Mnaoishi Dar, eneo gani unalisikia ila hujawahi kufika?

Maeneo ya wilaya ya Ilala,ambayo nina uhakika wengi hamja wahi fika au hampajaui.
1.Zavala
2.Viwege
3.Mbondole
4.Kigezi
5.Kiyombo
6.Ngobedi/Zingiziwa
7.Nzasa
8.Mkongeni
9.Mwanagati
10.Msongola
11.Mchafukoge...
ZAVALA unaweza ingilia kwa Mbili mbele ya Kinyamwezi (Pugu)
KIGEZI (kwa sina hela), unaingilia Taliani (Chanika) mbele ya Buyuni.
KIYOMBO ni jirani na Nyantila (Kitunda)
VIWEGE ni mbele ya Majohe.
MCHAFUKOGE ni eneo la Kitumbini hadi nyuma kule Mnara wa Saa
 
Mi naijua ya Kimara tu, kumbe Ilala pia kuna Bonyokwa 😳?
BONYOKWA ni Ilala, unaingilia Segerea kama 4km kutoka Segerea. Ni pazuri, hilo jina tu ndio linawatatiza watu na kudhani ni Uswazi. Ila Kimara BONYOKWA wanaiita tu kama mazoea labda kwa sababu ni njia ya kuelekea Kimara ukitoka BONYOKWA
 
Daah sikujua hili kabisa, asante kwa maelezo!
 
Mjuni Lwambo naomba mmwelekeze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…