Mnaofurahia Mikopo, Sri Lanka pia iIianza kama sisi

Na kwa Nini ukope na gesi asilia madini,bahari Kama sio UZUZU
Gesi asilia,Madini lukuki,Mafuta chini ya Ardhi,Bahari kuu,Maziwa makuu,Misitu asilia,Hifadhi za taifa ziko 22,Ardhi yenye rutuba,Mito mikuu inayotiririsha maji mwaka mzima non stop nk...nk....
 
Na kwa Nini ukope na hapo una gesi asilia madini,bahari Kama sio UZUZU huo
Ww kwa akili yako unahisi ivyo vyote vinaweza kuendesha nchi iwatengenezee miundombinu ilipe mishahara na hapohapo iwapunguzie gharama za maisha na kulipa Kodi mataki muwe mnafikilia kabla ya kusema
 
Kipindi JPM anakopa tulitoa mawazo kama haya ila tukaambulka matusi kwamba pesa inayokopwa inajenga reli na miundombinu hivyo tuache kuangalia mkopo ila tuangalie faida za huo mkopo kwenye uchumi!!

Cha kushangaza watu wale wale ndio Leo hii mnatambua mikopo sio mizuri?

CCM mpishe tu maana mmejaa unafiki tu
 
Wengi wao wanaongea kwa kufwata mikumbo
 
Bongo tukiongea juu ya kukopa wakenya wasemajee.
 
Ww kwa akili yako unahisi ivyo vyote vinaweza kuendesha nchi iwatengenezee miundombinu ilipe mishahara na hapohapo iwapunguzie gharama za maisha na kulipa Kodi mataki muwe mnafikilia kabla ya kusema
Kwa Nini nchi ya Libya haikuwa na mikopo
 
Aya kwaio kwa akili yako mbovu unataka kusema hawamu hi imepitiliza kiwango Cha mikopo si ndivyo?
Akili yangu mbovu inaniambia kwamba.......

Serikali ya CCM imekosa ubunifu wa jinsi ya kutumia na kunufaika na raslimali za nchi hii kwa maendeleo na ustawi chanya wa Taifa.
Bila kuwategemea wakopeshaji kwa asilimia sabini.(70%).

Unakwenda kukopa kila siku kisha kuja kuwagawia wananchi....

Utaendelea hivyo mpaka lini??
 
Kwani tukikopa hatulipi? Mwaka huu pekee tunakopa Til.8 na kulipa Til.10..Aliyekwambia Nchi inakopa bila mpango ni nani?

Na kwa taarifa yako ,madeni mengi yanayolipwa sasa yalikopwa toka enzi za Mwalimu na awamu zilizopita kutegemeana na muda wa kila deni.
 
Ww tatizo lako umeshindwa kufikilia zaidi umebakia kwenye majungu af mtoto wakiume ushupalia mwenyew
 
Ww kwa akili yako unahisi ivyo vyote vinaweza kuendesha nchi iwatengenezee miundombinu ilipe mishahara na hapohapo iwapunguzie gharama za maisha na kulipa Kodi mataki muwe mnafikilia kabla ya kusema
Unapokwenda kukopa uwe na dira ya kuja kuutumia ule mkopo kwa miradi ambayo baadae itakuwezesha kujikwamua kwenye kukopa na sio kukopa na kuja kujengea shule au matundu ya vyoo.

Wakati hata huduma kwa hao walimu hazijitoshezi.

Wakati hakuna ubunifu wa ajira mpya ili kuendana na kiwango cha uzalishaji wasomi kila mwaka nchini.

Vema kukopa kwa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile kilimo kikubwa cha kisasa na hivyo kupanua ajira za wananchi na kipato cha kitaifa.

Vema kukopa na kuwekeza kwenye miundombinu mikubwa ya uvuvi wa kimkakati katika bahari kuu na hivyo kuliwezesha taifa kiuchumi.

Kuna mambo meengi kuliko.

Na sio kinachoendelea kwa sasa.eti unakwenda kukopa halafu na wewe unakuja kukopesha kina mama wajasiliamali.
Mikopo ambayo haina historia ya urejeshwaji zaidi ya kugeuka hongo za kiuchaguzi.
 
Hizo takwimu ni zako na Mwigulu Nchemba lakini sio za kiuhalisia.
Vema hii ukawaambia wenzio kwenye mikutano ya Shaka!
 
kuilaumu CCM hakukusaidii
Ukirusha jiwe gizani ukasikia ukunga ujue tayari limetua kunako😊
 
Na hakuna nchi ambayo haikopi ndio maana ya kuwa na benk ya dunia ww uwezi kwenda kukoa kule ila serikali inaweza kwenda kukopa
Hatukatai mikopo bali tunakataa kasi ya ukopaji na matumizi ya mikopo husika.
 
Ww tatizo lako umeshindwa kufikilia zaidi umebakia kwenye majungu af mtoto wakiume ushupalia mwenyew
Kweli nimeshindwa "kufikilia" na nimeamua "kufikiri"

Wewe endelea kufikilia tu.
 
Kwaio ww unaona kujenga vyoo mashuleni ni Jambo la kijinga kwaio watoto waendele kupata magonjwa sio
 

Magufuli alijaza wabunge wa CCM huko bungeni kwa kisingizio kuwa ni wazalendo,na hawazuii maendeleo. Waambie wakazue kukopa.
 
Kwaio ww unaona kujenga vyoo mashuleni ni Jambo la kijinga kwaio watoto waendele kupata magonjwa sio
Kwa hiyo nchi kama nchi unaona fahari kuwa na bango la shukurani ya msaada wa kujengewa choo shuleni na kwingineko katika Jamii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…