shaka mtakuwa na ushahidi Fulani. Waweza kutupa ushahidi hata mmoja tu kuthibitisha hilo? Isijekuwa unajiita tu jina bila kuwa na chochote cha kuhalalisha nafasi yako.
 
Wewe uliyejifunza dini nyingine ukajihakikishia upo sahihi ndo useme hicho unachokiamini (kuhusu maswali yako)

Eti maswali..!? Hoja zenyewe hazina hata mashiko
 
Hiyo aya ya mwisho umenichanganya kabisa bosi, kwamba kama una imani dhaifu hutakiwi kujifunza imani zingine??
sasa si inatakiwa ujifunze na nyingine ili uijue ipi ina nafuu maana umesema haipo iliyokamilka.
Imani (dini) iliyokamilika ambayo utaona haina mapungufu ni ile unayoifuata na kuongozwa kwayo.

Imani Zingine zote ambazo husimami kwazo utaona zina mapungufu

mfano huyu mleta mada yeye dini yake ni hakuna Mungu mwenye enzi
 
Kiti au meza hata kiwe kizuri vipi hakiwezi kumjua seremala!!
 
When am in a deep Shit I call my lord and he always answer Me. Jesus Name has never failed me

Ukiniita kwa toba, nitaondoa laana kutoka katika nchi zenu na kuwabariki kwa baraka nyingi. Kama mtatubu na kuona aibu kwa ajili ya dhambi zenu, nitakuwa na huruma na kuwahurumia, na sitazikumbuka dhambi zenu tena. Omba kwamba uwe mshindi.
 
Imani (dini) iliyokamilika ambayo utaona haina mapungufu ni ile unayoifuata na kuongozwa kwayo.

Imani Zingine zote ambazo husimami kwazo utaona zina mapungufu

mfano huyu mleta mada yeye dini yake ni hakuna Mungu mwenye enzi
Sio kweli mkuu sema uoga huwa unatusumbua lakini ukifikiria vizuri utagundua hata dini tunazozifata huwa na udhaifu pengne kuliko hata tusizozijua
 
Huu uvivu huu kwa kweli mungu wenu awasaidie

Wala siyo uvivu labda kama hujaelewa ujumbe kwenye huo mstahili mfupi lakini ambao
Kwa Hakika ubeba karibu majibu yote ya maswali yako! Kwa ufupi pia ni kwamba walimu wa Elimu ni wengi sana lakini elimu ni Kimoja; japo image ya hiyo Elimu haiwezi kuwa sawa kwa Watu wenye kuimani.
 
Huwezi kutoa jibu kwa ujumla wa mitazamo ya wengine.

1. Mungu ni mmoja. Kwa vile hana mfano huwezi kumjengea taswira(imagination). Huwezi mfananisha.

2. Huwezi jibu swali lililopo akilini mwa MTU. Huwezi semea Fikra za Mtu.
Ila uhakika upo katika matendo na sheria.

3. Mungu hajatuagiza tumuwaze ila ametuagiza tushike sheria zake na kuwaza yaliyo mema.

4.Ndio nina uhakika dini niliyonayo ni sahihi. Sababu ni kuwa inanitaka nifuate kile Mungu alichokisema kuliko Mapokeo. Suala la wazazi kwenye dini kwa watu main halipo.

5. Ndio kwa kiasi kikubwa nimejifunza Dini nyingine kupitia Watu, mitandao na maandiko mbalimbali nikagundua nilipo ni sahihi zaidi.

6. Biblia ni sehemu ya maandiko ya Mungu japokuwa Mpangilio umepangwa na watu.

Hakuna mtu mwenye utashi wa Kuandika ile torati kwa zama zilizopita.

Maswali yako ni mepesi sana. Hakuna swali ulilouliza zaidi ya kuonyesha Mtagusano wako wa kifikra.
 
hv ushawahi kuuona upepo? kama ndiyo una rangi gani? upoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…