Mnaokaa Uswahilini (Wilaya ya Temeke) Mungu awafanyie wepesi ndugu zangu. Jana machozi yalinitoka

Temeke ni balaa mkuu..
 
Mnawatelekeza upande mkiwakuta upande mwingine mnawahurumia, mnazalisha wanawake upande mmoja ukiwakuta ukiwakuta upande wa pili unawahurumia, watoto na wanawake tabu zao nyingi zinatokana na wanaume Si LAZIMA ukubali ukweli uko wazi.
 
umetoka ilala na unawacheka wa temeka ndugu? mbona mpo sawa tu kiuswahiliniswahilini? pia, shukuru hata aliwapa 500, kuna wamama wengine hata hapo ilala hawana hiyo 500. wakati tunakua, jirani yetu alikuwa anatuma watoto kuja kuhemea kwetu, na tulikuwa tunawaita tunakula nao chakula cha mchana fresh tu, Mzee alinifundisha jambo kubwa sana kwenye utoaji. yaani ikifika mchana utakuta hao wamekuja kucheza, na baba hataki nile peke yangu natakiwa niwakaribishe tule wote. hao ndio walikua wakawa mafariki zangu hadi ukubwani huku, wengine wamefanikiwa tu ila ile bond ipo hadi leo tunajiona familia.
 
Sasa mbona wewe wa Ilala na huyo wa Temeke Hali zenu zinafanana?
Kwa sababu hao watoto kama wangekuwa wako hata wewe pia usingeweza kuwalisha mlo wa mchana na hiyo buku 2 yako
 
Sasa mbona wewe wa Ilala na huyo wa Temeke Hali zenu zinafanana?
Kwa sababu hao watoto kama wangekuwa wako hata wewe pia usingeweza kuwalisha mlo wa mchana na hiyo buku 2 yako
Ningesema niliwasaidia wale watoto, mngenirushia tena wale "KWA HIYO NDIO UMEKUJA KIJITANGAZA JF ILI UONEKANE UNA ROHO NZURI??"
 
umetoka ilala na unawacheka wa temeka ndugu? mbona mpo sawa tu kiuswahiliniswahilini?
Ningesema niliwasaidia wale watoto, mngenirushia tena wale "KWA HIYO NDIO UMEKUJA KIJITANGAZA JF ILI UONEKANE UNA ROHO NZURI??"
 
Hongera sana kwa kuwa na mzazi mwema..
 
Nyote ni walewale hata kwako mnashindia uji! Ulishindwa nini hata kumpigia mamsapu akutumie hata buku 5 ukawanunulie kilo mbili za mchele?
Ningesema niliwasaidia wale watoto, mngenirushia tena wale "KWA HIYO NDIO UMEKUJA KIJITANGAZA JF ILI UONEKANE UNA ROHO NZURI??"
 
Picha linaanza njia ya kwenda kivule tu............ kutokea Ukonga ni shida.

Ukisema upitie Msongola kutokea Chamazi Mbande nayo hovyo.

Ukikatiza pale kati kwa kufuata Bomba la songas wamejaa waganga wa kienyeji.

Kivule unayo jivunia imeizidi nini kata ya Chamazi ambayo ipo wilaya ya Temeke?

Unapojibu ukumbuke Mimi mwenyewe ni mtoto wa Wailes na huko kivule na Msongola Kuna vibanfmda vyangu
 
Nimelia sana kujiita wa ilala wakati unamiliki buku benga tu.......ila umaskini wa wananchi hasa wa kawaida unazidi kuwa wa kutisha huku watu fulani wanaojiita wanasihasa wakizidi kuwa na ukwasi wa kufuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…