Mnaosali KKKT bado mna imani na kanisa hili? Mbona migogoro imetamalaki?

Mnaosali KKKT bado mna imani na kanisa hili? Mbona migogoro imetamalaki?

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Migogoro ktk kanisa hili imeota mizizi na inakuwa sehemu ya utamaduni wa kanisa hili.

Ukiingia kwenye mitandao ukatfuta historia na taarifa za migogoro utakutana na lundo la migogoro iliyowahi kuripotiwa. Nitawakumbusha michache.

1. Wakati wa mgawanyo wa Dayosisi ya Pare na Mwanga maaskofu walimwagiana tindikali (acid). Huu unyama unaotisha unafaa kufanywa na kanisa?
2. Mwaka Jana walipotaka kuhamisha kiti cha uaskofu kule Dayosisi ya Konde kuliibuka timbwili la kufa mtu.

3. Dayosisi ya Mashariki na Pwani mchunganji Kimaro alisimamishwa kimagumashi kwa kupewa likizo isiyo na kichwa wala miguu kwasabb zisizofahamika mpk kesho. Ingawa taarifa za ndani zinasema ni maslahi ya kifedha.

4. Leo hii askofu wa Dayosisi ya Kusini amelazimishwa kustaafu baada ya mgogoro mkubwa uliosababishwa na matumizi mabaya ya fedha.

IMG_20230302_203253_279.jpg
 
PENYE WENGI PANA MENGI MIGOGORO NI SEHEMU ya MAISHA
 
Migogoro katika kanisa haikunza leo wala jana, tokea enzi za mitume wa Bwana Yesu na wafuasi waandamizi wa Yesu walihitilafiana sana
 
Hata kwenye maisha ya kawaida, Kama ni mtumishi wa umma fanya maendeleo makubwa utashangaa takukukuru wanakufuatilia Mara wezi, wachawi, wapiga fitna n.k, lakini ukikaa tu Kama zombi/teja hutakuwa na mgogoro wowote
 
Ni kweli ila hiyo haituhusu tupo tu ili mradi Kuna mchungaji wa kutongoza misa yasiku hiyoo
 
Hao ndugu nao wanatia aibu, tusichoke kuwashauri kuacha migogoro. Kama vipi wagawanyike tu kila mwenye nguvu ya ushawishi akaanzishe kanisa lake kuliko kubaki hapo na kulinajisi kanisa kwa migogoro
 
Hata kwenye maisha ya kawaida, Kama ni mtumishi wa umma fanya maendeleo makubwa utashangaa takukukuru wanakufuatilia Mara wezi, wachawi, wapiga fitna n.k, lakini ukikaa tu Kama zombi/teja hutakuwa na mgogoro wowote
Migogoro haipaswi kutokea kwa Wana w Mungu
 
Kanisa la KKKT linasumbuliwa na mambo matano makubwa 1. UDINI 2. UKABILA 3. UFISADI 4. WIZI .5 RUSHWA
 
Kanisa hili lina majivuno sana kisa limejaa wachagga wa marangu na machame pamoja na wameru yaani wanajisikia sana hawa. Mi mkatoliki nawachabo tu😄
 
Kanisa la wachaga. Migogoro kwa sababu ya pesa na mali lazima iwepo
Chuki dhidi ya wachaga haikusaidii na huwawezi wenzio waliwachukia kafa kawaacha disemba kama Kawa moshiiii!!
 
Back
Top Bottom