Kuna tatizo kubwa kchwani mwa mleta mada na hata Kabendera.
1. Rais wa nchi kufukuza wenye vyeti feki na kuondoa watumishi hewa ni kosa?.
Ilitakiwa wakamatwe wote na kupigwa kifungo cha maisha,na waliojipatia pesa kupitia watumishi hewa ilitakiwa kinyongwa had kufa, ila hakufanya hivo.
2. Ya kwamba alitaka kumbaka ....,unao uthibitisho toka kwa mhusika kuwa alitaka kunibaka?.
Au ulikuwepo kushuhudia hilo tukio?.
Na kama ulikuwepo,nani alikualika?.
3.Mara alikuwa katili kwa familia yake.
Ni mke wake au watoto wake ndo wamekupa hizo nyepesi au ni hisia zako?.
Au nawewe ulikuwa mmoja wa wanafamilia ya Hayati?
4.Mara katoke alifukuzwa kwa kuvuta bangi,bangi na kufukuzwa kwake shule wewe kama wewe vimekuathiri au vimekusaidia kivipi?.
Je ni mwl yupi wa katoke aliye mfundisha Hayati ambaye hadi Leo yupo aliyekupa huo ushahidi?..
5. Ombi kwa vijana wote wanaopitia mada humu jamii forum,kuweni na adabu kwa viongozi wa nchi,Rais si sawa na mjomba wako ama shangazi yako,Rais wa nchi ndo nembo ama kichwa cha nchi.
Uwe mwanasiasa kijana au nani ,heshimuni sana viongozi wa nchi hasa Rais.
Binafsi mjipange kama mnataka kumchafua Magufuli,vinginevyo huyo mtu atabaki kama lulu ya taifa hili ya kila kiongozi ajaye kuiga nyendo zake za kuwaletea wanyonge maendeleo.
Kabendera nakushauri,usitumike kama pampas au condoms na huyo jamaa,yeye hana cha kupoteza achana naye.
Angalia mambo yako utayamalizaje kwa mda tulionao sasa hivi.
Lakini kama wametoa mafungu makubwa ili umchafue mzee wa watu,tambua utarudi bongo na utakaa mitaani na wanyone aliokuwa akiwatetea Magufuli.
Kaa chini utafakari,je ulichokifanya ni sahihi?.
Bila kupokea hizo hundi je ungeweza kukifanya?.