Babarazack
Senior Member
- Sep 9, 2015
- 135
- 162
Habari za muda huu wanagenzi,leo nimeona nianzishe uzi huu ili niweze kuwashirikisha na nyinyi katika hili ambalo limekuwa likiniumizakichwa kwa kiasi kikubwa kulitafakari kwa muda mrefu bila kulipatia majibu.hivyo kupitia jukwaa hili ni Imani yangu kuwa ninaweza kupata suluhisho juu ya swala hili.
Kama kichwa cha habari hii kinavyoeleza hapo juu,kuna mkanganyiko kidogo katika sharia ya ndoa.japo si mtaalamu wa masuala ya sheria lakini nilijifunza kitu kidogo na kugundua udhaifu huu kutokana na kisa kilichomtokea rafiki yangu ambaye aliishia kupigwa faini baada ya kukutwa na hatia ya kumlaghai mke wa mtu na kuishi nae kinyumba (kama mke na mume)
Kwa kifupi ilikua hivi,siku moja nikiwa mjini katika mitkasi zangu ghafla nilikutana na rafiki yangu ambaye tulipotezana kwa muda mrefu sana baada ya salamu ikabidi tupate muda wa kukaa kuzungumza na kupiga stori mbili tatu kukumbushana yaliyopita na jinsi maisha yanavyokwenda kwa sasa,
Tulichukuana mpaka katika mgahawa Fulani ulio kando ya barabara tukaketi huku kila mmoja wetu akiwa na furaha ya kukutana tena baada ya kupotezana muda mrefu.tuliagiza vinywaji na mazungumzo yakaendelea tuliulizana mambo kadhaa kuhusu mwendelezo wa maisha kwa kipindi tulichopotezana,masomo,kazi,mahusiano na masuala mengine ya maendeleo katika maisha.
Baada ya mimi kumweleza kuwa nimeshapata kazi,nimejenga na nina mke na watoto wawili.alinipongeza sana kwa hatua niliyofikia na kunisihi nisibweteke nizidi kupambana na niwe makini sana na maisha maana muda wowote yanaweza kugeuka.maneno hayo ya rafiki yangu kunitaka niwe makini katika maisha yalinifanya niwe kimya kidigo nikitafakari.mara rafiki yangu akaendelea,kwa kweli tunapaswa kuwa makini sana maana kupoteza matumaini ni rahisi sana.hapo hapo nikamuuliza swali,kwanini?
Akasema brother mimi nimepata matatizo makubwa sana katika masuala ya wanawake na mpaka sasa sina hamu tena ya kuoa, miaka kadhaa nyuma nilipata mwanamke mzuri wa kuoa lakini yeye mwenzangu alikua tayari ameshatoka kutumikia ndoa moja,waliachana na mume wake baada ya kumfumania na mwanamke mwingine,hapo ndipo migogoro ya ndoa ikaanza,mwanamke alidai talaka kwa mume wake usiku na mchana.mume alihangaika kuinusuru ndoa yake lakini haikuwa kazi rahisi,aliomba msamaha akashindwa,akaomba msaada kwa mshenga ikashindikana,akaomba msaada kwa wazazi wa pande zote mbili lakini bado ikawa ngumu kubadili msimamo wa mwanamke yule.ndugu,jama na marafiki nao walijaribu wakashindwa.
Mwisho wote walikata shauri na kumtaka mume atoe talaka,basi kwa shingo upande yule bwana akalazimika kutoa talaka kwa mke ambaye bado moyo wake ulikua unampenda kwa dhati japo shetani aliingilia kati na kukatisha mapenzi hayo.
Basi jamaa alitoa talaka tatu (kwa wale waislamu watakua wanajua kuwa talaka tatu maana yake huwezi kurudia tena mke ni mpaka aolewe kisha aachwe kwa talaka tatu tena ) kwa hasira na kumtaka mwanamke yule asichukue chochote katika mali walizochuma,mwanamke kwa kipindi kile kwa kuwa shida yake kubwa ilikuwa ni kupewa talaka yake hakujali sana kuhusu mali alizochuma na mumewe.
Siku zikapita mwanake maisha ya kujihudumia yakawa magumu ndugu nao wakawa kikwazo kwake kutokana na masimango kumsema kwanini alishikilia uamuzi wa kudai talaka wakati alishaonywa kuhusu ugumu wa maishu lakini akaona kawaida.
Wakati anaedelea kupambana na shida za maisha dada yule ndipo akakutana na rafiki yangu nae akiwa na kiu ya kupata mwanamke wa kumuweka nda wafanye maisha,basi ukawa mwanzo wa mahusiano kwa wawili hao,mapenzi yakazaa uchumba rafiki yangu katuma mshenga,basi kama unavyojua tena kwa jamii zetu za kizaramo ukibisha hodi unakaribishwa hadi chumbani,rafiki yangu akawa ameshatambulika kwa wazazi akawa anatembelewa na mchumba wake siku moja moja mpaka akaamua aweke kambi kabisa hata kabla ya ndoa
Kumbe yule x-mume bado moyo wake haujatoka kwa mwanamke yule ingawa tayari ameshamuacha basi nae akaanza kujirudisha kimya kimya huku mwanamke akiwa bado amebaki na msimamo wake ule ule na kumkumbusha kuwa ametoa taraka tatu na hata hivyo yeye tayari ana mchumba mwingine (ambaye ndo rafiki yangu sasa) x-mume kusikia ivo akazidi kuchanganyikiwa aliondoka akiwa na huzuni kubwa moyoni mwake
MAAMUZI YAKE
Yule x-mume alitafakari akaona njia sahihi kwake ni kwenda mahakamani kufungua kesi ya kua amedhulumiwa mke na mshtakiwa namba moja akiwa ni rafiki yangu kosa lake ni kumlaghai mke wa mtu na kuishi nae kinyumba. Baada ya miezi na siku kadhaa za kusikilizwa kwa shauri hili katika mahakama ya mwanzo,hatimae rafikiki yangu alitiwa hatiani kwa kosa hilo kwa sababu zifuatazo
1.Mahakama ilijiridhisha kuwa ni kweli amemlaghai kwa sababu ilithibitika kuwa alikuwa anaishi nae katika nyumba yake na wana mahusiano ya kimapenzi.
2.Hakuwa na ushahidi unaotambulika kisheria wa kuvunjwa kwa ndoa ya mchumba wake na x-mume wake,ambapo yeye alionyesha zile talaka tatu ambazo x-mume alizionyesha lakina mahakama haikuzitambua kama uthubitisho wa kuvunjwa kwa ndoa hiyo badala yake alitakiwa kuonyesha HATI YA TALAKA ambayo hutolewa kisheria katika mahakama.
3.Hakukuwa na shauri lolote liliwahi kufunguliwa na mchumba wake kudai talaka katika mahakama yoyote dhidi ya x-mume (hali iliyopelekea aonekane bado ni mke halali kisheria wa yule x-mume)
4.Hakukuwa na mchanganuo wa mgawanyo wa mali.iliwezekana vipi kuwa ameachana na mume wake bila ya kuwa wamegawana mali walizochuma na mume huyo wakati wameishi miaka kadhaa.
Basi kwa sabababu hizo mahakama iliamuru mwanamke arudi kwa mumewe na endapo anataka kuachwa afuate utaratibu wa kisheria.
Na rafiki ya yangu nae alipigwa faini kwa makosa yake hayo.
Sasa mimi nikabaki na swali moja ambalo ni kwanini serikali itambue ndoa za kimila na kidini lakini isitambue talaka zinazotolewa kimila na kidini?
Au hakimu alihukumu kimakosa nimshauri rafiki yangu akate rufani? Mimi sio mjuzi wa masuala ya sharia nahitaji ushauri wenu wananzengo nimshauri vipi rafiki yangu?
Karibuni tujadili.
ASANTENI.