Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kuna watu wamekuwa kero kama kelele za mbu karibu na sikio. Wanalinganisha mafanikio ya Raisi Samia na yale aliyofanya Raisi Nyerere enzi za uraisi wake. Wanashindwa kabisa kutambua Nyarere kama Raisi hawakuwa na wigo wa serikali kupata mapato alionao Samia hivi sasa. Leo hii ukilinganisha hela aliyokuwa nayo Nyerere kwa ajili ya miradi ya maendeleo huenda ni 15% tu ya fedha alizo nazo Raisi Samia.
Fikiria miradi michache tu ya Nyerere katika hali duni ya uchumi enzi hizo; TAZARA; bomba la mafuta kwenda Zambia; uanzishaji wa viwanda vya umma kama vya chai, viatu, nguo kama Urafiki, Mwatex, vinu vya pamba, vifaa vya kilimo, cement, nk; benki ya CRDB, NBC; ujenzi wa nyumba za National Housing nchi nzima; barabara ya Tanzam Dar es Salaam hadi Zambia; mpango wa elimu ya msingi kwa watoto wote UPE; Miradi ya umeme ya maji ya Mtera, Hale, Kidatu, Nyumba ya Mungu, Uwemba, Pangani; ujenzi wa Chuo Kikuu cha DSM; Chuo Kikuu cha Sokoine; Mzumbe IDM; Chuo Cha Ardhi, meli na vivuko vya taifa.
Pia ujenzi wa mahoteli ya Taifa kama Kilimanjaro; vyuo vya Elimu kama Chang'ombe, Tabora nk; IFM Dar; vyuo vya Kilimo kama Uyole na Tabora; vyuo utabibu; Shirika la Elimu Kibaha; Shirika la Ndege ATC; Shirika la Reli TRC na treni za abiria za kila siku; elimu bure hadi Chuo Kikuu; matibabu bure kwa watanzania wote; bomba za maji za jumuia bure (gati); wanafunzi kula bure shuleni na kusafiri bure kwenda likizo hadi Chuo Kikuu; serikali kumudu gharama za wote wanaostahili kwenda JKT kwa kujitolea au mujibu wa sheria; Kila Mbunge kupewa gari ya serikali; kumudu gharama za vita ya Kagera; Kumudu gharama za kusaidi Ukombozi wa Afrika, nk.
Sasa bado unataka kusema Raisi Nyerere hakufanya kitu japo yote haya kwa zile fedha ndogo za kodi na mikopo alizokuwa nazo?
Na ukitaka kujua kwamba Nyerere bado angemzidi sana Samia, leo hii katika mapatao tunayopata kama nchi, mweke Nyerere kama raisi wa nchi ndio ungefikiria tungekuwa wapi, ukitambua kwamba karibu 40% ya mapato ya nchi inapotelea kwenye mifuko ya viongozi kwa ufisadi.
Na kabla hujamlinganisha Raisi Samia na Raisi Nyerere kwa miradi ya Taifa, kumbuka utekelezaji huo wa miradi ni deni la taifa, na jiulize tumefikia wapi kwenye deni la taifa, na linganisha na Nyerere kama yale aliyofanya yaliathiri vipi deni la taifa. Kwani nani ambae akipewa mkopo wa shilingi Bilioni mia moja, atashindwa kujenga vituo kumi vya afya ili watu wamsifie anapiga mwingi?
Badala ya kuwasifia wananchi kwa uvumilivu kutokana na mzigo wa kodi wanazotozwa na deni la taifa wanalotwishwa kila mwaka, tunawezaje kuimba kupita kiasi nyimbo za kumsifia sifia mtu ambae anatumia hizo kodi na fedha zetu kuwa anatuletea miradi mingi? Kwa nini watu wanashindwa kuelewa jambo dogo kama Raisi Samia anatoa wapi hizo fedha za hiyo miradi? Zinatoka kwenye biashara ya familia yake?
Hatuna tatizo kama watu mmeamua kuwa chawa, lakini msiwe chawa wajinga wa kumlinganisha Raisi Samia na Raisi Nyerere katika kutekeleza miradi ya taifa. Miradi aliyofanya Nyerere ndani ya miaka 23 ya utawala wake kwa fedha ndogo alokuwa nayo, si rahisi kwa Raisi Samia kuitekeleza hata kwa fedha ya kodi na mikopo aliyonayo hata tukimpa miaka 30 ya kuwa raisi wa Tanzania bara!