Mnaopokea salary take home chini ya milioni moja, huwa mnawezaje kutoboa mwezi mzima?

Acha uongo wewe,watu wa G unajua mshahara wao konyo ww
 
Mzee umepangilia kikubwa sana
 
Umeme 15k mwezi mzima?
 
Watu wananuka madeni, msululu wa madeni ni mkubwa mno, ukigeuza kuwa Kilomita unaweza kukuta ni Dar to Mwanza..
 
Mimi take home yangu ni kama 1.29m hivi, lakini huwa sitoboi week mbili nakuwa nimefulia hatari.

Sasa nyie wenzetu mnaopokea chini ya 1m huwa mnawezaje kutoboa mwezi mzima?

Tupeane mbinu hizo wakuu.
Huku Niliko Nikiwa na Mchele na unga Ndani na Maji ya kunywa ya kutosha mejaza na Vinywaji na matunda kwenye Friji ya Kutosha na Pesa ya mboga za anasa (nyama, Kuku Kienyeji) kama 50k maana Umeme natumia Wa 9000 miezi hata 2 niko matumizi madogo Friji Halitumii Umeme sana Nililonalo na Liko On 24hr Ukiachana na Huu Mgao, mboga za Majani Huwa Nachuma Upenuni na Sio mdau wa kwenda club kulewa au kunywesha watu Bia Natoboa mwezi mshahara wangu ukabakia kiasi unapumua.
 
Kuna mwalimu wa sekondari anae pokea hiyo pesa kweli?
Kuna walimu wanapokea Take home million 1.5 Take home na anafundisha Sekondary na bado kustaafu miaka 10 mbele wapo wengi tu inategemeana na Elimu ya mtu na kafanya kazi miaka mingapi.
 
Mimi take home yangu ni kama 1.29m hivi, lakini huwa sitoboi week mbili nakuwa nimefulia hatari.

Sasa nyie wenzetu mnaopokea chini ya 1m huwa mnawezaje kutoboa mwezi mzima?

Tupeane mbinu hizo wakuu.
Tunatoboa kimizengwezengwe hadi tunajishangaa wenyewe.
 
Tunalima vijijini. Tunalima.mahindi na mpunga na maharage pia. Tunalima alizeti kwa ajili ya mafuta. Hii ni mwaka mzima sinunui nafaka wala mafuta.

Tunafuga ng'ombe wa maziwa kwa ajili ya kuuza maziwa na hela ya mboga mboga na sehemu nyingine inalipa ada ya watoto.

Unafuga kuku kwa ajili ya mayai na nyama kama mboga.
Na pia nalima mboga mboga ( matembele Chinese, bamia na ntole yaani mboga mseto eneo dogo.

Baada ya hapo nilipe mshahara huo mshara.
 
Subir siku ukose hyo kazi utajua watu huwa wanatoboaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…