Mnaomtetea Magufuli mitandaoni wengi wenu hamumjui vizuri, mnamfahamu juu juu tu

Sasa mwajuma ndara ndefu ukimuambia hii story anaona unamdanganya.

Anakuletea za kwake sijui walimu walikua wanafundisha vzuri, mara manesi walikua wanachoma sindano vzuri
Ni ujinga tuu umewajaa.Kiuhalisia huko mtaani kumechangamka kinaendelea awamu ya mama tofauti kabisa na awamu Ile ya bwana Jiwe.

Watu maskini mara nyingi hawana Cha kupoteza ndio maana Huwa wanapenda viongozi wa imla.
 
Kaka Lucas Mwashambwa vijana hawa una waambiaje..?
 
Mbona ata hawa wa sasa nao wanapenda kutuona sie tukiteseka.
Hiyo ni hulka ya mwafrica in general
 
Huyo Dereva ni mgogo, ndie alikuwa alimuendesha akiwa Rais. Kwao ni Mbande, njia panda ya Kongwa
 
Swala la vyeti fake nilimpongeza sana. Unakuta anaestahili kupata hiyo kazi anasota na mwenye cheti fake kwa kuwa ana refa yupo kazini.
Haya sasa vijana wameondokana na suala la unemployment?
Rais Samia ndiye kaajiri angalau. Big up
Yule jiwe alikuwa haajiri, hapandishi madaraja wala annual increment.
Nilifurahi sana kifo chake.
Katika watu ambao walifurahi ni askari wa wizara ya mambo ya ndani.
Baada ya kifo chake wote waliostahili kupanda cheo wakapanda.
Si askari tu hata watumishi wa kada zingine.
 
Magufuli the best president ever.
Msipomsema sema na negativity hamtoboi au?
Mmekosa content au?
Kila mkimchafua ndio anazidi kung'aa.
 
Magufuli hajawahi kukokesea. Hata mimi natamani niwe kama yeye
Magufuli akiwa wizara ya ujenzi ukilipwa pesa yako kama mkandarasi usipompa bahasha sahau tenda. Hajawahi kukosea?
Mameneja wa Mikoa na vituo wa taasisi zote zilizokuwa wizara ya ujenzi wasipompa mkono huna umeneja. Fanya tafiti acha uvivu. Waulize waliokuwa mameneja feri enzi zake watakuambia.
Issue ya kula futi moja kila upande wa barabara zilizokuwa zikijengwa na tarlnroad kisha pesa anaichukua yeye na mfugale ulikuwa unaijua?
Magufuli hajawahi kukosea eti.
Nyie watoto hamna akili
 
Kama Magufuli alichukia sana wizi je, kulazimisha apewe pesa za maziwa kila siku pale feri ni uadilifu?
Kula futi moja kila upande wa barabara zilizokuwa zikijengwa kisha pesa kugawana yeye na mfugale ni uadilifu?
 
Binafsi nilitamani adumu miaka yake 10, Ili mwishowe aje ajue hakuna alichoacha chq maana na mambo yatarudi kama alivo pokea.
Mkuu samahani lakini kama nitakukosea nikisema haya "kama huoni alichoacha Magufuli utakuwa lipumbavu la mwisho!" Mwamba angekaa miaka yake 10 nchi hii ingekuwa juu sana kwenye huu ukanda!
 
Mameneja wanateuliwa na Waziri?
 
Wakati mwingine hakuna rais anayefanya huo unyama wa kuteka na kuua watu, uchafu unafanywa na sisi wenyewe na anasingiziwa rais wa nchi.

Kutekana na kuuana ni tatizo la dunia nzima, Afrika ya Kusini kumejaa utekaji lakini Tanzania inayotazamwa kisiasa kila utekaji unahusishwa na siasa wakati hao wanasiasa wanaishi maisha ya kibinadamu kama binadamu wengine.

Binafsi siamini iwapo Samia anaweza kumteka mtu na kumuua hata kama vipo vikosi vya usalama wa taifa vyenye kuzifanya kazi hizo haramu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…