Mnaojiweza au mliowahi kujiweza kiuchumi mkiwa chini ya miaka 30, nje ya ajira, utajiri wa familia, n.k mliwezaje?

Kama ni haya, kuyatimiza ndani ya miaka 30 ni ngumu kidogo hasa kama umeenda shule kwa kufuata ule utaratibu wa kawaida wa kitanzania but kama uliishia darasa la saba au kidato cha nne kisha ukapata bahati ya kupata njia ya kukuingizia pesa mapema unaweza kufikia huko.
 
Sijaajiriwa, sijasoma na wala sitoki ushuani.
Naishi maisha fulani hivi ya ki khoi khoi.
Hata laptop sijui kuitumia.
Ili kijana afike mbali kiuchumi anatakiwa kuwa na msichana mmoja anayesapoti vibiashara vyake au shughuli zake za kiuchumi (sio lazima ampe hela )

Tofauti na hapo kijana atakuwa ni mfuko uliyetoboka, na ataishi maisha ya hovyo hadi uzeeni.
 
experience,...watu wengi ninaowafahamu waliofanikiwa wakiwa kwenye 20's basi walianza hustle wakiwa kwenye 10's..... wengi ni school dropout
 
Mkuu sema kuna muda ukiwaza ukitoboa ukiwa na 60 au 70 sidhani hata hizo pesa unaweza kuzi-enjoy maana hapo nguvu zimeshakwisha ila mapambano yanaendelea hata kama uwanja umeinama na dakika zinakimbia ni get rich or die trying πŸ’ͺ
 
Mkuu sema kuna muda ukiwaza ukitoboa ukiwa na 60 au 70 sidhani hata hizo pesa unaweza kuzi-enjoy maana hapo nguvu zimeshakwisha ila mapambano yanaendelea hata kama uwanja umeinama na dakika zinakimbia ni get rich or die trying πŸ’ͺ
Kusema la haki mimi nimevuka 60 na bado nina nguvu na afya
Hapa wazungu wako tofauti na unachosema
Wanafanya kazi miaka zaidi ya 40 au 50 na wanapostaafu wanakuwa na malimbikizo mengi ya miaka waliyofanya kazi

Kwa mfano anastaafu kazi akiwa na 67 ana hela alizoweka private pension na zimekaa miaka 50 huku muajiri nae kila mwezi anakuwekea kiasi (kwa amri ya serikali)

Mwisho wa siku wakiwa na miaka 70 au zaidi wananunua nyumba kubwa na shamba na wanaendelea kula raha mpaka wanakufa
Kwa hiyo mkuu hata wazee wanafurahia marunda waliyotachuma bila kujali nani atabakia na hiyo nyumba siku wakifa

Wengi wao hapa UK wananunua manyumba Spain, Italy, France na hali ya hewa ni joto kuliko hapa


Yaani ukifika 60 una mingine 30 ya kula, ila ukijaaliwa kufika huko
Huku wanaishi vizuri bila kutegemea mtu kama walifanya kazi miaka

Sasa kwa huko nyumbani mambo ni tofauti mara hela za pension zimeelekezwa kwenye miradi
Wataacha kufa na pressure
 
Wenzetu mliwezaje wezaje, wengine tumejipata kwenye 30 na kitu, hali za huko nyuma zilikuwa mbaya sana
Mafanikio ni kitu kiko ndan ya mtu tangu kuzaliwa sio waliwezaje ni kuwa hata aliyefanikiwa hawez kuzuia mwili wake kuja na mipango endelevu. Angalia sana wanao tangu wakiwa wadogo utaona utofauti na wekeza kwa yule mwenye tofauti zaid maana ndie mbeba maono ya familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…