Wewe si ukisema yanga atoki baada ya Azam kufanya yake nje ya uwanja? Imekuwaje Tena unamsifia Azizi ki?
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ( TMA ) tokea Mwezi wa Nne ( April ) mwaka huu Walitutangazia kuwa kuanzia tarehe 1 hadi 13 Mwezi huu Oktoba, 2023 kutakuwa na Mvua Kubwa ya El Nino je, imenyesha?
Mbona hamuwashushui na hamuwashangai kwa Tabiri yao kwenda ndivyo sivyo ila kwa GENTAMYCINE kusema Yanga SC itafungwa na Azam FC na haijafungwa na imeshinda mnanishangaa na Kunishushua?
Halafu mnaotokwa na Mapovu dhidi yangu kwa Tabiri yangu kwenda ndivyo sivyo huwa mnakuwaga wapi pale Tabiri zangu zingine zikitokea kama nilivyotabiri? Je, nilivyoandika huo Uzi wa Kuitabiria Yanga SC kufungwa na Azam FC niliwalazimisheni muiamini au niliwaiteni mje muisome?
Ukielewa tu maana ya Neno TABIRI ( NUJUMU ) wala hutopata Taabu na Kilichotokea jana ila ukiwa ni Mpumbavu, Mswahili na Mshamba utaendelea kutokwa Povu na GENTAMYCINE na ninachowaahidi tu ni kwamba sitoacha KUTABIRI Matukio mengine yajayo kama ikinipendeza.
Tokea Juzi NILITABIRI kuwa Simba SC itafungwa na Al Ahly FC katika Mechi yake ya marudiano ya tarehe 24 Oktoba, 2023 na Kutolewa katika Michuano mipya ya African Football League ( AFL ) hivyo nawasubiria TABIRI yangu hii ikitokea kama NILIVYOITABIRI mtakuja hapa JamiiForums kwa Kasi hii hii Kunipongeza japo najua kwa ROHO MBAYA ZENU wala HAMTOKUJA kwakuwa MLICHOKIWEKEZA Kwangu ni KUNICHUKIA, WIVU na UNAFIKI pekee.
Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!!!
Kuhusu kwanini nimemsifia Mchezaji wa Yanga SC Aziz K jibu lako analo
Ghiti Milimo au utalipata katika moja ya Neno lililoko katika Signature yangu la Game Changer sawa?
Ukiwa na Akili Kubwa ni raha mno tu.