Mnaofanya mazoezi ya kukimbia kuna mambo mnadanganya

Mkuu toa location tuje tutoane upepo .

Sent from my CPH2349 using JamiiForums mobile app
Mkuu siko nchini halafu pia kwa sasa bado hali dhoofu mno. Kwa dakika 15 nimekimbia 2.25km tu. Hii ni hali mbaya sana. Lakini leo nimeona maendeleo kidogo kwasababi jana nilikimbia 2.19km kwa dakika 15. Nimejiwekea malengo ya kufikisha 3km kwa dakika 15 kisha nistaafu kwa heshima barabarani na kuhamia Gym.
 

Attachments

  • IMG-20230916-WA0023.jpg
    81.3 KB · Views: 7
Kulimbia ni swala jingine na kupungua kwasababu umekimbia ni jambo jingine.

Kuna level ya mwili ukifikia haupungui.

Yani kwenye ile minyama uzembe ukifanya zoezi itajikaza tu lakini usifikirie kuwa utakuwa slim.

By the way Sammo Hung namfuatilia sana
 
Kati ya vitu vinakata mwili uzembe ni kukimbia ndio maana wale Wakenya wanaochukua medali unaona mifupa tuu ila wakiacha mbio za medali mwili unakua kawaida ila wakimbiaji wengi hawa wa Road nawaona na Ubonge wao ni kama wanatafuta appetite tu ya kuendelea kula sana...
 
Huyo sommo hung ni nani? Unamfwatilia kwa mtandao gani? Nami ni mdau wa mazoezi hasa kukimbia mkuu
 
😳Jomoni yaani tangu kipindi bado hujasogea hata kufikasha km4😂 ? kwahiyo bado unaishia nusu km halafu roho inataka kukutoka.....
punguza ubonge bana, umezidi kuwa kibonge dah
 
Dont hate bro, be inspired. Mimi kwa wiki nina ratiba ya mazoezi siku 5 katika siku 7 ila mara nyingi huwa nafanya mazoezi mara 4 kwa wiki. Katika hizo 4 huwa nazigawa kwa siku mbili ni kukimbia (mostly 5~8kms) na kuruka kamba. Hizi siku 2 nyingine nafanya calisthenics.

Sasa mwanzo nilikua napata shida sana kumaliza hata km2 bila kupumzika ila baadae nikaanza kuzoea mpaka sasa naona kawaida tu.
 
Oyaa mi nakamua 4km, zamani ilikua dry mwanzo mwisho. Ila sasa utu uzima ushanijia nafanya run and walk ya hizohizo 4km. Yaani nakimbia nikiona roho inataka kuchomoka nawalk nikirecover na run tena.
Mazoezi sio vita fanya pumzi yako inapoishia. Usijedondoka barabarani buree.
 
Mkuu utu uzima ndiyo umri gani?
Maana kuna watu wako zaidi ya miaka 60 wanakimbia half marathon.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…