Mkuu sema kuna muda ukiwaza ukitoboa ukiwa na 60 au 70 sidhani hata hizo pesa unaweza kuzi-enjoy maana hapo nguvu zimeshakwisha ila mapambano yanaendelea hata kama uwanja umeinama na dakika zinakimbia ni get rich or die trying 💪
Kusema la haki mimi nimevuka 60 na bado nina nguvu na afya
Hapa wazungu wako tofauti na unachosema
Wanafanya kazi miaka zaidi ya 40 au 50 na wanapostaafu wanakuwa na malimbikizo mengi ya miaka waliyofanya kazi
Kwa mfano anastaafu kazi akiwa na 67 ana hela alizoweka private pension na zimekaa miaka 50 huku muajiri nae kila mwezi anakuwekea kiasi (kwa amri ya serikali)
Mwisho wa siku wakiwa na miaka 70 au zaidi wananunua nyumba kubwa na shamba na wanaendelea kula raha mpaka wanakufa
Kwa hiyo mkuu hata wazee wanafurahia marunda waliyotachuma bila kujali nani atabakia na hiyo nyumba siku wakifa
Wengi wao hapa UK wananunua manyumba Spain, Italy, France na hali ya hewa ni joto kuliko hapa
Yaani ukifika 60 una mingine 30 ya kula, ila ukijaaliwa kufika huko
Huku wanaishi vizuri bila kutegemea mtu kama walifanya kazi miaka
Sasa kwa huko nyumbani mambo ni tofauti mara hela za pension zimeelekezwa kwenye miradi
Wataacha kufa na pressure