Mnaopekua simu za wapenzi/waume/wake zenu huwa mnataka nini kifuate?

Mnaopekua simu za wapenzi/waume/wake zenu huwa mnataka nini kifuate?

Mshangazi dot com

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
1,345
Reaction score
3,503
Kuna binti kaja kwenye kikundi leo analia, jana mume karudi nyumbani amelewa binti kafungua simu amekuta meseji za kimapenzi za wanawake, picha za utupu kutoka kwa wanawake watatu na wawili kati yao ni wafanyakazi wenzake na mumewe. Asubuhi hii ameondoka nyumbani akaenda kanisani na hajaongea na mumewe bado.

Nina swali la msingi kwa wapekua simu: Hivi, mkiwa mnapekua hizo simu za wapenzi au wenza wenu, huwa mnafikiria na next step itakua nini? kama unahisi mume au mke anachepuka, je ukimkamata ni kweli anachepuka utafanyaje? au mnapekuaga tu ili umshike na kosa ila hujafikiria kitakachofuata.

Haya mshaurini huyu mwanamke mwezetu afanyaje maana haelewi cha kufanya. Ndoa ina miaka 8, wana watoto wawili, yeye ni mama wa nyumbani na kama familia wanajiweza kiasi kiuchumi.

Msisahau, kupekua simu ni kosa la jinai:
Screenshot 2025-03-01 at 13.57.18.png

View: https://youtu.be/y8jYZw60zPw?si=WOl6F_9z4FbSdgdN
 
Hawataki ku-share na watu baki haya maeneo 🙂
Screenshot_20250301-073445.png
 
Back
Top Bottom