Mnaodai kuwa mmeibiwa kura tunaomba uthibitisho wa haya maswali ya msingi

Mnaodai kuwa mmeibiwa kura tunaomba uthibitisho wa haya maswali ya msingi

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,746
Reaction score
5,772
Watalaamu wa Sheria wanasema anayetoa shutuma ndie anayethibitisha. Iwe ni kwenye kesi ya aina yoyote ile.

CHADEMA na ACT-Wazalendo mnasema kuwa mmeibiwa kura. Na madai haya yamekuja baada ya matokeo kutoka.

Lakini kiuhalisia hivi mlitegemea watanzania wampigie kura Lissu? Maana mimi binafsi nikikaa na watu na kufanya nao mazunguzo ana kwa ana wengi utasikia wanatoa kauli moja tu, Rais Magufuli amepiga kazi na alistahili kushinda. Kwa ufupi wanakubali kazi alizofanya hasa kuimarisha kila sekta.

Baada ya matokeo,zimeibuka tuhuma kuwa kura zilipigwa kabla. Je zilipigiwa wapi? Ni akina nani walizipiga? Ni nani alizipeleka vituoni kwenda kuzijaza kwenye masanduku? Je mawakala wenu walikuwa wapi wakati haya yanafanyika?

Je, mna ushahidi gani wa kuweza kuuthibitishia umma na mahakama juu ya hizi tuhuma?

Ushahidi wa picha za watu wakichoma karatasi za kupigia kura huku sura zao hazionekani ni utoto, na kuleta picha kutoka Twitter za watu wameshika karatasi za kupigia kura ni utoto pia. Maana sidhani kama unakubalika mahakamani.
 
Ma changudoa nao wanajikita kwenye siasa.

Hakika tutaendelea kuona mengi.
Kama vile tulivyoona viongozi wa Dini waongo awamu hii.

Umeandika ki pumbavu sana.
Ni suala la kuthibitisha tu madai yenu wala huitaji kuleta kashfa kamanda.
 
Mkuu, mbona mambo ya uchaguzi yalisha isha..[emoji848] maana hata mkuu jana alitangaza na akarudia mara tatu.
Ndio kusema hamtaki kuthibitisha madai yenu? Na mahakamani hamuendi kudai ubunge na udiwani? Au mlikuwa mnawadanganya Watanzania baada ya kichapo kikali.
 
Mbona kuna threads nyingi humu zinaeleezea na kutoa mpaka clips za watu wamekutwa na kura zilizopigwa waliingia nazo kwenye vituo. Au husomi ila tu umeamua KUTURINGISHIA upunguani wako?
Hizo za watu wanachoma kura huku sura wameficha? Jibu maswali niliyouliza kamanda ni muhimu sana.
 
Shauri hili linatakiwa kupelekwa mahakamani, lakini katiba hairuhusu. Pia nina waswasi kama katiba hii iliridhiwa na wananchi, kama ilifanyika hivyo kupitia wabunge, basi hawakuwa na maslahi mapana ya taifa.
 
Shauri hili linatakiwa kupelekwa mahakamani, lakini katiba hairuhusu. Pia nina waswasi kama katiba hii iliridhiwa na wananchi, kama ilifanyika hivyo kupitia wabunge, basi hawakuwa na maslahi mapana ya taifa.
Halima Mdee anadai kukamata kura zilizoopigwa tayari. Anatakiwa aende mahakani la sivyo ni aibu kubwa kudanganya watanzania.

Kuhusu urais,Lissu alivyomaliza kupiga kura alisema mchakato umeenda vizuri. Kwa hiyo ni wazi kulikuwa hamna udanganyifu. Malalamiko yalianza baada ya matokeo kutoka.
 
Huu uzi nauhifadhi potelea mbali yaliyotokea lakini mimi nina imani na una bii aliotoa mtumishi wa Mungu mmoja mhindi mwaka 2015 na Nabii mwingine aliyetoa matukio ya mwak a 2020 hapo January 2020.

Kwenye msiba mkubwa nabii alikuwa sahihi MKAPA kaondoka kweli ingawa hakutaja jina, na pia kuhusu maradhi kutishia afya familia ya Kiongozi MKUU ni kwrli Corona ilitinga kwenye familia ya JPM kama alivyothibitisha mwenyewe na kwasababu ya corona alikuwa sahihi kwama uchumi utayumba kutokana na janga litalalokumba Taifa, mengine aliyochangia ni CCM kusema poo hata baada ya kushinda n.k

Mi naendelea kusubiri utabiri. Hivyo jipe ushindi kwa sasa.

Mi sipendi sera za kijinga za majimbo za Chadema. Lakini tunapenda Haki ili wote tuwe na Amani.

Wako watu wa Mungu Tanzania Mungu hawezi kuachia dhuluma isimame.

Tafadhali hifadhi post hii nawewe tutaonana yakitimia.

" Our laugh comes last"
 
Mh Rais kasema jana uchaguzi umekwisha.
Wewe huna adabu.
 
Mungu hapangiwi kazi yake. Usihusishe msiba wa binadamu na manabii wa uongo.

We thibitisha dhuluma iliyofanyika kwa kujibu nilichouliza.
 
Mh Rais kasema jana uchaguzi umekwisha.
Wewe huna adabu.
Kwa hiyo ndio kusema mlikuwa mnasingizia uongo baada ya kushindwa? Nafasi ya urais kwani mlikuwa mnaitaka? Wabunge na madiwani waende wakathibitishe hizi tuhuma...
 
Back
Top Bottom