Mnaojua Mpira nielewesheni, kwa nini Balua anapangwa kulia?

Mnaojua Mpira nielewesheni, kwa nini Balua anapangwa kulia?

Kwa kuongezea tu, Yanga haijawahi kuwa na inverted winger, hili somo bado jipya kwao
 
Amna bna ukiangalia ile alipoenda kulia Kama sikosei ilikuwa ni wakati Simba walipata Kona kama sio faulo

Kwenye matukio hayo zimbwe huwa anabaki nyuma kama beki wa mwisho na mabeki wanaenda kucheza vichwa
Sema kilichofanya asurudi haraka ni mpira ulienda alipokuwa kwa hyo ikabidi abaki kule kwanza wamalizane hadi wachezaji wengine warudi kwenye nafasi zao
Hiyo ya nje ya mada: Mechi ya jana Simba walikuwa wanacheza walinzi watatu nyuma. Hivyo full back right na left wanakuwa na option ya kuongeza nguvu sehemu yoyote yenye mapungufu. Ingawa ni formation ya hatari pale ambapo timu poinzani ina wachezaji makini na wenye uwezo hasa kufanya mashambulizi ya kustukiza (counter attack). Rejea mechi ya fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Azam FC na Yanga.
Lakini haya matukio huwa anafanya robo ya mwisho wa mchezo hasa timu ikiwa inaongoza. Siongelei wakati wa kona au faulo. Msimu huu ameshafanya hivyo game mbili, msimu uliopita nakumbuka walau game moja kumshuhudia akifanya hivyo.
 
Labda kuna sababu nyingine mkuu mm sijui sana mpira ila nilijaribu kufikiria kulingana na tukio likivokuwa
 
Mimi nafikiri mchezaji akicheza opposite na position ya mguu wake, advantage alinayo ni kwamba anauwezo mkubwa wa kufanya curving ya mpira kwenda golini katika angle zote za goli kwa usahihi zaid tena kwa energy kubwa pia.
 
Enzi zetu za ligi za mchangani mtu anayetumia mguu wa kushoto huwa ama acheze namba tatu,sita na kumi na Moja (wahenga watanielewa)

Nashangaa Balua anatumia mguu wa kushoto lakini anapangwa namba saba.

Au ndiyo Mpira wa kisasa?
Unamjua Mo Salah? Anapangwa upande upi?
 
Wewe inaonekana ni mtu wa mpira lakini nashangaa hili swali kuliuliza leo wakati haya mabadiliko yameanza miaka mingi iliyopita.
Hapa ni sehemu ya kujuzana... Kudhani unachojua na wengine wanajua, ni kosa.

Huoni watu wametoa maoni mazuri tofauti tofauti?
 
Enzi zetu za ligi za mchangani mtu anayetumia mguu wa kushoto huwa ama acheze namba tatu,sita na kumi na Moja (wahenga watanielewa)

Nashangaa Balua anatumia mguu wa kushoto lakini anapangwa namba saba.

Au ndiyo Mpira wa kisasa?

Kwa nini Mahrez alikuwa anapangwa 7 na Pep, kwa nini Robben alikuwa anakula mbavu ya kulia akiwa Chelsea, Bayern nk...

Mpira wa zamani mawinga walikuwa wanatumika kumimina majalo tu, nfio maana walipangwa pande ambazo ni za miguu yao natural...

Lakini kwenye modern football, mawinga wanahesabika kama washambuliaji wanaoshambulia toka pembeni na kuingia kati, winga anayetumia mguu wa kushoto akiwa upande wa kulia, akiingia kati na mpira inamuwia wepesi wa kushoot kwa kutumia upande wa ndani wa mguu...
 
Lakini nadhani kwa Balua hana ufanisi unaotarajiwa.
 
Back
Top Bottom