minyoo
JF-Expert Member
- May 25, 2013
- 23,510
- 22,529
Naona unausaka uteuzi kwa nguvu lakini kama unakuja hivi laana inakunasa hupati uteuzi ng’oo , Tanzania hakuna uchaguzi umefanyika zaidi ya CCM kuulawiti kuubaka kuunajisi uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani hilo halina ubishi hata uje na Maelezo gani hakuna mwenye Akili timamu atakaa akubali utetezi wenu CCM kwani kila kitu kipo wazi hadi vipofu wanajua.Watalaamu wa Sheria wanasema anayetoa shutuma ndie anayethibitisha. Iwe ni kwenye kesi ya aina yoyote ile.
CHADEMA na ACT-Wazalendo mnasema kuwa mmeibiwa kura. Na madai haya yamekuja baada ya matokeo kutoka.
Lakini kiuhalisia hivi mlitegemea watanzania wampigie kura Lissu? Maana mimi binafsi nikikaa na watu na kufanya nao mazunguzo ana kwa ana wengi utasikia wanatoa kauli moja tu, Rais Magufuli amepiga kazi na alistahili kushinda. Kwa ufupi wanakubali kazi alizofanya hasa kuimarisha kila sekta.
Baada ya matokeo,zimeibuka tuhuma kuwa kura zilipigwa kabla. Je zilipigiwa wapi? Ni akina nani walizipiga? Ni nani alizipeleka vituoni kwenda kuzijaza kwenye masanduku? Je mawakala wenu walikuwa wapi wakati haya yanafanyika?
Je, mna ushahidi gani wa kuweza kuuthibitishia umma na mahakama juu ya hizi tuhuma?
Ushahidi wa picha za watu wakichoma karatasi za kupigia kura huku sura zao hazionekani ni utoto, na kuleta picha kutoka Twitter za watu wameshika karatasi za kupigia kura ni utoto pia. Maana sidhani kama unakubalika mahakamani.