Mnaojiita Vyama Pinzani Tanzania msipokubali kuacha ubinafsi na kuwatumikia Wananchi kwa Elimu ya Siasa Ikulu mtapasikiga tuu

Mnaojiita Vyama Pinzani Tanzania msipokubali kuacha ubinafsi na kuwatumikia Wananchi kwa Elimu ya Siasa Ikulu mtapasikiga tuu

Wanaojua wameshindwa ni wale wanaojichapishia makaratasi yao ya kura majumbani, kujiwekea tiki wao wenyewe na kuzipeleka katika vituo vya kura chini ya ulinzi wa polisi. Kama unajua utashinda kwa nini uchapishe makaratasi yako mwenyewe nyumbani?
Tofauti sio vyama ni strategies. Viongozi wa wapinzani wa nchi hii wanakula ruzuku na familia zao badala ya kuimarisha vyama.

Kama hamtakua waaminifu na wenye dhamira ya dhati ya kujenga nchi hata mkawachukue NEC ya zambia mtashindwa tuuu

Acheni harakati za mitandaoni kaeni chini muimarishe vyama na mjenge nchi
 
Wanaojua wameshindwa ni wale wanaojichapishia makaratasi yao ya kura majumbani, kujiwekea tiki wao wenyewe na kuzipeleka katika vituo vya kura chini ya ulinzi wa polisi. Kama unajua utashinda kwa nini uchapishe makaratasi yako mwenyewe nyumbani?

Wanaojiita wana nguvu ya umma lakini wanalialia kwa tatizo hilohilo miaka30 bila suluhu tunawaitaje!?

Hivi kina Chief Mkwawa walioweza kumtingisha mzungu aliyekua na technojia ile kipindi kile wangekua wamelegea na kulialia hivi hili taifa lingekuepo kweli

Vitu vingine ni aibu buana
 
Baada ya kuingia vyama vingi,Chama cha mapinduzi kilijimilikisha kwa njia za wizi rasilimali nyingi za nchi hii,mashamba,viwanja vya wazi,viwanja vya michezo,majengo makubwa,nyumba za serikali,shule za serikali n.k lakini pamoja na kujilimbikizia vitu vyote hakuna la maana imefanya.

Wameishia kuuza na kugawana baadhi ya nyumba,zilizo baki zipo katika hali mbaya sana,wameuza mashamba,wameuza viwanja vya wazi,na vilivyobaki vimekosa uendelezaji!! Viwanja vya michezo vimekuwa chakavu na magofu,baadhi ya majengo makubwa walioiba hawajawai kuyaendeleza yamebaki magofu mf:bukoba,Singida,Tabora nk,shule walizoiba wakazigeuza za jumuiya yao ya wazazi karibu zote wameuza kwa watu binafsi,zilizobaki hazifahi kuitwa shule ni kama mabanda ya kufungia nguruwe.

Watu hao hao ndio wanaponda na kuwaita wenzao wa upinzani ni wabinafsi,nchi ina vituko sana hii!!mwizi anapiga ukunga kujifanya yeye ndio kaibiwa!! chama limekwapua rasilimali kibao za nchi linazitumia kuingiza mabilioni ya shilingi,na bado linapokea mabilioni ya ruzuku kila mwezi,lakini hakuna chochote cha maana wanafanya kwenye chama chao kulipa tu watumishi wao ni mtihani.
watumishi wa chama chao hawapelekewi michango kwenye mifuko ya kijamii,wanaishia kulalamika kudhulumiwa haki zao,wanadhulumiana hadi wao kwa wao!!
Hizo akili wanazotumia kuendesha chama chao ndio hizo hizo wanatumia kuendesha nchi,ndio maana hata baada ya miaka zaidi ya sitini toka tupate uhuru hakuna maendeleo ya maana yamepatikana.

Maendeleo machache tunayaona ni mikopo ya benki ya dunia,nchi marafiki,na michango ya wahisani,nchi inadaiwa fedha zinazozidi mpaka rasilmali zote tulizonazo kama nchi, na bado wanaendelea kukopa kama wendawazimu,uku wakikandamiza wananchi makodi na michango ya ajabu.
Wananchi hawana pa kupumulia utafikili wako utumwani,kila kitu ni kodi tu,halafu kuna mijitu inasema CCM ni bora!!!na nchi ni tajiri tutembee kifua mbele!! na watu wanashangilia kabisa!! uku kula yao ya siku haijulikani itatoka wapi?!

Chama kinajivunia kuzalisha vijana ambao ni wamachinga na kuwaacha wakizagaa bila mpangilio na kinasema kina mipango mizuri ya kupeleka nchi mbele!

Ukweli usemwe nchi hii inatafunwa na kansa ambayo ni CCM na magenge yake,bila ccm kutoka madarakani hakuna maendeleo ya maana yatapatikana nchi hii.

Ma-ccm yalivyo na roho mbaya zaidi, hata ajira yanapeana yao kwa yao tu kupitia makada wao,leo ajira za kitaalamu wanapewa watu wasio na ujuzi,sifa wala elimu ya maana ili mradi kama ni kijana uwe mnafiki au una roho mbaya ya kikatili na unauzoefu wa kusema CCM oyee kwa sauti kubwa!!

Kama ni binti uwe na makalio makubwa na usiwe na roho mbaya kuwahudumia kimwili viongozi wenye vitambi wa chama waliojilimbikizia mali ndani ya nchi na uko ughaibuni.

Wewe kama ni mtoto wa maskini utaishia kupata ajira za chini ambazo nazo hakuna kupanda madaraja ya ajira,hakuna nyongeza ya mishahara,na ukistaafu mafao utayachukua kwa mafungu na kwa mbinde sana, utafikili wanakupa kwa hisani yao wakati umevuja jasho.

Yaani hadi mafao kukupa wametunga sheria za kiroho mbaya ili mradi tu mtu ateseke!! CCM sio chama ni mtandao na genge la kimafia la kutafuna nchi.

Huwa nashangaa inakuaje watu wazima timamu wanalalamikia tatizo moja miaka30 bila kupata utatuzi!?
Hii ni wazi kabisa hakuna wanachokiweza zaidi ya kulialia na kuomba huruma ya ccm
 
Sijui unaombea nini? Vita? Akili mbovu sana. Ndio maana mnaajiriwa wa fomu 4 division 3 na 4 tu.
Wanaojiita wana nguvu ya umma lakini wanalialia kwa tatizo hilohilo miaka30 bila suluhu tunawaitaje!?

Hivi kina Chief Mkwawa walioweza kumtingisha mzungu aliyekua na technojia ile kipindi kile wangekua wamelegea na kulialia hivi hili taifa lingekuepo kweli

Vitu vingine ni aibu buana
 
CHADEMA na Vyama vingine vya upinzani wakati umefika sasa mkae chini na kujitafakari!

Tena mjitafakari na kuwa wakweli nafsini mwenu kwamba siasa mnazofanya ni kwa maslahi ya familia zenu huku vyama vyenu vikiwa havina hata misingi imara kwa jamii

Hakuna mtanzania anayekataa au asiyejua umuhimu wa upinzani katika taifa lakini hakuna mtanzania anayeweza kukubali upinzani usio na dira wala maslahi kwa wananchi walio wengi.

Vyama pinzani Tanzania vimekua vyama vya watu wachache ambao ni viongozi wa vyama hivyo. Vyama pinzani havina msingi imara sababu nguvu yao kubwa iko kwa viongozi huku wananchi wakiwa hajui wala kuona maslahi yoyote toka kwa vyama hivyo zaidi ya wao kutafutwa tuu wakati wa kupiga kura.

CCM wanaielewa jamii ya watanzania kwa uzuri sana ndio maana upinzani mnaishia kupumilia mashine kila uchaguzi.

Na kinachozidi kuwapoteza ni kwamba viongozi wote wa vyama vya upinzani sio wakweli kwa vyama vyenu wala kwenu wenyewe. Mmeshindwa kuwa wakweli sababu hamuangalii nyie na vyama vyenu vinawafanyia nini watanzania na nchi yetu kwa ujumla Ila mnaangalia tuu vyama vinawawezeshaje nyie binafsi na familia zenu kuishi maisha mazuri.
Watanzania wameshawaelewa na wanawapuuza sababu ubinafsi wenu umewafanya mjifikirie wenyewe na kusahau kwamba wananchi ndio mtaji wenu

Upinzani unapogeuka kuwa sehemu ya kujipatia rizki lazima malengo ya chama yasahaulike ili kufanikisha kwanza maslahi ya wachache.

Watanzania sio wajinga mnavyofikiria, ushirikiano wapinzani mliofanya na ccm hadi kufanikisha kumuondoa Lowasa kwenye nafasi ya uwaziri mkuu uliwajengea heshma kubwa na imani kwa jamii, na maana halisi ya upinzani ilidhihirika! Ila sasa, usaliti mlioufanya kwa wananchi kumpa huyohuyo jamaa nafasi ya kugombea urais haujasahaulika, hautosahaulika na hamjasamehewa
Wananchi wanajiuliza, kama Lowasa aliweza kuwanunua chadema wakageuka wasaliti kwao si taifa lolote lenye fedha linaweza kuitumia chadema kuwanunua watanzania?

Mkiweza kupata wataalamu wa siasa na uongozi nje ya vyama (wasiokua na maslahi binafsi) watakaoweza kufanya utafiti wa kueleweka jinsi ya kuimarisha chama na kujenga imani kwa wananchi. Mkamwacha huyo mtaalamu awatengenezee mfumo na mbinu za kujenga vyama
Mkamwacha awasimamie nyie viongozi ili kuhakikisha mnatimiza kile anachowaambia kwa muda uliopangwa mtainuka tena na kuwatumikia wananchi

Vinginevyo CCM itaendelea kuwa chama pekee chenye nguvu Tanzania na wapinzani mtaendelea kulalamika kwa tatizo lilelile miaka30

Na sisi kina mama D tutaendelea kusema KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan🙏
Sidhani kama wewe ni mwananchi Wa kawaida wewe ni mnufaika wa utawala Wa ccm.
Masikini kabisa aliyeko vijijini na mijini hawezi kukuelewa. Maisha ni magumu vijijini na mijini usipime.
Kingine in hivi ccm haijawahi kushinda kihalali uchaguzi wowote.
Nyinyi bila policcm hamshindi, na wewe unalijua hili sema unajipendekeza tu.
 
CHADEMA na Vyama vingine vya upinzani wakati umefika sasa mkae chini na kujitafakari!

Tena mjitafakari na kuwa wakweli nafsini mwenu kwamba siasa mnazofanya ni kwa maslahi ya familia zenu huku vyama vyenu vikiwa havina hata misingi imara kwa jamii

Hakuna mtanzania anayekataa au asiyejua umuhimu wa upinzani katika taifa lakini hakuna mtanzania anayeweza kukubali upinzani usio na dira wala maslahi kwa wananchi walio wengi.

Vyama pinzani Tanzania vimekua vyama vya watu wachache ambao ni viongozi wa vyama hivyo. Vyama pinzani havina msingi imara sababu nguvu yao kubwa iko kwa viongozi huku wananchi wakiwa hajui wala kuona maslahi yoyote toka kwa vyama hivyo zaidi ya wao kutafutwa tuu wakati wa kupiga kura.

CCM wanaielewa jamii ya watanzania kwa uzuri sana ndio maana upinzani mnaishia kupumilia mashine kila uchaguzi.

Na kinachozidi kuwapoteza ni kwamba viongozi wote wa vyama vya upinzani sio wakweli kwa vyama vyenu wala kwenu wenyewe. Mmeshindwa kuwa wakweli sababu hamuangalii nyie na vyama vyenu vinawafanyia nini watanzania na nchi yetu kwa ujumla Ila mnaangalia tuu vyama vinawawezeshaje nyie binafsi na familia zenu kuishi maisha mazuri.
Watanzania wameshawaelewa na wanawapuuza sababu ubinafsi wenu umewafanya mjifikirie wenyewe na kusahau kwamba wananchi ndio mtaji wenu

Upinzani unapogeuka kuwa sehemu ya kujipatia rizki lazima malengo ya chama yasahaulike ili kufanikisha kwanza maslahi ya wachache.

Watanzania sio wajinga mnavyofikiria, ushirikiano wapinzani mliofanya na ccm hadi kufanikisha kumuondoa Lowasa kwenye nafasi ya uwaziri mkuu uliwajengea heshma kubwa na imani kwa jamii, na maana halisi ya upinzani ilidhihirika! Ila sasa, usaliti mlioufanya kwa wananchi kumpa huyohuyo jamaa nafasi ya kugombea urais haujasahaulika, hautosahaulika na hamjasamehewa
Wananchi wanajiuliza, kama Lowasa aliweza kuwanunua chadema wakageuka wasaliti kwao si taifa lolote lenye fedha linaweza kuitumia chadema kuwanunua watanzania?

Mkiweza kupata wataalamu wa siasa na uongozi nje ya vyama (wasiokua na maslahi binafsi) watakaoweza kufanya utafiti wa kueleweka jinsi ya kuimarisha chama na kujenga imani kwa wananchi. Mkamwacha huyo mtaalamu awatengenezee mfumo na mbinu za kujenga vyama
Mkamwacha awasimamie nyie viongozi ili kuhakikisha mnatimiza kile anachowaambia kwa muda uliopangwa mtainuka tena na kuwatumikia wananchi

Vinginevyo CCM itaendelea kuwa chama pekee chenye nguvu Tanzania na wapinzani mtaendelea kulalamika kwa tatizo lilelile miaka30

Na sisi kina mama D tutaendelea kusema KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan🙏
Nadhani wapinzani ni wabinafsi na wanafiki sana ndio maana ikulu watapasikia tu.
Maana ni miaka 60 ya uhuru lakini bado hakuna maji Safi na salama, hakuna elimu wala huduma bora za afya.
Naona miaka yote kujisifu kufanya maendeleo lakini hakuna uchaguzi huru na haki zaidi ya kujaza makada wa chama kwenye nafasi mbalimbali za uteuzi ie maRC, maDC, maDED, mwenyekiti wa time pamoja na watumishi wengine wa time ya uchaguzi
Kweli upinzani ikulu wataisikia tuu maana bajeti ya serikali 80% ni kwa matumizi ya kawaida na 20% ni matumizi ya maendeleo yaani hela nyingi zinaenda kununua viete,kujaza mafuta kwenye misafara ya mwenge au kuzindua miradi ambayo sio endelevu
Kweli wapinzani ikulu wataisikia maana kundi kubwa la vijana hawana uhakika wa maisha kiuchumi na ajira huku waliambiwa wajiajiri bila sera na sheria zinazorahisisha na kuwezesha miundombinu ya kujiajiri na fursa za ajira kwa usawa
Kweli wapinzani ikulu watapasikia maana bunge linapitisha sheria za mapato na Kodi na tozo kandamizi bila kudhibiti matumizi ya serikali
 
Vyama vya upinzani vyote vimejikita kudai chaka la katiba ambalo hata likiwekwa bado ikulu wataisikia tuu nahisi hata miaka 30 ijayo,, Hakuna siku chama chochote kimezungumzia swala la maisha ya mtanzania na kero zao za maisha bali kutudanganya tu ati wananchi wanadai katiba mpya na wapi alikutana nao wakamtuma hawatuonyeshi.

Katiba mpya takwa na hitaji la hao viongozi wa vyama vya upinzani kwani wanajua labda kwa kupitia chaka la katiba hata tume ya uchaguzi itakuja kuwa kichochoro cha wao kupitia kuelekea magogoni

Hawa watu ni hatari lkn kizuri watanzania wamewajua vizuri,,, Nenda kijijini uliza watu laki moja kama kuna mtu anaijua katiba hakuna sasa upinzani wametumwa na nani?

Wametumwa na tamaa na ndoto zao,,, Msomeni mzee Warioba alienguliwaje kwenye kinyang'anyiro cha urais huko nyuma muone ilikuwaje ili muone kwa nini anaongea kuhusu katiba mpya mpuuzeeni ana lake jambo!!!!
Kwanini mnakataa katiba mpya, kwanini msiache watu wajadili na kutoa elimu ya uraia na katiba badala ya kutumia nguvu ya polisi kuzuia watu wasijadili
 
Jipe moyo tuu ndugu yangu sababu vyama pinzani vya nchi yako havina vinachofanya mfanano na huko ulikotaja

Acheni kumsingizia Mungu uzembe wenu
Lauryn Hill ni critical thinker
Hana akili mbovu kama zako
Nakuamrisha kuondoa picha yake na uweke ya shonza au dorithy gwajima
 
Lauryn Hill ni critical thinker
Hana akili mbovu kama zako
Nakuamrisha kuondoa picha yake na uweke ya shonza au dorithy gwajima

Hiyo kritkothinkin ya Lauryn Hill unaijua wewe

Kwendraaas
 
Fisi anamfundisha Swala jinsi gani ya kuepuka kuliwa na mbwa mwitu.
Only in Africa.
 
Unafikiri upinzani wa zambia walikua wachumia tumbo wa kutafuna ruzuku kama nyie!??
Endeleeni kujipa moyo ila msipotushawishi wananchi kura mtazisikia na maandamano mtafanya na wake na watoto zenu
Yaani wewe hata hujui kinachoendele. CMM wanapata ruzuku ya Serikali. CHADEMA wanapata michango ya wananchi.
Halafu helasio Kila kitu mje muelewage Hilo, Ni muhimu sana.
 
Yaani wewe hata hujui kinachoendele. CMM wanapata ruzuku ya Serikali. CHADEMA wanapata michango ya wananchi.
Halafu helasio Kila kitu mje muelewage Hilo, Ni muhimu sana.

Wewe ndio huelewi wala kujielewa kabisaaa
Sasa CMM ndio ndio nini🙄🙄🙄

Kwa hiyo Mbowe na Tundu walikuongopea kuwa hawapati ruzuku!? Pole kwa kutapeliwa
 
Wewe ndio huelewi wala kujielewa kabisaaa
Sasa CMM ndio ndio nini🙄🙄🙄

Kwa hiyo Mbowe na Tundu walikuongopea kuwa hawapati ruzuku!? Pole kwa kutapeliwa
Mnawanyayasa sana na hivyo viruzuku wamewaachia ili mchukue fungu lao mpate za kukipana posho wao uao wataipata kwa wananchi wanaowaunga mkono.
 
Watanzania sio wajinga mnavyofikiria, ushirikiano wapinzani mliofanya na ccm hadi kufanikisha kumuondoa Lowasa kwenye nafasi ya uwaziri mkuu uliwajengea heshma kubwa na imani kwa jamii, na maana halisi ya upinzani ilidhihirika! Ila sasa, usaliti mlioufanya kwa wananchi kumpa huyohuyo jamaa nafasi ya kugombea urais haujasahaulika, hautosahaulika na hamjasamehewa
Wananchi wanajiuliza, kama Lowasa aliweza kuwanunua chadema wakageuka wasaliti kwao si taifa lolote lenye fedha linaweza kuitumia chadema kuwanunua watanzania?
Hiki ndicho kilinifanya mimi niache kuiunga mkono chadema. Jamaa walitusaliti sana kwa pesa kiduchu tu. Hawaaminiki hawa, hakuna anayeweza kuwaamini vigeugeu.
Mama D umesema vizuri, chadema ya sasa hivi ni kagenge ka wahuni fulani tu wenye interest zao binafsi na wanakitumia chama ili kufanikisha hayo malengo yao binafsi. Hakuna chama hapo, ni utapeli mtupu.
 
Hiki ndicho kilinifanya mimi niache kuiunga mkono chadema. Jamaa walitusaliti sana kwaa pesa kiduchu tu. Hawaaminiki hawa, hakuna anayeweza kuwaamini vigeugeu.
Mama D umesema vizuri, chadema ya sasa hivi ni kagenge ka wahuni fulani tu wenye interest zao binafsi na wanakitumia chama ili kufanikisha hayo malengo yao binafsi. Hakuna chama hapo, ni utapeli mtupu.
Sawa usiiamini. Je unaamini kuwa tunaihitaji tume huru ya uchaguzi nakatiba mpya?
 
Back
Top Bottom