Mnaonaje tubadili katiba yetu ili Rais Samia aendelee kuongoza Taifa letu baada ya kumaliza muhula wake 2030?

Mafanikio ya Raisi Samia na yale yote makubwa aliyoyafanya nimeshaandika sana humu jukwaani kwa kina na kirefu sana na kwa ushahidi murua

Endelea kutuhabarisha kuhusu hayo Mkuu maana kazi ya utume wake ndo kwanza inaanza, sio kuandika nyuzi za kusisimua hisia mseto kwa Jamii ya Watu makini kama hii. Rejea kauli ya Mheshimiwa J.K wa pili alielekeza Wana CCM namna ya kunadi sera na Mafanikio ya Chama kwa Wasioamini… kwamba Wanapoonyesha Dosari, na sisi tukazane kuonyesha mafanikio na sio kushindana nao kwa hoja zao.

Huwezi kumshinda Nguruwe kwenye mchezo wa kujipaka uchafu, hiyo tabia ipo kwenye vinasaba vya mwili wake. But unaweza kumburuza vizuri kwenye Game ya Wasafi. Stick to the Good Guys script Mkuu, you will never lose!!
 
Mawazo ya mwanadamu akishashiba ugali...

 
NI kiongozi mzuri ila kubadili katiba itafanya hata yeye akitoka atakayeingia atabadili katiba ili kujipendelea yeye na familia zao, katiba ibaki kama ilivyo kwa maslahi mapana ya nchi, when people start to deviate they dont know where to stop
 
Hilo ndo hitaji la wananchi wengi kwa sasa. Inabidi wabunge wafanye kitu pale kwenye katiba ili Mama aendelee kuongoza angalau hadi 2035.
Nadhani angeendelea mpk atakapoamua mwenyewe yaan ukomo wa mihura ufutwe kwanza utarudishwa baadae akimaliza
 
Hilo ndo hitaji la wananchi wengi kwa sasa. Inabidi wabunge wafanye kitu pale kwenye katiba ili Mama aendelee kuongoza angalau hadi 2035.
Kwanini Katiba iguswe kwenye hilo tu !? Mbona kuna mambo mengi sana ya kurekebishwa kuliko la kiongozi kuendelea kutawala?!
 
Dogo unapenda sana kupandisha watu hasira.
 
Kwa sasa watanzania wanataka Mama aendelee kuongoza Taifa letu. Maana chini ya uongozi wake wameona mafanikio makubwa yaliyopatikana na namna Maisha ya watanzania yalivyo badilika na kuwa yenye Matumaini makubwa sana .
Kila kitu kina mwisho, katiba ifuatwe.
 
Ukiona mwanaume anakubali kuongozwa na mwanamke ujue huyo mwanaume anamapungufu makubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…