Alhamdullilahi namshukuru Mola Muumba wa vyote kwa kunijaalia mafanikio ya kutunukiwa Degree ya Pili (2nd Dan) ya Sanaa ya Kujilinda kwa Mikono Mitupu ama Karate mtindo wa Jundokan Goju Ryu kutoka kwa Mwalimu wetu Mkuu wa @jundokan_tanzania Sensei @fundi_romi_ siku ya Ijumaa Juni 17, 2022.
ANGALIZO: Jamani ndugu zangu sanaa hii ni ya kujilinda kiafya, kiakili, kinidhamu na ki-utii na sio kupigana na mtu au watu. Ndio maana nina miaka takriban 40 nafanya Karate lakini hadi sasa ni wachache kweli waliojua nacheza sanaa hio.
Ni kweli kabisa sikupenda na sikuwa najionesha hadharani kwamba mimi ni Karateka, na hii kutoka hadharani sasa ni kuwatia moyo na hamasa watu wa umri wowote ama jinsia yoyote kwamba Karate ni sanaa ya kujilinda kiafya, kiakili na kinidhamu. Mie imenisaidia sana kwa kweli!
Ukikuta Karateka mbabe au mpenda shari basi tambua kuwa huyo jamaa ni aidha feki au hajaiva kisawasawa.
Kwa mwenye nia ya kujiunga nasi karibu DM kwa maelezo kamili.