Mnaojua Mpira nielewesheni, kwa nini Balua anapangwa kulia?

Mnaojua Mpira nielewesheni, kwa nini Balua anapangwa kulia?

Enzi zetu za ligi za mchangani mtu anayetumia mguu wa kushoto huwa ama acheze namba tatu,sita na kumi na Moja (wahenga watanielewa)

Nashangaa Balua anatumia mguu wa kushoto lakini anapangwa namba saba.

Au ndiyo Mpira wa kisasa?
Siku hizi wanaita "Inverted winger", mchezaji anacheza upande tofauti na ule uliozoeleka. Ni kama Percy Tau. Kuna faida zake kuwa na mchezaji wa namna hii.

Nje ya mada, hivi kwa nini Zimbwe katikati ya mchezo amekuwa anabadili position, kuna wakati anaenda kucheza beki wa kati, kiungo au beki mmoja wa kati anahamia pembeni. Leo alihamia kulia, Kapombe akaenda kucheza middle. Hizi ni mbinu za mchezo za mwalimu au ndiyo usenior wenyewe?
 
Mjomba aulizaye anataka kujua... Sasa wewe GT ukamiliki mbingu.!? Vitu vingine punguza ujuaji....
Ndio nyie wajinga .... Kwahiyo Dunia hii ya mpira mchezaji kucheza kushoto wakati anatumia kulia ni ajabu?, mbona haulizi kibu kucheza kushoto au karabaka kucheza kulia!!. Punguzeni utoto k6jaza Seva za jf.
 
Uneambiwa punguza ujuaji...

Ungekuwa Mwalimu ungejua kuwa kuna kitu kinaitwa mbinu ya kutunga swali kwa lengo Mahsusi.

Wewe GT Kaa pembeni wakati mbumbumbu tunaendelea kujuzana.
 
Modern football imekuja kubadilisha mifumo mingi ambayo zamani ilionekana kama utamaduni unaofanyika kwa mazoea.

Asilimia kubwa ya mawinga wa kisasa wana uwezo wa kucheza pande zote pamoja na ule upande ambao upo opposite na mguu wake ambao ni favorite.
 
Enzi zetu za ligi za mchangani mtu anayetumia mguu wa kushoto huwa ama acheze namba tatu,sita na kumi na Moja (wahenga watanielewa)

Nashangaa Balua anatumia mguu wa kushoto lakini anapangwa namba saba.

Au ndiyo Mpira wa kisasa?

Ndivyo wanavyotumika siku hizi, right handed to left vs left handed to right.

Ni rahisi kukatisha uwanja kuja ndani ya uwanja badala ya kwenda pembeni mfano: wa mguu wa kushoto(kwani hawezi kwenda pembeni ambako hatumii vyema mguu wa kulia).

Hii huongeza nafasi ya yeye kupiga shuti moja kwa moja(with high accuracy vs high precision) golini badala ya krosi kwani anakuwa analiangalia goli moja kwa moja.
 
Hata kwenye Derby kama utakumbuka Pacome alicheza winga ya kulia lakini mambo yalipomuendea vibaya ikabidi ashuke chini kushoto akutane na Kapombe ambaye siku hiyo hakuwa na mchezo mzuri.

Na kuanzia hapo ndio akawa ana ng'aa kwenye mchezo tofauti na ambavyo alikuwa kulia.
 
Ndivyo wanavyotumika siku hizi, right handed to left vs left handed to right.

Ni rahisi kukatisha uwanja kuja ndani ya uwanja badala ya kwenda pembeni mfano: wa mguu wa kushoto(kwani hawezi kwenda pembeni ambako hatumii vyema mguu wa kulia).

Hii huongeza nafasi ya yeye kupiga shuti moja kwa moja golini badala ya krosi kwani anakuwa analiangalia goli moja kwa moja.

Mtu wa mpira kabisa...
 
Ndivyo wanavyotumika siku hizi, right handed to left vs left handed to right.

Ni rahisi kukatisha uwanja kuja ndani ya uwanja badala ya kwenda pembeni mfano: wa mguu wa kushoto(kwani hawezi kwenda pembeni ambako hatumii vyema mguu wa kulia).

Hii huongeza nafasi ya yeye kupiga shuti moja kwa moja(with high accuracy vs high precision) golini badala ya krosi kwani anakuwa analiangalia goli moja kwa moja.
Hata mim huwa nafikiri hivyo,lakini kwa simba huenda kocha hajamuelekeza vizuri balua,kwasabab yeye badala ya kuuweka mpira kwenye upande wa mguu wake wenye nguvu akalazimisha kukimbia mbele mpira ukakaa kulia akashindwa kuukontrol beki akamnyanganya kwa wepesi,
Inabid kwa namna yoyote balua anapocheza upande wa kulia mpira auweke kushoto kwake
 
lengo ni kushambulia kwa kuingia ndani na kuliface lango na kufunga goli na siyo kutanua uwanja na kupiga krosi isiyokuwa na uhakika inafika kwa nani.

haya mabadiliko yamekuja baada ya mifumo kubadilika badilika kutoka 4-4-2 iliyokuwa imezoeleka hapo awali.

zamani no. 7 na 11 tuliwaita mawinga, ila kwa mifumo tofauti tofauti inayotumika sasa mfano ya 4-3-3, 4-2-3-1, na 3-4-2-1 nk.. tunawaita midifilders, inayojumuisha viungo wakabaji, viungo wachezeshaji na viungo washambuliaji.

NB: beki no. 2 na 3 wanaweza wakatumika mbadala kufanya majukumu ya mawinga(right back & left back).

Bila shaka utakuwa umenielewa.
 
Modern football imekuja kubadilisha mifumo mingi ambayo zamani ilionekana kama utamaduni unaofanyika kwa mazoea.

Asilimia kubwa ya mawinga wa kisasa wana uwezo wa kucheza pande zote pamoja na ule upande ambao upo opposite na mguu wake ambao ni favorite.
Wanaita othodox winger ambapo ni Bora zaidi kukreat chances na caving
 
Enzi zetu za ligi za mchangani mtu anayetumia mguu wa kushoto huwa ama acheze namba tatu,sita na kumi na Moja (wahenga watanielewa)

Nashangaa Balua anatumia mguu wa kushoto lakini anapangwa namba saba.

Au ndiyo Mpira wa kisasa?
Wanaitwa "inverted wingers".
Nikupe faida au mfano mmoja simple tu.
Ahoua alifunga kwa mguu wa kulia lakini akiwa ametokea kushoto. Sasa Ahoua angetaka kutumia mguu wa kushoto pale sababu yuko kushoto angeishia kupiga cross.

Pia winger anaetumia mguu wa kulia tuseme akikaa kushoto ambako anakutana na beki wa kulia anaetumia mguu wa kulia ni rahisi zaidi kumpita.

Yaani winger anaetumia mguu wa kulia akikabiliana na beki anaetumia mguu wa kulia ni kama miguu inapishana hivi so rahisi kumsumbua.

Nimalizie tu Edibily Jonas Lunyamila aliwika sana enzi zake lakini hakua mfungaji ki hivyo. Sababu alikua ana uwezo wa mbio na chenga ila hakua akiingia sana kati hivyo mwishowe alikua akipiga kross wanafunga wengine.

Sasa inverted Wingers hawako hivi.
 
Back
Top Bottom