Kuna kitu nimeona nikieleze kuhusu Roman Catholic church baada ya kuona Kuna watu hapa nchini Tanzania wanatukana, wanashambulia watumishi wakatoliki, wanakejeli katoliki (TEC) n.k kwakutumiwa na wanasiasa wasio na akili pia walioishiwa hoja na wasiosoma historia kutoka CCM pia watanzania wengine kwa misingi ya itikadi za kidini.
Hiki kitu nawakumbusha kwa kutowatisha bali uhalisia wa jambo lenyewe yani Roman Catholic church ( Roman Empire au Byzantine Empire).
Nitaeleza kwa kifupi ili nieleweke,
Roman imekuwepo kabla ya ujio wa Yesu Kristo kabla ya ujio wa mtume Mohammad (SAW) na imeendelea kuwepo hadi Sasa katika mifumo tofauti ya Kisiasa, Kiuchumi, Kidini, Teknolojia n.k
Hao ndio walioanzisha Kalenda unayotumia Leo yenye miezi kumi na mbili, mifumo ya Sheria, uhandisi, mipango miji, utawala, mbinu za kivita n.k hao watu wanaijua historia ya Dunia, Siri za Dunia n.k kuliko kawaida.
Hao ndio wanaitawala Dunia kwa upande usioonekana kwa kuwatumia UK na USA kwa sasa, pia hao watu wako hadi mlangoni kwako na wana taarifa za mambo Yako unayofanya kila siku.
Hao watu wanavyuo vikuu, hospital, orphanage center, shule n.k Dunia nzima.
Msidanganywe na hao wanasiasa wa CCM wasio na akili kwamba mnaweza kuwakejeli, kutukana au kushambulia Roman Catholic church na Kisha kuwavuruga, katika hilo mnajisumbua sababu hao watu wana intelejesia kubwa kuliko unavyojua wewe, wana wasomi wa kiwango Cha juu duniani, wanauchumi mkubwa zaidi kuliko hata nchi yetu hii mnayofikiri ni tajiri.
Mnatakiwa mjue kwamba kiongozi wao mkuu yana Papa (Pope) ndio kiongozi pekee wa dini anayeingia United Nations (UN) General Assembly na kuhutubia.
Baadhi ya mapambano ya kihistoria waliyofanya ni pamoja na.
1. Kuvuruga Ukristo halisi na kuleta ukristo feki uliopo Sasa kutoka kikao Chao cha Nicea
(Nicea Conference)
2. Vita ya msalaba (Crusade War) kuzuia ueneaji wa uislamu duniani na wakafanikiwa Kisha kuvuruga uislamu halisi kwa kuleta uislamu feki uliopo sasa.
Kuendelea kuvuruga uislamu na ukristo kwa kupiga nchi zote zinazoendelea kushikilia itikadi Kali za kiislam au kikristo, kwa upande wa nchi za kikristo walishamalizana nazo Sasa zimebaki nchi za kiislamu kama Iran kwa kuwatumia vibaraka wake yani USA, UK, Israel, EU n.k
Kwa kifupi huyo ndio shetani mwenyewe je mtamuweza?
Kazi kwenu